Hizi graduation za day care na nursery zimeanzia wapi?

Hizi graduation za day care na nursery zimeanzia wapi?

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
16,911
Reaction score
28,469
I salute you kinsmen
Wakuu

Kuna jambo huwa linanishangaza sana

Ninapoishi kuna ukaribu kidogo na day care moja hivi.

Sasa jioni nimerudi nikawa naskia muziki mule

Kumbe wameweka graduation party wazazi wamealikwa jioni hiyo

Yaani kiufupi ni graduation ya watoto kumaliza day care! Hapo hata nursery hawajafika!

Nikajiuliza sana
Na majoho wamevalishwa kabisa, mama mmoja nimeskia alilia mpaka kuzimia kabisa, hakuamini kuwa mwanaye kamaliza hiyo day care ..

Kiukweli elimu inapoelekea inaenda kudharaulika sana kwa kweli

Mtoto akimaliza la kwanza anafanyiwa graduation ya kufa mtu na joho anavaa

Means kila mwaka anafanyiwa graduation
Maana ya elimu inapotea kabisa .

Waacheni watoto waufaidi utoto wao msiwabebeshe matumaini makubwa wakiwa wadogo
Sasa mama junior and the likes ni mwendo wa graduation tu.

Wazazi wa watoto wanaohitimu elimu ya awali kuna muda wanakuza sana mambo.
Utakuta mzazi analia hadi anazimia.

Ukimuuliza, anajibu "Siamini kama mwanangu kapiga hatua kubwa hivi kwenye maisha yake".

Hatua ipi wakuu? Mbona Junia mwenyewe hawezi kuandika "a" hajui kuandika "i". Sijaongelea kabisa suala la kuhesabu 1-5.

Kitu pekee ambacho Junia amekifanya kwa mwaka mzima ni kupaka tu rangi picha ya tembo!

Kwanza Junia avue hilo joho. Kwani akivaa nguzo za chekecheana yebo na akafanya hako kasherehe kuna nini?

1765128981008.jpg
 
Pesa za kwao wivu wa nini bwana, acha watu wale maisha, juzi tu hapa nimealikwa mtoto wa sister anamaliza elimu ya madudu, nilienda kiroho safi nikifikiri nitakutana na kapart ka mchongo kilichotokea usipime, nyama za kutosha zimeliwa siku 2 mfululizo huku mimi nikiwa kama mjomba nikatengewa kret 2 za bia nimekesha nazitwanga, sasa wewe naona unataka kutuhalibia fursa wazee wa jiji hivihivi tunaona.
 
Upo sahihi kabisa sioni umuhimu wa ilo naona kama shule zina tengeneza namna ya kupata pesa utakuta kuchangia ni 70k hiyo nguo pee bado hela ya sherehe na wana unganisha kwenye ada ya mtoto
Day care kwa Tanzania ni wizi mkubwa tu

Watoto wanafundishwa kwa kuforce eti mtoto wa miaka miwili anafundishwa kusoma kweli?

Tangu lini maana ya day care ikawa shule ya kusoma? Ni wezi
 
Daycare anagraduate nini?
Daycare ni uangalizi kwa mtoto muda ambao walezi labda wanakua kazini au sababu yoyote waionayo. Ndio maana zipo mpaka zakulipia kwa siku moja, wiki n.k kama mzazi/mlezi ana dharula.

Sasa daycare anagraduate kitu gani?
Ndio tulipofikia mkuu ila kwa kuwa pesa ni.ya mtu basi acha afanye atakalo tu ila kiukweli wanashangaza

Na sikuhizi day care zimeanza kuforce watoto wasomeshwe kwa nguvu
 
Day care kwa Tanzania ni wizi mkubwa tu

Watoto wanafundishwa kwa kuforce eti mtoto wa miaka miwili anafundishwa kusoma kweli?

Tangu lini maana ya day care ikawa shule ya kusoma? Ni wezi
Wamama ndio wamepumbazwa na hizo day care


Ukifwatilia day care nyingi hazina sifa
 
I salute you kinsmen
Wakuu

Kuna jambo huwa linanishangaza sana

Ninapoishi kuna ukaribu kidogo na day care moja hivi.

Sasa jioni nimerudi nikawa naskia muziki mule

Kumbe wameweka graduation party wazazi wamealikwa jioni hiyo

Yaani kiufupi ni graduation ya watoto kumaliza day care! Hapo hata nursery hawajafika!

Nikajiuliza sana
Na majoho wamevalishwa kabisa, mama mmoja nimeskia alilia mpaka kuzimia kabisa, hakuamini kuwa mwanaye kamaliza hiyo day care ..

Kiukweli elimu inapoelekea inaenda kudharaulika sana kwa kweli

Mtoto akimaliza la kwanza anafanyiwa graduation ya kufa mtu na joho anavaa

Means kila mwaka anafanyiwa graduation
Maana ya elimu inapotea kabisa .

Waacheni watoto waufaidi utoto wao msiwabebeshe matumaini makubwa wakiwa wadogo
Sasa mama junior and the likes ni mwendo wa graduation tu.

Wazazi wa watoto wanaohitimu elimu ya awali kuna muda wanakuza sana mambo.
Utakuta mzazi analia hadi anazimia.

Ukimuuliza, anajibu "Siamini kama mwanangu kapiga hatua kubwa hivi kwenye maisha yake".

Hatua ipi wakuu? Mbona Junia mwenyewe hawezi kuandika "a" hajui kuandika "i". Sijaongelea kabisa suala la kuhesabu 1-5.

Kitu pekee ambacho Junia amekifanya kwa mwaka mzima ni kupaka tu rangi picha ya tembo!

Kwanza Junia avue hilo joho. Kwani akivaa nguzo za chekecheana yebo na akafanya hako kasherehe kuna nini?

View attachment 3512768
Ujumbe umefika mkuu😂😂

Ila kama umetia chumvi kidogo
Kukazia Point zako
Kuna Bi Mkubwa alibubujikwa na machozi ya furaha kuliko Luka mwashambwa😂😂.
 
Back
Top Bottom