Hizi Gari: kubadili OIL ni milioni 47.

Hizi Gari: kubadili OIL ni milioni 47.

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
FB_IMG_1685982599665.jpg

#FAHAMU : Kama utakuwa ni moja kati ya watu ambao wanandoto siku moja kuja kumiliki magari ya kifahari basi leo kwa uchache tunakufahamisha gharama za kubadilisha oil kwa magari baadhi ya kifahari.

Kupitia mtandao wa Bugatti Browad unaandika gharama za kubadili oil kwa magari hayo ni kuanzia Million 47,340,000 hadi Million 59,175,000 na kutofautia huku inategemeana na modeli ya Bugatti husika, na wauzaji wa magari haya pia wanashauri walau oil ibadilishwe mara moja kwa mwaka.

Mtandao wa J.D. Power unataja gharama za kubadili oil kwenye gari aina ya Lamborghini ni Kuanzia Laki 946,800 hadi Million 4,734,000 kwa kutegemeana na modeli ya Lamborghini husika, na inashauriwa kubadilishwa kwa kila baada ya Miles 9,000 ambayo ni sawa na Kilomita 14,484.

Mtandao wa Rolls-Royce Motor Car unataja gharama za kubadilisha oil kwenye gari hizo ni kuanzia Millioni 1,538,550 hadi Millioni 4,734,000 na hii pia inategemeana na modeli ya gari na mwaka husika, Kwa kawaida pia wameshauri kubadilishwa kwa oil wa gari hiyo kuanzia Kilomita 4,828 hadi 11,265 ambayo ni sawa na mara mbili hadi moja kwa mwaka.

Kwa upande wako unatumia muda gani kubadilisha oil ya gari yako? na huwa inakugharimu kiasi gani?

📝: @goodluckepafra

#EastAfricaTV #SupaTech
 
Kwa wenye mijihela yao sio kesi, wenzangu na mimi tuendelee unga unga mwana
 
Nafikiri wanaweka gharama kubwa zimilikiwe na watu wachache /matajiri ,tena kwa oda maalumu. Zisije kuwa km ist zetu au harrier matako ya nyani 😂😂😂😂
 
Ni 47 mil au 4.7 mil.
Any way wazungu uchumi wao unawategemeA WAARABU,WAARABU wata nunua tu.
 
Wazee wa Oil za SAE tukutane hapa[emoji28]
 
Back
Top Bottom