"Kila zama na kitabu chake". Mzee Ally Hassan Mwingi.Naona kuna majamaa ya huko Geita ,Kahama na Katoro yanasumbua mji sana kwa zawadi ya sendoff ya bilioni moja na ushee.
Yani ukija mgodini bwashee ni mwendo wa udi na matambiko sana! ni hatari.hii fedha ya madini ina ushetani sana
Sasa kama mtu anaibuka na kilo 17 za dhahabu kwanini ajitebanebane na hapo 1g unaambiwa hata 280k.Kwasasa katoro watu wanamiliki ndinga za mbele unakuta kijana anamoliki ndinga ya millioni 350 na sio moja hata tano hivi
Naona kuna majamaa ya huko Geita ,Kahama na Katoro yanasumbua mji sana kwa zawadi ya sendoff ya bilioni moja na ushee.
Kama ingekuwa mimi ni Chadema nisingepost hii kitu.
Kama ingekuwa mimi ni Chadema nisingepost hii kitu.
Ni aibu mno kukiri kushindwa kutoka.
🤣 Hahaha; Digala..enzi zetu kuna wimbo chorus yake tuliiwekea hili neno enzi za Machimbo ya Dhahabu huko Nyamikonze-Geita..!Machimbo ya tunduru miaka ile yamelipuka watu wakipiga mshindo starehe walikuwa wanazifanyia mtwara mjini...wasukuma wakati huo utasikia bora uishiwe damu kuliko kuuishiwa pesa (1)Kuna mtu mmoja alipigishwa magoti huku amebeba Kreti za bia kichwani wao wakawa wanakunywa yaani walimfanya kama meza...(2) Kuna jamaa mmoja akifanya kazi mkoani pale kwahiyo alimfungulia biashara mkewe pale stand... kwahiyo Digala wa madini akampenda sana yule dada aisee kama utani aliivunja ndoa ya watu kwa jeuri ya pesa,,,ndio mara ya kwanza nilimuona mtu analia hadharani huku anamuomba digala amuachie mkewe kwasababu anampenda na wametoka mbali na wana mtoto mdogo aiseee ni tukio la kikatili mno kuwahi kuliona tena stand watu wamejaa Kibao.