Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

Dar ni jiji la kibiashara la Tz ...huwezi linganisha na hao wengine
 
Dar Es Salaam litabaki kuwa kuwa Jiji kubwa katika nyanja zote Kwa miaka mingi ijayo katika nchi hii
 
Waziri wa viwanda na biashara Selemani Jafo ametembelea na kukagua viwanda viwili vya Magari na mafuta Mjini makambako na kuwahakikishia usalama wa mitaji yao ambayo itaongeza uchumi wa taifa.

Viwanda vilivyo tembelewa ni pamoja na Kiwanda cha Mafuta ya Parachichi cha AVO AFRICA ambacho tayari ujenzi wake umekamilika pamoja na kiwanda cha Utengenezaji wa Magari ambacho ujenzi wake umeanza rasmi na kinatarajia kutumia chuma cha Liganga na Mchuchuma kitakachoanza kuchimbwa wilayani Ludewa mapema mwaka huu.

Waziri Jafo amesema, kukamilika kwa viwanda hivyo viwili kutatoa fursa ya Ajira, Mapato kwa serikali pamoja na kupunguza ombwe la uagizaji wa bidhaa kutoka nnje ya nchi, yakiwemo mafuta.

Wakazi wa Mkoa wa Njombe na mikoa jirani wanasema, Uwekezaji uliofanyika unatoa fursa si tu ya kukuza sifa ya Mkoa bali uchumi, ajira na maendeleo ya Taifa katika sekta ya viwanda.

Ikumbukwe kwamba viwanda hivyo vyote viwili vinatarajia kutumia malighafi zinazopatikana mkoani Njombe yaani Chuma cha Liganga pamoja na Parachichi ili kuongeza mnyororo wa thamani katika malighafi hizo.

#StarTvUpdates
 
Makambako steel industrial park ni mwendelezo wa kuufanya mji mkubwa wa viwanda na biashara nyanda za juu kusini
 
JPM angekuwepo mpaka leo kule Dsm watu wangekuwa wameshapungua sanaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…