Historia hujirudia. Kuna Don mmoja wa madini kule Mererani/Arusha alijulikana kama "Askofu" alitesa sana mwaka 1995. Mwamba alipata matofali ya Tanzanite ya kutosha kununua magari kadhaa aina ya Landrover, alinunua hotel ya ghorofa kadhaa pale Arusha alijulikana kama Pallson Hotel na kwa wiki moja alikuwa akiamka asubuhi anarushia watu pesa kutoka ghorofani.
Watu kama hawa wanapaswa kuingizwa kwenye vitabu vya TRA na kukatwa kodi zaidi ya 50% ya mapato ghafi, nchi ingepiga hatua haraka.