Hizi ndio nchi ambazo ukikamatwa na madawa ya kulevya hutoboi hata kwa dawa

Hilo ni kweli kabisa pamoja na Dubai aisee ukidakwa tu habari yako inakua imekwisha kuna hawa ndugu wawili wamekwishaaa
 
Mkuu bila shaka unafanya utani , Iran ipi hiyo inayo kufunga kwa kesi ya madawa ya kulevya ?labda Iran nyingine sio hii tunayo ijua.
Mwaka jana tu Iran ndo nchi iliyo nyonga watuhumiwa wengi wa madawa ya kulevya kuliko nchi yeyote duniani ikifuatiwa na China ,Iran mwaka jana tu imenyonga watuhumiwa zaidi ya 300 na ushenzi wa dawa za kulevya alafu unasema nini mkuu?
Alafu kesi zake zinachukua muda mfupi sana mfano hii kesi ya huyu mkenya aliye kamatwa Vietnam imechukua miaka karibia 3 lakini kwa Iran hizo kesi hazifiki hata miezi 3 umesha kula kitanzi.

China ,Malaysia na Indonesia unaweza ukanusulika iwapo utakamatwa na madawa chini ya kg 1 lakini ukikamatwa na kg1 kwenda mbele kitanzi kinakuhusu hakuna mjadala juu ya hilo.
Iran ukikamatwa na kuanzia nusu kilo tu kichwa huna.
Ndani ya Iran kuna makosa ambayo ukikamatwa nayo unahitaji muujiza wa mungu kuchomoka ni madawa ya kulevya, kubaka,na kuifanyia ujasusi Israel au Marekani.
 
Iran imefungwa sn miaka 15 unarudi kula ugali na dagaa mtaani,,

Kivumbi hapa Kwenye inchi ya kusadikika .

Tunatolea macho wauza madawa kuliko wanaotapeli na kuhujumu inchi.
Bora hao wahujumu nchi kuliko hao wauza unga hao wanahujumu nchi wanakuachia afya yako lakini wauza unga ni waharibifu wakubwa.
 
Mmea wa opium sio mbaya sema wakulugwa wanapoa za kulichalanga lile tunda litoe utomvu ili wavune ndo shida inapoanzia Hapo
 
Kwa kweli Ridhiwani Kikwete ana bahati sana kuishi mpaka leo hii.
 
Haya wauza madawa uzi wenu huu
 
Pakistan kifungo si zaidi ya miaka 5 tu.
India ni miaka 13 Hadi 15 jela na utakaa miaka 8 au 9 tu unarudi mtaani kula dagaa na ugali.,

Hakuna anayenyongwa Pakistan Kaa kesi ya madawa.
Pakistan vipi? Maama kuna mwana wa kitaa enzi hizo 2001 alinyongwa huko karach
 
Pakistan kifungo si zaidi ya miaka 5 tu.
India ni miaka 13 Hadi 15 jela na utakaa miaka 8 au 9 tu unarudi mtaani kula dagaa na ugali.,

Hakuna anayenyongwa Pakistan Kaa kesi ya madawa.
Mbona jamaa yetu alinyongwa mzeya
 
Bora hao wahujumu nchi kuliko hao wauza unga hao wanahujumu nchi wanakuachia afya yako lakini wauza unga ni waharibifu wakubwa.
Hapo ndy mzungu alipotushinda watu wa Africa.
Ulaya kesi za unga ni kesi za kipuuzi sana,hata ukutwe na gunia Zima hufungwi maisha Wala hufungwi zaidi ya miaka 5.


Kesi kama uhujumu inchi.
Rushwa.
Human trafficking.
Wizi wa silaha
Kujeruhi watu.
Terrorist.
Ulanguzi wa silaha.

Hapo mzungu utamjuwa atakavyo kunyoosha miaka mingi.

Lakini Africa tunashadadia. Kesi ,
Za madawa ambayo yana athiri Kwa mtu mmoja mmoja na sio taifa Zima.

Mtu anayeihujumu au anayeifisadi inchi ni mbaya mara milioni ya muuza madawa ya kulevya.
Fisadi anauwa uchumi wa inchi na maendeleo Kwa ujumla,
Hyo sio wa kucheka nae hata kidogo.

Mmarekani na ubabe wake wote lakini hafungi maisha mtu wa madawa Wala hakufungi zaidi ya miaka 5.
 
Pakistan hanyongi labda jamaa yenu alikuwa mwizi akauawa na wanaichi wenye hasira kali.
🤣🤣🤣 Ah alikuwa anasukuma mzigo bwana ata pale kwetu kitaaa mie nilisukuma mzigo toka kwake ndio na mie kushika shika hela za maana. Mwana alinyongwa huko karachi...daah rip west is best😭😭😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…