Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

inategemea kwako unamaanisha mshahara mkubwa ni sh ngapi. kwa mimi hapo sioni hata taasisi moja inayolipa mshahara mkubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada nikupe tu TAARIFA WATUMISHI wengi NI WATUMISHI wa kawaida wasokua na vyeo

Na mshahara wa MWISHO wa mtumishi wa serikali NI sh 2,727,500/- unless km ana cheo km mkuu wa KITENGO au idara au mkuu wa taasisi msikaririshane Mambo ambayo hayapo na nkupe tu TAARIFA huyo ambaye yupo TRA mwenye degree anaeanza Kazi Hana tofauti na mwenye degree ya maendeleo ya JAMII wa Moshi vijijini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na serikalini kinachowaokoa WATUMISHI baadhi ya taasisi NI maposho na upigaji taasisi km NAOT pale MISHAHARA NI ya kawaida

ila Kazi zao NI za field trip Sana hivyo kinawabeba posho

SERIKALINI watu wanafanyia njaa tu lakini hakuna MISHAHARA ya namna hiyo ila NI vimishahara vya kizalendo tu ili vipunguze gap la walonacho na wasonacho na ndio maana kuna walimu hawawez jenga mpk wapate pension unakuta mwalimu huyo kaishia 1,480,000/- pamoja na kufanya Kazi miaka 40 au 35

Bro Mambo yaone nje tu ila ndani balaa MISHAHARA mpk Sasa miaka 5 Sasa inakaribia hakuna MISHAHARA mipya


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kujipa moyo binti kiziwi, ujue kuna taasisi zinazalisha pesa tena bila kutumia mtaji mfano kama TPA, EWURA, TBS n.k kwanini zisiwamwagie mishahara minono watu wake.
Lete ile pale ya JKT kigoma. Malizia,uliishia ulipomuona askari mrembo anafanana na Sophia. Au ulikuwa unacopy mahala?. Halafu mwenyewe ameichana chana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…