Gari ni kama nguo, wewe unapenda suti mwenzio cadets, wewe unafia kwenye jeans mwenzio suruali za vitambaa!
Hali kadhalika huwezi kumtaka fundi gereji avae suti na kazi yake unaijua, ndiyo hivyo hivyo huwezi kumlazimisha afisaa wa benki kuvaa overrall kazini kwake kisa wewe unashindia hilo!
Wananzengo, wanasahau kuwa kumiliki gani kuna factors nyingi!
1. Matumizi
2. Gharama za uendeshaji
3. Mazingira
4. Uchumi
Mazingira na shughuli zangu yanaruhusu mimi kutumia Passo, unawashwa nitumie VX! Una akili mzuri?
Pengine nikitumia VX hasara natumia Passo kumaintain faida!
Uchumi / kipato changu ni cha kuweza kumudu Vitz wewe unalazimisha nitumie Kluger, akili ipo sawa sawa?
Wewe una watoto sita utawaza noah au gari yoyote seven seater, sina mtoto sina mke! Ninunuea noah ya nini? Nikiingia zangu gheto nachomoka misele yangu midogo midogo mjini hapa, nitafute brevis ya nini?
Sina safari ndefu, wazazi naingia hapo Mbagala nawaona narudi zangu Tandika, nitafute gari engine kuubwa ili iweje? Kaangalia matumizi yake, inamtosha maisha yasonge mbele.
Tatizo waswahili tunaiga sana na kupenda kujikweza hata tusipostahili!
Hii nakupa ni Live story! Ndugu yangu kabisa, alinicheka sana mimi kununua terios kwa kujinyima yeye akiwa hana gari akaja kununua kluger kwa kukopa kupitia mshahara! Madai yake hawezi kuendesha 'vibebi woka'
Kumbuka mshahara unapungua kukata mkopo na umeongeza matumizi ya mafuta, kilichotokea haikupita miezi sita! Ana madeni kila kona ya 20,000 au 50,000.
Gari inatembea wiki moja baada ya mshahara, wiki zingine tatu anaomba lifti gari ipo home anashindwa kumudu gharama za uendeshaji!
Aliuza kluger akanunua porte sasa hivi anafurahia maisha mwaka wa pili sasa, kila siku gari ipo njiani na madeni hana tena!
Hapo akaelewa logic yangu kwa nini nilitafuta gari ya uwezo wa chini! Unatoka Pugu karibu na Chanika, unafanya kazi posta unataka uwe unasukuma Kluger kila siku lazima ufe kwa mawazo!
Kila mtu aangalie matumizi na kipato chake, kama wewe umejaaliwa kuwa na kipato kikubwa shukuru Mungu lakini si kusema ulimtema mtu mate chini kwa kumuona yupo kwenye passo! Mitandao isiwafanye mkufuru Mungu!