Hizi ndio nchi ambazo ukikamatwa na madawa ya kulevya hutoboi hata kwa dawa

Itoe China kwenye list yako maana kuna kijana wa wahuni alikamatwa watu wakahonga gesi kijana akaachiwa hata rumande tu hakuingia.
 
Itoe China kwenye list yako maana kuna kijana wa wahuni alikamatwa watu wakahonga gesi kijana akaachiwa hata rumande tu hakuingia.
Hizo ni story za kusadikika na ni ajabu kwa mtu mwenye akili timamu kuziamini.
 
Weka na Thailand hapo
 
China ni uongo.kuna mtoto wa kigogo ambaye Naye Kwa Sasa ni kigogo aliwahi kukamatwa huko china kati ya 2012,2013 au 2014 akiuza madawa ya kulevya lakini baba yake akaweka mambo sawa na rais wa china hadi akafutiwa KESI na Kuja nyumbani haraka.
 
Hukumu za madawa ya kulevya inategemea ila trafficking ni hatari kokote pale ,hiyo hata human trafficking kesi yake ni nzito.

Kuna drug dealers ,drug users na drug trafficking : Trafficking ni hatari hasa ukiwa raia wa kigeni, drugs users hawa sio wa kukamata ni wa kupewa msaada kupelekwa sober tena wanajulikana kbisa ,Drugs dealer ni mapap huwezi kukamata maana mpaka uwakute na ushahidi.


Yote tisa , trafficking ni hatari sana ,china unaweza kuwaona wamepunguza makali kwa raia wa bongo ila kuna sababu za mahusiano mazuri baina ya China na Tz ..Kuna mazingira serikali inaweza kusaidia adhabu ikawa ya size ya kati kutokana na ushikiriano.​
 
Hiyo namba 7 sidhani maana mwaka juzi katik jamaa zangu kipindi cha jk walokamatwa china wakahukumiwa kunyokwa(kama utakumbuka kuna tetesi ziliwahi toka kuwa kuna mtoto wa jk kakamata na mzigo huko pamoja na watanzania wengine)jamaa yangu nae alikuwepo kuzi hapa 2022 karudi mzimaa kaachiwa na amerudi na sasa kaingia kwenye kilimo analima dodoma huko.
 
Achaneni na Stori za kutunga,Yaani kabisa Riz1 abebe sembe yeye mwenyewe?Inaweza ikawa kweli ni Supplier lakini kwa akili ya kawaida Baba wakati ule ni number 1,Yeye abebe mzigo mwenyewe kweli?
Hiyo story ilitungwa vizuri sana,ukifikiria ni kitu ambacho ni none sense!haiwezekani,Baba Raisi !sinachota tu na kukupa hela,hakuna wa kumwuliza
 
China ni uongo.kuna mtoto wa kigogo ambaye Naye Kwa Sasa ni kigogo aliwahi kukamatwa huko china kati ya 2012,2013 au 2014 akiuza madawa ya kulevya lakini baba yake akaweka mambo sawa na rais wa china hadi akafutiwa KESI na Kuja nyumbani haraka.
Hizo ni story za kusadikika hakuna ukweli wowote.
 
China ukikamatwa na kiasi cha chini ya kg1 hunyongwi bali unafungwa jera tu.
 
Hizo ni story za kusadikika na ni ajabu kwa mtu mwenye akili timamu kuziamini.
Unaweza kutuambia wale wachina wanaobeba gesi kule Mtwara wanabeba kwa mkataba upi? Hivi hujui kuwa ngada asilimia kubwa inayoingia nchini ni biashara ya born town? kwa kifupi wewe ndio hujui kitu. Kina kisa cha maafisa wa TRA na Police waliokama gari imejaa ngada, katika kuiwakilisha wakachomoa kiasi kadhaa, uliza afisa vipenyo walichowafanya katika harakati ya kurudisha mzigo uliopigwa baada ya mwenye mzigo kudai mzigo uliokamatwa sio uliowakilisha wakati wanamkabidhi mzigo wake. Kama unaenelea kubisha fika kota za TRA Kurasini ulizia kisa cha Afisa mapato aliefia lupango kilikuwa je na mzigo ulipatikana wapi na nani aliupata?
 
Weka ushahidi wa haya unayo yaongea sio kuleta story za masikani ya wavuta bangi.
Ya kwamba Riziwan awe punda wa kubeba madawa ya kulevya tumboni na kuhangaika nayo kwenye viwanja vya ndege?
 
Njia rahisi ni kuwakamata mateja wote mtaani na kuwauliza wanapata wapi, ukimkamata supplier atakwambia, nani ana ingiza au kuzalisha nchini, kisha unaifuata chain yote, na kumaliza tatizo.

Watawala ndio wamiliki wa chain nzima, ukitaka kujua ingiza unga wako, anzisha chain yako ya kuuza, ndani ya siku mbili watakuwa na taarifa na watatangaza operation kusaka wauza unga.
 

Nchi nyingi sana za Asia ya Kusini, ukikamatwa na Madawa ya Kulevya (Narcotics) adhabu yake ni Kunyongwa hadi kufa. Wana Sheria zao Kali Sana.

Isipokuwa nchini China kuna baadhi ya maneno na Majimbo, ukikamatwa na madawa ya kulevya haunyongwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…