Hizi ndio biashara 17 zitakazofanya utoboe haraka maisha

mkuu habari,

unaweza dadavua kiufupi changamoto kuu za hii biashara ni zipi na pengine nini mzizi wa suluhu yake kwa upeo wako tafadhari?
Changamoto ya hii biashara ni kwamba inahitaji usimamizi imara sana kuanzia kuwaongoza watu na kusimamia mambo ya fedha. Hapo kwenye kusimamia watu ndo changamoto kubwa zaidi kwasababu inabidi ufuatilie kwa karibu waalimu, wafanyakazi wasio waalimu na wanafunzi. Kinyume na hapo ndo utakuta taaluma duni na kashfa za kipuuzi kama vile ticha kutafuna wanafunzi, au wanafunzi kuwa watovu wa nidhamu.

Kushindwa kudhibiti nidhamu ya wafanyakazi na wanafunzi inapunguza imani ya wazazi/walezi hivyo kupata wanafunzi wapya inaanza kuwa shida. Hata wanafunzi wengine huhama. Mwisho wa siku ni mapato kupungua. Kitu kibaya kuliko vyote ni kuwa ukishindwa kuongoza vizuri watu kuna hatari ya taaluma kuzorota. Taaluma ikiwa mbovu ina maana matokeo ya mitihani ya NECTA yatakuwa mabovu na ndo mwanzo wa wanafunzi kukosekana na mwenye shule kufilisika. Wazazi/walezi hawana subira wala huruma kwa shule yenye matokeo mabovu.

Kimsingi ni kuwa ukiwa unamiliki shule lazima sehemu ya akili na roho yako ijue ni biashara yenye wito kwahiyo inakuwa kama familia yako. Kuna wanafunzi kuugua, migomo na mambo madogo madogo ya kuyatatua kila siku ambayo ni ya kibinadamu zaidi. Kinyume na hapo wazazi wanahamisha watoto ubaki na majengo.
 
kwa dsm ni location ipi nzuri kufungua kiwanda cha kusaga na kupaki unga?
 
Nimejifunza mengi sana mkuu

Natamani uendelee tu kuteleza madini haya hadimu..

Kama kuna nyongeza niongezee mkuu
 
Mbona hujaweka kufungua kanisa na kuniita mtume au nabii ili uzikamate zile tilatila?
 
Umesahau umarioo unalipa sana hata wanaojiuza kiakili wanatoboa sana bila kusahau ,hardware hutoboi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…