Hizi gari hapana, nitabadilishana na Bodaboda

Hizi gari hapana, nitabadilishana na Bodaboda

Nyie mnao jimwambafai hamyapendi magari flani hamnaga hata baiskeli, kwa mtu mpambanaji aliewahi/anaemiliki gari (sio ya uridhi, kuhongwa au wizi) anajua nini maana ya gari haijalishi imekaaje na ina muonekano gari.

Kwa kua sikujui na hakuna uwezekano wa kukujua ndio maana unajitapa humu JF
Ukitaka kunijua au kujua kama similiki au namiliki gari/magari ya aina gani wala sio kazi ngumu mbona, ni suala la uamuzi na muda wako tu.
 
Ukitaka kunijua au kujua kama similiki au namiliki gari/magari ya aina gani wala sio kazi ngumu mbona, ni suala la uamuzi na muda wako tu.
Sawa mkuu mwenye gari zake za maana mjini
 
Gari ni kama nguo, wewe unapenda suti mwenzio cadets, wewe unafia kwenye jeans mwenzio suruali za vitambaa!

Hali kadhalika huwezi kumtaka fundi gereji avae suti na kazi yake unaijua, ndiyo hivyo hivyo huwezi kumlazimisha afisaa wa benki kuvaa overrall kazini kwake kisa wewe unashindia hilo!

Wananzengo, wanasahau kuwa kumiliki gani kuna factors nyingi!
1. Matumizi
2. Gharama za uendeshaji
3. Mazingira
4. Uchumi

Mazingira na shughuli zangu yanaruhusu mimi kutumia Passo, unawashwa nitumie VX! Una akili mzuri?

Pengine nikitumia VX hasara natumia Passo kumaintain faida!

Uchumi / kipato changu ni cha kuweza kumudu Vitz wewe unalazimisha nitumie Kluger, akili ipo sawa sawa?

Wewe una watoto sita utawaza noah au gari yoyote seven seater, sina mtoto sina mke! Ninunuea noah ya nini? Nikiingia zangu gheto nachomoka misele yangu midogo midogo mjini hapa, nitafute brevis ya nini?

Sina safari ndefu, wazazi naingia hapo Mbagala nawaona narudi zangu Tandika, nitafute gari engine kuubwa ili iweje? Kaangalia matumizi yake, inamtosha maisha yasonge mbele.

Tatizo waswahili tunaiga sana na kupenda kujikweza hata tusipostahili!

Hii nakupa ni Live story! Ndugu yangu kabisa, alinicheka sana mimi kununua terios kwa kujinyima yeye akiwa hana gari akaja kununua kluger kwa kukopa kupitia mshahara! Madai yake hawezi kuendesha 'vibebi woka'

Kumbuka mshahara unapungua kukata mkopo na umeongeza matumizi ya mafuta, kilichotokea haikupita miezi sita! Ana madeni kila kona ya 20,000 au 50,000.

Gari inatembea wiki moja baada ya mshahara, wiki zingine tatu anaomba lifti gari ipo home anashindwa kumudu gharama za uendeshaji!

Aliuza kluger akanunua porte sasa hivi anafurahia maisha mwaka wa pili sasa, kila siku gari ipo njiani na madeni hana tena!

Hapo akaelewa logic yangu kwa nini nilitafuta gari ya uwezo wa chini! Unatoka Pugu karibu na Chanika, unafanya kazi posta unataka uwe unasukuma Kluger kila siku lazima ufe kwa mawazo!

Kila mtu aangalie matumizi na kipato chake, kama wewe umejaaliwa kuwa na kipato kikubwa shukuru Mungu lakini si kusema ulimtema mtu mate chini kwa kumuona yupo kwenye passo! Mitandao isiwafanye mkufuru Mungu!
[emoji122][emoji122][emoji122]
 
*Ukiona unaweza kula milo mi3 na hujui njaa, tambua Kuna mtu hata mlo mmoja hapati
*Ukiweza kumiliki V8 bas tambua Kuna mtu hanauwezo wa kununua hata baiskel
*ukiweza kulipa nauli ya daladala kumbuka kuna watu wanatembea kwa mguu kwa kukosa nauli

Kwenye maisha tuko tofaut tofaut kuna mwngine akimiliki Porte familia/ukoo mzima unampa heshima
 
*Ukiona unaweza kula milo mi3 na hujui njaa, tambua Kuna mtu hata mlo mmoja hapati
*Ukiweza kumiliki V8 bas tambua Kuna mtu hanauwezo wa kununua hata baiskel
*ukiweza kulipa nauli ya daladala kumbuka kuna watu wanatembea kwa mguu kwa kukosa nauli

Kwenye maisha tuko tofaut tofaut kuna mwngine akimiliki Porte familia/ukoo mzima unampa heshima
Noted...[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Ongeeni yote na toeni povu hadi makoo yakauke ila Passo, Fun cargo, Toyota IQ na mengine ya ukoo huo ni sawa kwa sheria na taratibu za kejeli kuyaita Sanlg zenye body ya station wagon
 
Nimecheka sana na comment za wananchi wa JF[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kwa wachaga mnaorudi mkoani kwenu kula sikukuu, kuna yeyote ametoboa Dar-Kilimanjaro akiwa na Fun cargo?
 
Siku hizi watu hawajali muhimu wanatembelea kishuzi!
 
Huu uzi ukiuchunguza kwa kina utagundua wachangiaji wengi ni wapanda daladala, bodaboda na wale wachache wanaomiliki magari ya urithi.

Wale wenzangu na mimi waliojipinda na kununua hizo passo, suzuki, funcargo, nk. wametulia kimya huku wakishangaa nini hasa lengo la huu uzi! ni kejeli tu, kujimwambafai, sizitaki mbichi hizi, au!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habarini Wakuu,

Tangu mwaka wa 2018 June nilikuwa nikihitaji at least kupata usafiri binafsi. Katika mchakato wa kuwashirikisha wajuzi zaidi wa magari na madalali baadhi wamekuwa wakisuggest aina za magari ambayo zilikuwa zinanichekesha sana Wallah

Kuna aina za magari binafsi naona zina muundo mbaya (body structure) hasa kwa Wanaume.

Ikitokea nikapewa zawadi ya magari hayo nitabadilishana na mtu mwenye pikipiki BOXER muda huohuo kabla ya Masaa 6.

Gari hizo ni Porte, Nadia na aina flan ya Suzuki:

Kwahiyo hapo umeona uweke Nadia
Hivi Nadia ina ubaya gani??? inamaana we huzijui funcargo? Probox, Nissan cube au Fogo??
 
Back
Top Bottom