Hizi mechi ndizo zitaamua nani anakuwa bingwa 2025/2026

Hizi mechi ndizo zitaamua nani anakuwa bingwa 2025/2026

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,982
Reaction score
51,157
Bila ya kujali msimamo wa ligi ulivyo hivi sasa, mechi sita za mwisho za ligi kuu Tanganyika, ndizo zitakazoamua nani atakuwa bingwa Kwa msimu wa mwaka 2025/2026.

Wakati Simba itaanza na Dodoma Jiji (24/05/2026) Yanga wao siku inayofuata itakutana na Namungo. Mechi ngumu kwa Simba, Yanga mechi ya kawaida.

Tarehe 13/06/2026, Yanga watapambana na Mashujaa, wakati Simba kesho yake itakuwa uwanjani kupimana nguvu na Pamba Jiji. Mechi ngumu kwa wastani Kwa Simba na pia Yanga.

Tarehe 17/06/2026, Yanga itakutana na Singida big stars wakati kesho yake Simba watavaana na Mbeya City. Mechi za kawaida kwa Simba na Yanga.

Tarehe 24/06/2026 timu zote mbili zitashuka dimbani kwa Simba kupambana na Mtibwa sugar wakati Yanga watavaana na Azam. Mechi ngumu wastani kwa Simba mechi ngumu kwa Yanga.

Simba itapambana na Singida Big stars tarehe 27/06/2026, wakati Yanga siku hiyo hiyo itakuwa na kibarua dhidi ya TRA. Mechi ngumu kwa wastani kwa timu zote mbili.

Tarehe 30/06/2026 Yanga itakuwa na mechi ngumu ya wastani dhidi ya JKT, wakati Simba siku hiyo hiyo itamaliza ligi kwa kucheza mechi ya kawaida na KMC.

Hizi mechi ndizo zitakazoamua nani anakuwa bingwa wa NBCPL kwa mwaka 2025/2026.
 
Back
Top Bottom