Hizi hapa bifu zaidi ya 60 zilizowahi kutikisa hapa nchini zinazohusisha wanamuziki, watayarishaji wa muziki, media nk

Man-X alidai aliitaka beat, akamcheki Bwana Misosi, Misosi akampa beat kwa CD
wimbo ulivyotoka uka-hit sana kuliko ule wa Misosi, ndipo beef lilipoanzia, Misosi akakomaa chinichini mpaka redioni usipigwe
Prof J alisuluhisha
Haha nakumbuka Hiyo...
Haina tofauti na ile ya Fid Q na Rado
😅😅
 
Umesahau bifu hizi bendwa za miaka ya 2000-2008..

Mwana FA vs Dudubaya (Baada ya kuombana msamaha wakatoa nyimbo inaitwa tuliza kitenesi i think ilikuwa 2004 kama sio 2005)

MwanaFA Vs Wandago ( Baada ya kuimba ingekuwa VIPI jmaa walimind wakaanzisha Bifu na wakamjibu ingekuwa Poa)

Bwana Misosi vs Man x (hii ilikuja baada ya Man x kuiba beat la Bwana misosi nitoke vipi nakuimba kwenye nyimbo yake nimechezea bahati ambayo alimshirikisha dully sykes)

Prof jize vs Chamilion...

Juma Nature vs Jaymo (
jaymo alitembea na Sinta ndo bifu likaanza na nyimbo kibao album nzima ya Ugali ilikuwa na majungu ya sinta tu na jaymo)

PNC vs Babu tale na abdubonge (Tip Top)

Baba levo na Nay wa mitego (
Kama unakumbuka miaka 2005 au 2006 hivi Ney alitoka Bongo records akatoa nyimbo ya Itafahamika akatukana watu akiwemo P funk...Na kipindi hicho baba levo yuko chini ya Pfunk majani akaamua kuanzisha bifu na akamjibu kwa nyimbo inaitwa wanyee mwaka 2006)

Hallow ziko nyingi tuanze na hizi kwanza nitaongeza zingine
Hii ishu ya Sinta ni kuwa aliliwa na Moe Technic au na marehemu Cool James mtoto wa Dandu?
 
na bado hawajasuluhisha hii, kila leo Rado akihojiwa anaongea kwa hisia kweli dhidi ya Fid
Vivyo hivyo kwa Fid Q, huwa anapenda kuhamisha mada likija swali la RADO na yeye.

Na RADO ni kuwa hata akienda kutambulisha wimbo mpya, watangazaji wanaachana na wimbo mpya na mahojiano yanakua kuhusu USIULIZE na bifu zima kati yake na Fid Q
 
Hii diss ilikaa kikuda sana. Chanzo cha bifu ni pale Afande aliposhinda shindano la rapa bora na kupewa gari. Solo alidai yeye ndio alistahili kuwa mshindi na sio "Mgambo Sele". Sijajua kama walishapatana. Ila ile "Mtazamo" ndio inabaki kuwa collabo yangu ya muda wote
Solo alimind kwa kuwa kwa namna Top 5 ilivyowekwa, ilikuwa lazima tu ashinde Afande Sele. Yaani top 5 iliwaacha Prof. J na Solo Thang nje, hapo ndio ikaonekana ushindi ni wa kupangwa mezani.

Shindano linahusu Vina halafu Solo Thang anatupwa nje!!
 
Vivyo hivyo kwa Fid Q, huwa anapenda kuhamisha mada likija swali la RADO na yeye.

Na RADO ni kuwa hata akienda kutambulisha wimbo mpya, watangazaji wanaachana na wimbo mpya na mahojiano yanakua kuhusu USIULIZE na bifu zima kati yake na Fid Q
mie niko na Rado kwa hili, Fid aliiba mistari bila ridhaa ya mshikaji, kwa miaka zaidi ya 15 jamaa analalamika
 
Nikki mbishi vs P mawenge
Belly white vs Belly black
Harmonize ft dogo janja
 
mie niko na Rado kwa hili, Fid aliiba mistari bila ridhaa ya mshikaji, kwa miaka zaidi ya 15 jamaa analalamika
Na RADO alionesha ukubwa wake kuwa ni kweli anaweza kuwa ameibiwa kwa kutoa track yenye mistari yenye ujazo wa kutisha. Nafikiri mpaka sasa ile ndio BEST DISS TRACK of all time kwa Tanzania
 
NAKAZIA HAPA, Nick Dizzo alizidi kuitendea haki zaidi kwa instrumental kali
Unaambiwa kina Puff Daddy na BiG walipoisikia Hit Em Up hata nguvu za kuijibu ziliwaishia, yaani wanaona watajibu nini kuipiku ile ngoma.

Sasa nafikiri ndicho kilichomkuta Bwana Kubanda Mwanza Mwanza - alipararaizi.
 
Fid alidai jamaa alibahatisha,

huwezi bahatisha na bars zote zile ndan ya dk 4 nzima
 
Solo alimind kwa kuwa kwa namna Top 5 ilivyowekwa, ilikuwa lazima tu ashinde Afande Sele. Yaani top 5 iliwaacha Prof. J na Solo Thang nje, hapo ndio ikaonekana ushindi ni wa kupangwa mezani.

Shindano linahusu Vina halafu Solo Thang anatupwa nje!!
Sasa Soggy ndo alikuwa hamtaki kabisa kusikia na mpaka leo hakubali kuwa Afande ndo mfalme wa Rhymes 😅😅
 
Yeah, nakumbuka Soggy alisema kabla ya mchuano haujaanza kwa top 5 kuwa pale lazima Afande apewe ushindi maana aliwekwa na watu wa uwezo wa chini (kivina). Yaani hakukubali kabisaa
 
Hii ishu ya Sinta ni kuwa aliliwa na Moe Technic au na marehemu Cool James mtoto wa Dandu?
Hahaha mzee hapo kuna scandel mbili Hapo 😅😅 na una kumbukumbu sana umanifanya nimekumbuka mbali sana...Ngoja niziweke sawa hizo scandel ili uzielewe vizuri...Hiyo ilikuwa 2001 mpka 2002..

Ishu ilianzia Kwa Mtoto wa dandu (Cool James) kweli ila ilikoishia Ni Kwa Jaymo

Ishu ilikuwa Hivi kipindi cool james (Mtoto wa dandu) ndo ametoka sweeden na vihela hela kibao wakishua tena akaja akaanza kufanya mziki na nyimbo zake pale kwa Master J..

Nakumbuka kipindi hicho Mwanamke aliyekuwa moto kweli kweli ndo alikuwa Sinta, Sasa jamaa kuona hivyo akamwita sinta mwanza kwenye kufnya naye Shooting ya nyimbo yake inaitwa mapenzi kama sijakosea sana alitka awe kama video vixen,

unamkumbuka rafiki yake na Sinta kipindi hicho walikuwa wanaigiza naye alikuwa anaitwa Nina (Mdada fulan alikuwa ana macho fulan hivi) Ndo walienda naye sasa shida ikaja Nina alipobanwa sana na Nature aliporudi Bongo baada ya scandel kuzagaa mwenye magazeti ya udaku ya shigongo ikabidi aropoke tu Mzigo wake umeliwa na Dandu 😅😅

kipindi hicho wanashoot Nature alikuwa south na scandel ya JMo ilikuwa bado iko chini chini bado haijawaza hadharani sana..na haikuwa confirmed

na ndo maana kwenye ile nyimbo ya inaniuma sana
kuna kipande anasema

"Wengine ni Rafiki zangu nikiwataja huwezi kuamini"

ningekuwa na Muda ningekuandikia Hadi mistari yote Inavyochana watu humo nikakuchambulia vizuri..

Sasa nature ikamuumiza ndo akaingia Studio
katoka na Nyimbo Ya INANIUMA SANA..

sasa Hapa na pale wakarudiana ndo akatoa ile nyimbo kama unaifahamu ya Aah wapi (Sijui kama itawezekana,Mtu niliyempenda sana,Tukaja tukafarakana kwa sababu wanachonga sana)

sasa Kilichomuuma Sana mpaka akatoa nyimbo Mbili Double za Sitaki Demu na remix yake...
ni baada ya kuthibitisha kwamba Sinta anachukuliwa na Jaymo 😅😅

hapa ndo aliamua kuacha kabisa na hii ndo scandel na zingine zilizifuata ndo zilomfanya mpaka sinta akaondoka nchini maaana watu kadhaa walipiga Saini pale ..ahaah

ukisikia vizuri nyimbo ya Sitaki Demu verse ya kwanza jamaa anamalizia amasema " haya Sasa nimeghairi nenda kwa huyo Jaymo"
 
Yeah, nakumbuka Soggy alisema kabla ya mchuano haujaanza kwa top 5 kuwa pale lazima Afande apewe ushindi maana aliwekwa na watu wa uwezo wa chini (kivina). Yaani hakukubali kabisaa
Dah leo nimekumbuka mbali sana unajua baya mambo ni ya miaka 20 ilopita 😅😅
Halafu kama juzi tu
 
Fid alidai jamaa alibahatisha,

huwezi bahatisha na bars zote zile ndan ya dk 4 nzima
Ha ha haa, kubahatisha!! ChemChem na Wana.. track moja iliyoshiba, diss Fid Q, diss ECT..yaani dah..acha tu, marehemu Dee 7 alikuwa anacheka sana Dj Maliz akianza kupiga beat ya usiulize (akii-loop). Ilikuwa lazima D7 aongee, anasema haya sasa msiulize😃😃

Fid angekuwa Babu Tale enzi zile angezuia kabisa hii ngoma isichezwe radioni, kama kina Gulu walivyokuwa wanamfanyia Mr. Blue baada ya kuondoka G Records
 
Hahaha mzee hapo kuna scandel mbili Hapo 😅😅 na una kumbukumbu sana umanifanya nimekumbuka mbali sana...Ngoja niziweke sawa hizo scandel ili uzielewe vizuri...Hiyo ilikuwa 2001 mpka 2002..

Ishu ilianzia Kwa Mtoto wa dandu (Cool James) kweli ila ilikoishia Ni Kwa Jaymo

Ishu ilikuwa Hivi kipindi cool james (Mtoto wa dandu) ndo ametoka sweeden na vihela hela kibao wakishua tena akaja akaanza kufanya mziki na nyimbo zake pale kwa Master J..

Nakumbuka kipindi hicho Mwanamke aliyekuwa moto kweli kweli ndo alikuwa Sinta, Sasa jamaa kuona hivyo akamwita sinta mwanza kwenye kufnya naye Shooting ya nyimbo yake inaitwa mapenzi kama sijakosea sana alitka awe kama video vixen,

unamkumbuka rafiki yake na Sinta kipindi hicho walikuwa wanaigiza naye alikuwa anaitwa Nina (Mdada fulan alikuwa ana macho fulan hivi) Ndo walienda naye sasa shida ikaja Nina alipobanwa sana na Nature aliporudi Bongo baada ya scandel kuzagaa mwenye magazeti ya udaku ya shigongo ikabidi aropoke tu Mzigo wake umeliwa na Dandu 😅😅

kipindi hicho wanashoot Nature alikuwa south na scandel ya JMo ilikuwa bado iko chini chini bado haijawaza hadharani sana..na haikuwa confirmed

na ndo maana kwenye ile nyimbo ya inaniuma sana
kuna kipande anasema

"Wengine ni Rafiki zangu nikiwataja huwezi kuamini"

ningekuwa na Muda ningekuandikia Hadi mistari yote Inavyochana watu humo nikakuchambulia vizuri..

Sasa nature ikamuumiza ndo akaingia Studio
katoka na Nyimbo Ya INANIUMA SANA..

sasa Hapa na pale wakarudiana ndo akatoa ile nyimbo kama unaifahamu ya Aah wapi (Sijui kama itawezekana,Mtu niliyempenda sana,Tukaja tukafarakana kwa sababu wanachonga sana)

sasa Kilichomuuma Sana mpaka akatoa nyimbo Mbili Double za Sitaki Demu na remix yake...
ni baada ya kuthibitisha kwamba Sinta anachukuliwa na Jaymo 😅😅

hapa ndo aliamua kuacha kabisa na hii ndo scandel na zingine zilizifuata ndo zilomfanya mpaka sinta akaondoka nchini maaana watu kadhaa walipiga Saini pale ..ahaah

ukisikia vizuri nyimbo ya Sitaki Demu verse ya kwanza jamaa anamalizia amasema " haya Sasa nimeghairi nenda kwa huyo Jaymo"
Aisee umenisanua sana, hii ishu ya J Moe sikua naifahamu. Ila line ya haya sasa nenda kwa J Moe nilijua imekaa kimbwembwe tu kumbe ilikua ina maana.

Nature aliumia sana aisee, ile album nzima alikuwa analia, na huenda ikawa ni album ambayo labda hapendi kuzisikiliza nyimbo zake, maana japo zilimpa hela ila zinamkumbusha machungu.

Sawa na ile forgive me ya P Funk, nahisigi mwamba itakuwa inamkera sana akiisikia siku hizi.
 
Ha ha haa, kubahatisha!! ChemChem na Wana.. track moja iliyoshiba, diss Fid Q, diss ECT..yaani dah..acha tu, marehemu Dee 7 alikuwa anacheka sana Dj Maliz akianza kupiga beat ya usiulize (akii-loop). Ilikuwa lazima D7 aongee, anasema haya sasa msiulize😃😃

Fid angekuwa Babu Tale enzi zile angezuia kabisa hii ngoma isichezwe radioni, kama kina Gulu walivyokuwa wanamfanyia Mr. Blue baada ya kuondoka G Records
Dah halafu ujue Guru Jamaa Hazeeki nilikutana naye siku moja mpaka nikashangaa Dah...
Ila Guru na Pfunk walikuwa na Roho kama zinafanana tu kwa Hali yake wanafaa kulaumiwa kuhusu kupotea kwa wasanii mbalimbali
 
Back
Top Bottom