Hiyo Dar yenu inapigwa bao siku si nyingi

Mleta mada hivi unajua kuwa kwa sasa zaidi ya 40% ya pato la taifa linazalishwa na Dar pekee.
Sasa ni vipi Dar ididimie halafu huko maporini paweze kuinuka?
Wewe fahamu tu, Ubongo, Uti wa mgongo na moyo wa taifa la Tanzania ni Dar, bila Dar hii nchi kiuchumi haiwezi kuikaribia hata Sudani kusini wala Burundi.
 
Umeona wawekezaji bado wanapendelea maeneo yaliyo karibu na bandari

Ndio maana kumekuwa na uwekezaji mkubwa wa viwanda mkoa wa Pwani hasa hapo Kibaha na Bagamoyo kwa sababu ni karibu na bandari ya Dar
Waliwekeza hivyo kutokana na watu wengi walikua dar na malighafi nyingi zilikua zinakuwa imported we fikilia kama tu makaa ya mawe nayo yalikuwa imported kutoka sauz afrika. Sasa kwanini wawekezaji wajenge mbali na dar lakini for now mambo ni tofauti kutokana na machine za kichina za bei nafuu kama vile xcmg , snlg watu hata wengine ni wazao wanajishughulisha na uchimbaji madini na uvunaji resources.
 
Sio waliwekeza yaani tunapoongea sasa hivi mkoa wa Pwani viwanda vinajengwa kwa kasi sana.

Hatuzungumzii wakati uliopita tunazungumzia kinachoendelea sasa
 
40% ya Pato la taifa? Mkuu sources please
 
Sio waliwekeza yaani tunapoongea sasa hivi mkoa wa Pwani viwanda vinajengwa kwa kasi sana.

Hatuzungumzii wakati uliopita tunazungumzia kinachoendelea sasa
Mkuu hiyo nikawaida kutokana viwanda vingi vya hapa bongo vinategemea marighafi kutoka nje lakini Kwa siku zinavyo zidi kwenda uvunaji wa malighafi unakuwa Kwa Kasi hivi we fikilia kama mradi wa ludewa ukikamilika sidhani kama kunamwekezaji atajenga kiwanda Cha nondo dar au pwani. Viwanda vikubwa sikuzote hufuata Cha kwanza huwa ni malighafi kiwanda Cha mufundi paper na dangote vimeprove haya.
 
Unaongea ukiwa mkoa gani kwanza maana km ungekuwa dar usingethubutu hata kuwaza kuandika hii thread..
 
Njoo ukae mjini hata Mwaka mmoja utajiona jinsi gani ulivyoandika pumba hizi.
Yaani Nije huko ambako vijana wenzangu walioko huko wanaomba niwakope elfu tatu ya kula. Nije huko ambako vibarua wanalipwa elfu nne Kwa siku. Nije huko ambako mtu mpaka anazeeka Hana nyumba.
 
Yaani Nije huko ambako vijana wenzangu walioko huko wanaomba niwakope elfu tatu ya kula. Nije huko ambako vibarua wanalipwa elfu nne Kwa siku. Nije huko ambako mtu mpaka anazeeka Hana nyumba.
Kumbe unadeal na watu wenye kiwango hicho cha maisha, ndio maana umepuyanga.
 
Nakataaa...........bado sana ..........hebu nitajie mtu au watu au taasisi au kikundi kinachomiliki rolls loyce curinan? Huko mkoani? Je bahkresa wa mkoani yupo? Masham love minyonyo yupo huko? Wale wanao oga barabarani pia huko mkoani wapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…