Hizi ndio nchi kumi Afrika zenye uwezo mkubwa wa kijeshi

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,971
Reaction score
14,538
Habari zenu ndugu zangu wakubwa kwa wadogo.

Leo nimeangalia katika BBC Swahili nikakutana na list ya nchi kumi za Afrika zenye uwezo mkubwa kijeshi.

Ki ukweli hii list imenishangaza kuona baadhi ya nchi ambazo zimeshindwa hata kuleta amani au hata kutuliza hali ya usalama katika nchi zao zikishika nafasi ya nchi zenye uwezo wa kijeshi huku nchi zinazoonekana kuwa imara, mahiri na zenye uwezo halisi wa kijeshi zikikosekana katika list.

Mfano wa nchi hizo ni Tanzania, Botswana, Rwanda nk. List ya nchi hizo zinazosemekana kuwa zina uwezo wa kijeshi ni hii

1) Misri
(2) Algeria
(3) South Africa
(4) Nigeria
(5) Ethiopia
(6) Angola
(7) Morocco
(8) Sudan
(9) Democrat Republic of Congo
(10) Libya.
 
Inawezekana neno 'uwezo mkubwa' labda limekuwa gumu kwako...
  • Ukubwa wa bajeti ya jeshi
  • Ukubwa wa jeshi (idadi ya wanajeshi)
  • Ukisasa wa jeshi (Vifaa na utaalam/intelijensia)
Hayo ndio walau mambo matatu yanayoweza amua uwezo wa jeshi...
 
sijajua kigezo gani kimetumika kumuweka DRC kwenye list
 
Yah tena eti imeshika nafasi ya tisa mbele ya Libya.
 
Inawezekana neno 'uwezo mkubwa' labda limekuwa gumu kwako...

  • Bajeti ya jeshi
  • Ukubwa wa jeshi
  • Ukisasa wa jeshi (Vifaa na utaalam)

Hayo ndio walau mambo matatu yanayoweza amua uwezo wa jeshi
Labda hapo kwenye ukubwa wa jeshi lkn kwa ukisasa na bajeti sizani kama Congo wanatushinda.
 
Akili za kuambiwa changanya na zako.
Boko Haram imeitesa Nigeria mwaka wa ngapi huu?
Ethiopia ilipambana na kajikabila kamoja ikasalimu amri Sasa hivi hicho kijikabila kimekua nchi huru.
DRC ipi unayoongelea wewe?
 
Kama hiyo ndio sababu basi Congo hii list haiwahusu, Nigeria [emoji1184] huko boko haraam wanawanyanyasa wanavyojiskia.
 
Hivi Congo ina intelijensia kubwa kuliko Tanzania, Kenya, Rwanda na nchi zingine ambazo hazipo kwenye list? Kama wana intelijensia kubwa kama hiyo unayoongelea mbona wameshindwa kuleta amani au kutambua mahali yalipo makundi ya wanamgambo kwa zaidi ya miaka 20 sasa? Hata M23 imesambaratika baada ya majeshi ya Tanzania kupelekwa Congo kupambana nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…