Usiweke Sheria tuongee fact Kwamba Nini? Ambacho Kwa Sasa Dar itaendelea kua nacho Cha kipekee
Mkuu, kwanza elewa Dar ni moja,
Uwanja wa Ndege,
Embassies zote zipo Dar, hazihamii Dom leo wala kesho,
Ikulu bado issue nyingi zipo Dar,
Vyuo vikuu vingi vipo Dar, UDSM, MUHAS, NIT na ujue hiv ndio vyuo % kubwa ya wanafunzi wa Tz wanataka kusoma hapo, hapo sijataja lundo la vyuo vikuu vingine, hiv vya diploma vipo vingi kuliko idadi ya secondary za hapo Dom,
Miundombinu, wengi wanajitahidi ila Dar kawaacha mbali mno
Utajiri wa mtu mmoja mmoja, Tazama kwenye ile list ya per capital Tz kimkoa, DSM analead kwa mbali na pia ndio ambae pato lake linakua kwa kasi kuliko mkoa wowote ule
Population, population ya city center ya Dar ni 5M+, mji unaokaribia una 1M, utaona ni jinsi gani gape lilivyo kubwa sanaaaa
Ueleww wa mtu mmoja mmoja, mkoa wa Dar ndio mkoa wenye watu wenye kiwango kikubwa cha elimu kuliku mkoa wowote Tz hii,
Fursa za biashara, hapa population na kuwa mkoa tajiri zaidi unaifanya dar iendelee kuwa makao makuu ya biashara Tz kwa muda wa miaka mingi ijayo
Center ya burudani na starehe, No way utaitoa center ya mziki, filamu na mpira kutoka Dar kwenda mkoa wowote ule Tz ndani ya miaka 50 ijayo,
Ukiona hizo point zote na nyingine nyingi sanaaaa, utakuta ona hizo center zitachangamka ila hazitafikia Dar leo au kesho au within our lifetime