Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

Nimezaliwa na kukua Dar ila ni pamawaida sana labda kwa idadi ya watu na bandari ila kama umetembea miji ya Nairobi N. K ndio utaamini na kujua kwamba maendeleo sio bandari tu
Na bandari Ipo moja ya mombasa tu still Nairobi imeipiku Mombasa Sasa bongo bandari zipo tatu. Huku ya tanga ishaanza kuchanganya. Na ya mtwara ikiisubiri Ile ya mbambabay bado Kuna mtu anakaza fuvu.
 
Quantity au quality? wengi kweli halina ubishi ila wenye uwezo kwa maana purchasing power labda 30% tu population. Dar maeneo yenywe watu wengi ni maneneo maskini sana uwezo wakununua sigara moja moja na mafuta ya kupima.
Yaani mda mwingine mi nashangaa mtu analipwaje elfu tatu, nne, Tano kutwa nzima. Kuna mikoa ukitangaza Hilo dau mikoa mingine hiyo kazi unaweza fanya mwenyewe.
 
Aaah! Wakazi wa daslam hivi mbona nyie ni wabishi sanaView attachment 2895951
Screenshot_20240206-130708.jpg
 
Haya sasa Mtwara[emoji95][emoji95][emoji95][emoji95]
 
Ukitaka kujua kama Kuna siku dar itapigwa bao, Angalia taarifa ya uwekezaji kwenye kituo Cha uwekezaji TIC . Uwekezaji unaofanyika nchini zaidi ya 85% unafanyika Dar na Pwani.Na ukisema Dar kwa Sasa hivi hauwezi itenganisha na pwani.Kwa hiyo siyo rahisi Dar kuwa nyuma au kuzidiwa na Mkoa wowote.
 
Wakuu ni hivi kutokana Hali ilivyo sasa naona kuna kila sababu ambayo itaitoa Dar kama namba moja katika swala Zima la uchumi. Sababu ni hizi.

1. Kuhamishwa Kwa ikulu na ofisi za Serikali. Hii imepunguza idadi kubwa ya watu ambao wangelazimika kusafiri na kuwepo mjini Dar. Hivyo imepunguza wananuzi wa mahitaji na huduma mji Dar es Salaam.

2. Ujenzi wa SGR ya Dar Hadi Dodoma hii itapelekea kuhamishwa kwa viwanda vingi kwani vikiwepo Dodoma kutakuwa na urahisi wa usafirishaji wa mizigo na magarifi kutoka mikoa mingine. Pia viwanda vingi vitapenda kuwa karibu na ofisi za Serikali.

3. Ujenzi wa miundo mbinu Bora Kwa mikoa mingine Kwa kipindi kifupi kilichopita tumeshuhudia ujenzi wa miundo yenye tija Kwa mikoa mingine Mfano mpango wa upanuzi wa bandari ya Mtwara na ya Mbambabay pia ujenzi wa reli ya Mbambabay Hadi Mtwara. Kwa hiyo baadhi ya mizigo itapungua bandari ya Dar pia baadhi ya viwanda vitajengwa huko Mtwara.

4. Ukuaji wa science na technology Kwa Sasa rasilimali nyingi ambazo zilikua hazivuniki lakini Kwa Sasa Kwa mashine za kisasa za bei nafuu. Zimefanya hata wazawa na wageni wakizitumia kuvuna rasilimali zilipo mkoani Mfano Iringa kumekuwepo na viwanda vingi vya playwood ambavyo Kwa Sasa vingi vinamatawi Njombe hivi vimeifanya Dar kupunyuliwa mkiani Kwa uchumi na Iringa na uwepo wa solar na bodaboda n.k umefanya watu waweze kulima hata sehemu za mbali.

5.Ukuwaji wa center nyingine za kibiashara kama vile Mwanza, Makambako na Dodoma kutapunguza umaarufu wa Dar.

Karibu Kwa mjadala
Hivi kwani Dar ina maajabu gani yani kwa mfano? Dar ni mji wa hivyo sana, Dar utaiona ya maana kama haujatoka nje ya nchi. Ukitembea utaiona ni Jalala tu, mipangilio ya miundombinu, hovyo, huduma za kijamii shaghalabaghala, Dar ni takataka tu linalobebwa na serikali.
 
Kupitia maboresho haya Kuna centre zinaenda kukua zaidi kibiashara kama makambako mikoa ya iringa,njombe,ruvuma na baadhi ya wilaya za mbeya zitachukulia mizigo hapo mabus yanaenda kupungua na maroli ya mizigo wachina lazima waende kibiashara zaidi
425861739_376953388376876_3050052746144727492_n.jpg
 
Wachina kazi washajua fursa ziko wapihttps://www.facebook.com/100064759594121/posts/pfbid031tXHpMd8QJgVfWR9FwETprDWyQai5U7z9Dx5YNLNo2SNwuV5rqxYjLAxB6ULntadl/?app=fblhttps://www.facebook.com/100064759594121/posts/pfbid031tXHpMd8QJgVfWR9FwETprDWyQai5U7z9Dx5YNLNo2SNwuV5rqxYjLAxB6ULntadl/?app=fbl
 
Kwa mabadiliko ya kimiundombinu kama sekta ya reli tukubaliane lazima Kuna centre za miji zinaenda kukua zaidi kibiashara na dar Kuna vitu vinaenda kupungua Sana mfano centre zinazoenda kukua zaidi ni dodoma ,makambako,,mwanza hii ni kutokana na ujenzi wa hizi rel I miji hii lazima fursa zinaenda kuongezeka maana watu wengi watatumia treni kusafirisha mizigo yao na hizi centre mikoa mingi itachukulia mizigo yao na ndio maana tayari maeneo husika yamesha Tenga maeneo ya bandari kavu shida ya watu wanabeza Hawa fatilii mambo yanavo Enda tazara inaenda kuwa chini ya mchina na Hawa wapo kibiashara zaidi na tayari ukienda makambako huko wanafungua maviwanda ya kutosha wanajua kinacho fuata
View: https://www.facebook.com/100064759594121/posts/pfbid031tXHpMd8QJgVfWR9FwETprDWyQai5U7z9Dx5YNLNo2SNwuV5rqxYjLAxB6ULntadl/?app=fbl
 
Back
Top Bottom