Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Hapa unazungumzia watu wengi kukubaliana na msimamo wa Magufuli au usahihi wa msimamo wa Magufuli? Maana hata viongozi waliofanya mambo maovu kwa binadamu wengine pia waliungwa na watu wengi na historia imetunza kumbukumbu hizo. Mfano mrahisi kabisa, Kaburu Pieter Botha wa Afrika kusini aliungwa mkono na wengi katika kuwabagua weusi.Magufuli ni Raisi wa aina yake, siyo mtu wa kumumunya maneno kuogopa mabeberu watamfikiriaje. Kwa Africa hadi sasa sijaona Rais mwenye uthubutu Kama huo, maraisi wengi wa Africa ni wanafiki wanaojipendekeza kwa mabeberu wakiogopa kusitishiwa misaada...
Kama msimamo wa Magufuli ni sahihi, taja ni watu wa nchi gani, au kiongozi yoyote wa Afrika aliyesimama na kuunga mkono msimamo wake ili kuibeba hoja yako. Kitu kipekee alichopatia kwenye huu ugonjwa, ni kutokutuweka watanzania lockdown, hayo mengine anaongea mambo ya aibu tu, hasa ukizingatia yeye ni msomi wa sayansi kama ni kweli.