Hizi graduation za day care na nursery zimeanzia wapi?

Hizi graduation za day care na nursery zimeanzia wapi?

I salute you kinsmen
Wakuu

Kuna jambo huwa linanishangaza sana

Ninapoishi kuna ukaribu kidogo na day care moja hivi.

Sasa jioni nimerudi nikawa naskia muziki mule

Kumbe wameweka graduation party wazazi wamealikwa jioni hiyo

Yaani kiufupi ni graduation ya watoto kumaliza day care! Hapo hata nursery hawajafika!

Nikajiuliza sana
Na majoho wamevalishwa kabisa, mama mmoja nimeskia alilia mpaka kuzimia kabisa, hakuamini kuwa mwanaye kamaliza hiyo day care ..

Kiukweli elimu inapoelekea inaenda kudharaulika sana kwa kweli

Mtoto akimaliza la kwanza anafanyiwa graduation ya kufa mtu na joho anavaa

Means kila mwaka anafanyiwa graduation
Maana ya elimu inapotea kabisa .

Waacheni watoto waufaidi utoto wao msiwabebeshe matumaini makubwa wakiwa wadogo
Sasa mama junior and the likes ni mwendo wa graduation tu.

Wazazi wa watoto wanaohitimu elimu ya awali kuna muda wanakuza sana mambo.
Utakuta mzazi analia hadi anazimia.

Ukimuuliza, anajibu "Siamini kama mwanangu kapiga hatua kubwa hivi kwenye maisha yake".

Hatua ipi wakuu? Mbona Junia mwenyewe hawezi kuandika "a" hajui kuandika "i". Sijaongelea kabisa suala la kuhesabu 1-5.

Kitu pekee ambacho Junia amekifanya kwa mwaka mzima ni kupaka tu rangi picha ya tembo!

Kwanza Junia avue hilo joho. Kwani akivaa nguzo za chekecheana yebo na akafanya hako kasherehe kuna nini?

View attachment 3512768
Unge lalamikia gharama za kiuchumi ningekuona una hoja ila ulicho lalamikia wewe zaidi ni upumbavu wa kutokujua umuhimu wa hayo mambo kwa kuwapa moyo watoto kisaikolojia .
 
Unge lalamikia gharama za kiuchumi ningekuona una hoja ila ulicho lalamikia wewe zaidi ni upumbavu wa kutokujua umuhimu wa hayo mambo kwa kuwapa moyo watoto kisaikolojia .
Una uhakika?
 
Back
Top Bottom