Hahaha mzee hapo kuna scandel mbili Hapo [emoji28][emoji28] na una kumbukumbu sana umanifanya nimekumbuka mbali sana...Ngoja niziweke sawa hizo scandel ili uzielewe vizuri...Hiyo ilikuwa 2001 mpka 2002..
Ishu ilianzia Kwa Mtoto wa dandu (Cool James) kweli ila ilikoishia Ni Kwa Jaymo
Ishu ilikuwa Hivi kipindi cool james (Mtoto wa dandu) ndo ametoka sweeden na vihela hela kibao wakishua tena akaja akaanza kufanya mziki na nyimbo zake pale kwa Master J..
Nakumbuka kipindi hicho Mwanamke aliyekuwa moto kweli kweli ndo alikuwa Sinta, Sasa jamaa kuona hivyo akamwita sinta mwanza kwenye kufnya naye Shooting ya nyimbo yake inaitwa mapenzi kama sijakosea sana alitka awe kama video vixen,
unamkumbuka rafiki yake na Sinta kipindi hicho walikuwa wanaigiza naye alikuwa anaitwa Nina (Mdada fulan alikuwa ana macho fulan hivi) Ndo walienda naye sasa shida ikaja Nina alipobanwa sana na Nature aliporudi Bongo baada ya scandel kuzagaa mwenye magazeti ya udaku ya shigongo ikabidi aropoke tu Mzigo wake umeliwa na Dandu [emoji28][emoji28]
kipindi hicho wanashoot Nature alikuwa south na scandel ya JMo ilikuwa bado iko chini chini bado haijawaza hadharani sana..na haikuwa confirmed
na ndo maana kwenye ile nyimbo ya inaniuma sana
kuna kipande anasema
"Wengine ni Rafiki zangu nikiwataja huwezi kuamini"
ningekuwa na Muda ningekuandikia Hadi mistari yote Inavyochana watu humo nikakuchambulia vizuri..
Sasa nature ikamuumiza ndo akaingia Studio
katoka na Nyimbo Ya INANIUMA SANA..
sasa Hapa na pale wakarudiana ndo akatoa ile nyimbo kama unaifahamu ya Aah wapi (Sijui kama itawezekana,Mtu niliyempenda sana,Tukaja tukafarakana kwa sababu wanachonga sana)
sasa Kilichomuuma Sana mpaka akatoa nyimbo Mbili Double za Sitaki Demu na remix yake...
ni baada ya kuthibitisha kwamba Sinta anachukuliwa na Jaymo [emoji28][emoji28]
hapa ndo aliamua kuacha kabisa na hii ndo scandel na zingine zilizifuata ndo zilomfanya mpaka sinta akaondoka nchini maaana watu kadhaa walipiga Saini pale ..ahaah
ukisikia vizuri nyimbo ya Sitaki Demu verse ya kwanza jamaa anamalizia amasema " haya Sasa nimeghairi nenda kwa huyo Jaymo"