Hizi ndio hesabu za Ney wa Mitego kwenye wimbo wake mpya uitwao " Baba"

Hizi ndio hesabu za Ney wa Mitego kwenye wimbo wake mpya uitwao " Baba"

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Kwa maoni yangu wimbo wa " Baba" by Ney wa Mitego ni " commercial" Na sio wimbo wa kisiasa kama watu wengi wanavyo weza kuutafsiri

Msanii Ney wa Mitego amemtumia Hayati Magufuli kama " point of contact" kufikisha ujumbe wenye lengo la kupush agenda yake ktk biashara ya muziki wake

Lengo Hasa la Ney wa Mitego ni Ku acquire popularity among the so called " Wamachinga"

Ney wa Mitego amegundua kwamba Magufuli alipendwa Sana Na Wamachinga Kwa Sababu aliwalea Na kuwapa uhuru wa kufanya umachinga mahali popote..

Leo Magufuli hayupo amekuja kiongozi mwingine ambae ameona kwamba si vyema Wamachinga wakaachwa kuzagaa zagaa bila utaratibu, Wamachinga pamoja Na wananchi wanao sympathise Na Wamachinga Wana complain huku wakitaja ngano za kumkumbuka Hayati Magufuli

Ney wa Mitego ame capitalise kwenye hiyo factor so ameamua kufanya Huu wimbo Kwa lengo la kujitengenezea popularity Kwa Wamachinga..

Hongera Sana Ney wa Mitego , show zianze sasa Wamachinga watajaa kwenye shows zako ila ukweli utabaki pale pale Mama Samia ana upiga mwingi Sana. Binafsi Nina Imani kubwa Sana Na mama Samia and am telling you Mama huyu atafanya mambo mengi makubwa Na mazuri Kwa nchi yetu..

Ni mapema mno kumjudge mama huyu Kwa chochote cause tangu apewe nchi ana miezi Saba Tu..

NB: let me refresh ur memories. Niliwahi kuandika hapa kwamba Mama Samia amewekwa madarakani Na Mungu mwenyewe.. Her Presidency is an act of God himself)

Usijaribu kushindana Na maamuzi / mipango ya Mungu
 
Miezi saba mnasema ni michache kum-judge, how long should we wait? Miaka 15?
 
Uweke huo wimbo hapa,umeandika kama vile wote tunaujua au tumeusikia huo wimbo!
 
Maneno matatu ya mwanzo ya andiko lako yanatosha kukutambua wewe pamoja na rangi zako, acha Ney aongee kile anachokiona Ni sawa kwa wamachinga,. Ukiona inafaa na wewe unaweza ukatoa nyimbo yako ukawabeza utakavyo, huyo atakua ni wewe Sasa!
 
Maneno matatu ya mwanzo ya andiko lako yanatosha kukutambua wewe pamoja na rangi zako, acha Ney aongee kile anachokiona Ni sawa kwa wamachinga,. Ukiona inafaa na wewe unaweza ukatoa nyimbo yako ukawabeza utakavyo, huyo atakua ni wewe Sasa!
How
 
Miezi saba mnasema ni michache kum-judge, how long should we wait? Miaka 15?
WaTz hatukui mkuu.
Fikiria tangia Uhuru upatikane ni lini na bado tunajiita Nchi changa,
Sembuse siku-makumi-matatu-saba🤣
 
Kwani kwenye Nyimbo nzima kaimbia Machinga??.. unataka kuwafanya watu kama hawajaisikiliza hii nyimbo mbona kasemea kila kitu mule kasema Swala la mbowe, sabaya,machinga,uwanja wa Ndege,Swala la Polepole na mengine kwanini wewe umeona sehemu hio tu au Nyimbo umeisikilizia kwa BOOMPLAY?
 
Unasema ni mapema sana kumjudge mama halafu wewe unatuambia una imani nae?

Chanzo cha hiyo imani ni nini wakati umekataza kutoa judgement kwa kipindi hiki cha miezi 7?
 
Back
Top Bottom