Hizi gari hapana, nitabadilishana na Bodaboda

Hizi gari hapana, nitabadilishana na Bodaboda

Tusubiri kiwanda cha kutengeneza magari cha nyumbu kitengeneze gari Kali kuliko hata v8.
 
Huu uzi ukiuchunguza kwa kina utagundua wachangiaji wengi ni wapanda daladala, bodaboda na wale wachache wanaomiliki magari ya urithi.

Wale wenzangu na mimi waliojipinda na kununua hizo passo, suzuki, funcargo, nk. wametulia kimya huku wakishangaa nini hasa lengo la huu uzi! ni kejeli tu, kujimwambafai, sizitaki mbichi hizi, au!!!
Until a man akijua uchungu wa kusave money step by step and kukukua his own car na his own cash (Isiyo na mkopo) na aweze kulihudumia monthly.. ndo aje hapa atukane magari ya wengine.. aiseee i agree with you here ni comments za wapanda daladala, gari za urithi na za kuhongwa na wanawake ndo wanacoment ujing ujinga hapa

Kila mtu anabuy gari kutokana na mahitaji yake.

Fun Cargo - ina nafasi kubwa ya mzigo ndani.. mfano mtu kama electrician inamfaa sana vifaa vyake anaweka ndani vyote na mengineyo

Etc.. etc..
 
yani wewe ukijijua ni masikini alafu una jeuri...basi sahau kununua hata baiskeli ya mataili manne.....kama hawa masikini wa humu.....
 
Nyingine hiyo
 

Attachments

  • IMG_20200718_170837.jpg
    IMG_20200718_170837.jpg
    34.7 KB · Views: 9
bora ninunue sedan yoyote kuliko gari hizo
 
halafu wanakuwa na viherehere sana,mziki mnene afu gari dogo,kwa jinsi wasivyokuwa na aibu wanashusha vioo,bora nikomae na noah yangu japo ni ya urithi
 
Wengi ulioandika kwa kuponda hizo gari huenda hamna hata magari, mnaendesha magari ya ndugu zenu au mnaulimbukeni fulani wa kumiliki gari. Ngoja niwape somo kidogo hapa hapa.

-Kila muundo wa gari ulibuniwa kwa kwa kuzingatia sababu maalum au mahususi. Ikiwemo fashion, ushindani wa kibiashara, Usalama, Speed, Mazingira, Uhitaji, gharama, jamii nk.

-Muundo wa gari unaokuvutia wewe haina maana ndio kila mtu unamvutia hivyo hivyo na vice versa hivyo hivyo.

-Gari binafsi ni sehemu ya maisha binafsi ya mtu. Ni vigumu sana kujua msukumo wa mtu binafsi kujua ni kwa nini amemiliki gari fulani.
 
Dream Car yangu Mimi ni Harrier haijaloshi Old au New model napigana usiku na mchana niipate, Nina miaka mitano serikalini toka niajiriwe lengo langu ni Ndani ya hii miaka mitano ya mwisho ya JPM niinyakue haijalishi kwa mkopo wa Bank au cash yangu binafsi
Usisahau pia, kumiliki Harrier ni jambo moja, na kulihudumia (fuel& services) ni jambo lingine tofauti kabisa. Hivyo jipange kwa vyote. Hayo magari yaone tu barabara hivyo hivyo, lakini furaha au maumivu yake yapo mioyoni mwa wamiliki wake.
 
Huu uzi ukiuchunguza kwa kina utagundua wachangiaji wengi ni wapanda daladala, bodaboda na wale wachache wanaomiliki magari ya urithi.

Wale wenzangu na mimi waliojipinda na kununua hizo passo, suzuki, funcargo, nk. wametulia kimya huku wakishangaa nini hasa lengo la huu uzi! ni kejeli tu, kujimwambafai, sizitaki mbichi hizi, au!!!

[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji16][emoji16] Na wote walokupa hizo likes40 ni wenye hayo Magari wamefurahi kweli wamepata mtetezi
 
Dume zima juzi namkuta anaendesha kapasso[emoji3][emoji3]

Mkuu mbona wanawake wanaendesha Range Benz hadi basi ya mkoani tatizo liko liko wapi ndo uwezo wake ulipofikia sasa na nyumba je ukisikia anakaa kwenye kajumba cha vyumba viwili pia utamcheka kwa maana ajenge nyumba ya gorofa usitucheke na vigari vyetu.
 
Ukistaajabu ya Porte utakuwa hujakumbana na Passo short chasis. Juzi kati kamenipita ka passo milango miwili nilijikuta natema chini

Gari ni kama nguo, wewe unapenda suti mwenzio cadets, wewe unafia kwenye jeans mwenzio suruali za vitambaa!

Hali kadhalika huwezi kumtaka fundi gereji avae suti na kazi yake unaijua, ndiyo hivyo hivyo huwezi kumlazimisha afisaa wa benki kuvaa overrall kazini kwake kisa wewe unashindia hilo!

Wananzengo, wanasahau kuwa kumiliki gani kuna factors nyingi!
1. Matumizi
2. Gharama za uendeshaji
3. Mazingira
4. Uchumi

Mazingira na shughuli zangu yanaruhusu mimi kutumia Passo, unawashwa nitumie VX! Una akili mzuri?

Pengine nikitumia VX hasara natumia Passo kumaintain faida!

Uchumi / kipato changu ni cha kuweza kumudu Vitz wewe unalazimisha nitumie Kluger, akili ipo sawa sawa?

Wewe una watoto sita utawaza noah au gari yoyote seven seater, sina mtoto sina mke! Ninunuea noah ya nini? Nikiingia zangu gheto nachomoka misele yangu midogo midogo mjini hapa, nitafute brevis ya nini?

Sina safari ndefu, wazazi naingia hapo Mbagala nawaona narudi zangu Tandika, nitafute gari engine kuubwa ili iweje? Kaangalia matumizi yake, inamtosha maisha yasonge mbele.

Tatizo waswahili tunaiga sana na kupenda kujikweza hata tusipostahili!

Hii nakupa ni Live story! Ndugu yangu kabisa, alinicheka sana mimi kununua terios kwa kujinyima yeye akiwa hana gari akaja kununua kluger kwa kukopa kupitia mshahara! Madai yake hawezi kuendesha 'vibebi woka'

Kumbuka mshahara unapungua kukata mkopo na umeongeza matumizi ya mafuta, kilichotokea haikupita miezi sita! Ana madeni kila kona ya 20,000 au 50,000.

Gari inatembea wiki moja baada ya mshahara, wiki zingine tatu anaomba lifti gari ipo home anashindwa kumudu gharama za uendeshaji!

Aliuza kluger akanunua porte sasa hivi anafurahia maisha mwaka wa pili sasa, kila siku gari ipo njiani na madeni hana tena!

Hapo akaelewa logic yangu kwa nini nilitafuta gari ya uwezo wa chini! Unatoka Pugu karibu na Chanika, unafanya kazi posta unataka uwe unasukuma Kluger kila siku lazima ufe kwa mawazo!

Kila mtu aangalie matumizi na kipato chake, kama wewe umejaaliwa kuwa na kipato kikubwa shukuru Mungu lakini si kusema ulimtema mtu mate chini kwa kumuona yupo kwenye passo! Mitandao isiwafanye mkufuru Mungu!
 
Back
Top Bottom