Hizi gari hapana, nitabadilishana na Bodaboda

Hizi gari hapana, nitabadilishana na Bodaboda

Well said..
Wachangiaji wengi wanaochangia kishabiki kwenye huu uzi hawana magari..

Maana ya kuwa na gari si muonekano..
Ni namna gani gari hilo linatatua shida zako za kiusafiri au uchukuzi wa mizigo ya hapa na pale...

Suala la muonekano huwa ni la mwisho kabisaa..
Huu uzi ukiuchunguza kwa kina utagundua wachangiaji wengi ni wapanda daladala, bodaboda na wale wachache wanaomiliki magari ya urithi.

Wale wenzangu na mimi waliojipinda na kununua hizo passo, suzuki, funcargo, nk. wametulia kimya huku wakishangaa nini hasa lengo la huu uzi! ni kejeli tu, kujimwambafai, sizitaki mbichi hizi, au!!!
 
Sijawahi kujutia uwepo wangu humu jf...[emoji23][emoji23], Maana.....
Wasomi nyie,
Matajiri nyie,
Wenye magari nyie,
Wenye wake/wame wazuri nyie,
Mlio kamilika/msio na mapungufu nyie,
Jf hata mimi inanichekeshaga sana kila mtu yuko juu na kila mtu ni mbabe yaani hakuna mnyonge.
Yaani ukisema uwasikilize mikwara yao unaweza ukajiona hauna maisha kabisa.
 
Kama usafiri wa gari unao sawa kejeli. Ila kama unagombaniaga daladala na unakejeli basi upo kwenye hatari ya kugombania daladala maisha yako yote. Maisha ni step, kuwa kwanza na usafiri ndo uuchukie ili upande zaidi.
Kuanzia mleta mada mpaka wanaomsupport hakuna hata mmoja anaemiliki gari.
Gari muhimu sana haswa sisi tunaoishi mjini unakuta mmelundikana watu kibao kituoni mnasubiri daladala.
Anapita jamaa na Passo yake kafunga vioo yupo peke ake ndani mwendo mdogo mdogo wewe upo kituoni toka saa 12 jioni mpaka saa tatu usiku unakimbilia daladala ukiingia ndani limejaa unashuka chini unasubiri lingine tena mwendo huo huo ukizubaa hata simu unaweza poteza.
Sasa lwa nini usimuonee wivu mwenye Passo maana mwenzio dakika tano tu kashafika kwake kajipumzikia wewe upo kituoni unahangaika kutafuta daladala. Mimi natafuta ela nianze na hizo wanazoita baby walker.
 
Kila la kheri mkuu!
 
Jf hata mimi inanichekeshaga sana kila mtu yuko juu na kila mtu ni mbabe yaani hakuna mnyonge.
Yaani ukisema uwasikilize mikwara yao unaweza ukajiona hauna maisha kabisa.
Hahaha...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwamba "unaweza ukajiona kama ni wewe tu ndie umechoka"....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hahaha...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwamba "unaweza ukajiona kama ni wewe tu ndie umechoka"....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ndio hivyo mkuu.
maana kwa mfano ukiwaelezea kuhusu mshahara wako watajitokeza watu na kusema wanapata mara 10 ya wewe,na watajitokeza wengine na kusema huo mshahara wako wanaingiza kwa siku moja tu.
Lakini ukifuatilia uhalisia kumbe hata elfu 10 hana.[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom