Hata mimi. Hivi kuna rafiki yangu naye yupo katika process ya kuwekeza katika kupiga story akaniambia katika usimamizi wa kazi zake atamuweka ndg yake mtoto wa mama yake mkubwa nimemshauri usithubutu kabisa japo kamfagilia sana yule ndg katoka chuo anajua kila kitu nimemwambia heri hata mtu baki ukikoswa warudi au mtu yeyote wa nje.
Mwambie asijaribu hata kidogo, huyu ndugu yake labda amfanye kibarua tu lakini sio kuwa mtendaji mkuu, ataumia.
Mwaka 2016 Kuna dogo nilikuwa nafanya nae biashara ya samaki na dagaa kuwatoa mwanza kuwapeleka Dar, mtaji ulikuwa wangu, yule dogo ni mtoto wa rafiki wa karibu wa bimkubwa wangu, yaani mama zetu ni watu walioshibana na wanatoka sehemu moja, hivyo tulikuwa tunachukuliana sisi ni kama ndugu.
Mimi kazi yangu ilikuwa ni kununua mzigo huko mwanza maeneo ya mwaloni na kisha kumtumia ambapo yeye kazi yake ilikuwa nj kusambaza tu Kwa wateja na kukusanya hela basi, na uzuri soko la dagaa siku zote huwa lipo tu wateja sio wa kutafuta sana.
Hili kumfanya afanye kazi kwa moyo mmoja na asijhisi kama namnyonya kwa namna yoyote ile, faida iliyokuwa inapatikana tulikuwa tunagawana 50/50.
Nakumbuka kipindi hicho tulikuwa tunauza kwa kilo ambapo kilo Moja ya dagaa tulikuwa tunauza 4,000/= na samaki ilikuwa ni 2,600= au 1,700/= kunategemea na aina ya Samaki, na mzigo wetu ulikuwa haukawii yaani ukifika tu ndani ya siku Moja unagombaniwa na wateja.
Sasa basi tumefanya kazi vizuri KABISA miezi kama minne ya mwanzo, baadae mwenzangu akaja akaniambia tuachane na samaki tudeal na dagaa tu ndio zinaenda kwa haraka, na kweli nikakubaliana na wazo lake hivyo tukawa tunafanya uchuuzi wa dagaa tu basi.
Kumbe bwana mwenzangu huku tayari siku nying sana alishanizidi akili. Miezi yote hiyo tunafanya nae kazi Mimi najua dagaa anauza 4,000/=per kg kumbe mwenzangu alishawapandishia wateja bei ya daga siku nyingi sana anauza kilo moja 5,500/= na Mimi Sina taarifa yoyote.
Kwa hiyo kumbe hata faida tuliyokuwa tunagawana nae ni ile iliyokuwa inatokana na hesabu ya 4,000@kg..... Imagine na nilikuwa namtumia mpaka mzigo wa 300kg kwa wiki, kwa hiyo yeye alikuwa ananufaika zaidi yangu Mimi Tena kwa kiasi kikubwa sana kwenye biashara ambayo Mimi ndio nilimkaribisha na ndio nilitoa capital kwa 100%.
Kwa baadae nikajagundua kumbe hata lile wazo lake la kutaka tuachene na samaki kisha tudeal na dagaa tu ni kwa Sababu ya hiyo bei aliyokuwa ameongeza kinyemera nyemera kwenye dagaa, kwenye samaki haikuwa rahisi na pia wateja wa samaki walikuwa sio wengi sana kama wa dagaa.
....niliwaza sana siku nilivyogundua dogo ananifanyia mchezo mchafu kiasi kile, yaani licha ya Mimi kuweka mgao sawa wa faida lakini Bado alitafuta njia ya yeye kunufaika kuliko Mimi, siku hiyo ndio niliamini binadamu(hususani mbongo) hawafadhaliki hata kidogo.
Kwa hiyo na huyo jamaa mwambie aache kabisa ujinga wa kuamini amini ndugu, huyo ndugu yake mwambie amfanye kibarua wa kuwa anamwagilizia tu basi.