Hizbullah wazirusha tena na Syria waanza kuionya Israel

Hizbullah wazirusha tena na Syria waanza kuionya Israel

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Leo tena maroketi kadhaa yameruswa uwelekeo wa kaskazini ya Israel na kumfanya waziri wa ulinzi wa Israel atoe onyo na vitisho kwa serikali ya Lebanon.
Kuonesha ya kuwa maroketi hayo baadhi yametua na kupiga yalipokusudiwa,waziri huyo amesema madhara yanayoipata Kiryat Shmona basi yataipata na Beirut pia.
Kwa upande wa Syria baada ya kimya cha muda mrefu huku wakishambuliwa mfululizo,utawala mpya ya Syria umeionya Israel iache kuua raia na kuendeleza kupiga maeneo ya nchi hiyo kwa kutumia visingizio visivyo na msingi.
Onyo hilo linafuatia hapo juzi kushambuliwa kwa maeneo ya kusini ya Syria na kuua raia 6 huku jeshi la Israel likisema kuna watu waliwarushia risasi askari wao wanaokalia maeneo hayo.
 
Back
Top Bottom