Asante sana mkuu...naona leo ulikuwa na hamu ya kutukana na kweli umefanikiwa.....
Ninachokukumbusha ni kwamba aliyekujaalia wewe mgao wa escrow ndio katunyima sisi....wakati wewe unawaza ule chakula cha aina gani ,wengine tunawaza tutakula nini maana tumakula tunachopata na sio tunachotaka....
Wakati wewe unatupa chakula kilicho lala.....
Kuna mtu mwingine anakufa na njaa....
Wakati wewe unamnunulia kimada wako zawadi ya gari, kuna mtu anakaribia kukata roho kwa kukosa hela kwa ajili ya matibabu......wakati wewe unamwagilia maua maji safi na salama kwa kunywa ,kuna mtu anakunywa maji ya mtaroni.....
Ninachokukumbusha ni kwamba duniani hatulingani........hayo maneno uliyoyaandika ni ya mtu aliyevimbiwa na shibe na kamwe hatamkumbuka mwenye njaa.....wakati wewe unanishangaa kumaliza mwaka wa tatu kudunduliza hela ya baiskeli kuna watu wanamaliza mwaka wa nne wanatafuta hela ya kandamabili.......hii ndio dunia....