Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Una maanisha JWTZ?? Kama ndio hivyo haipo mzee.. Jamaa wanalipwa pesa ya kawaida tu.
Pesa ya kawaida wakati mtu mwenye diploma tu anakula 2M+ we unaiita hela ya kawaida hio kwa level ya mishahara ya kibongo?
 
Tena kwa organization mtu wa bachelor anakula hata zaidi ya milion tano kumzidi Prof wa chuo kikuu usishangae tembea uone. Hata huko sijui TRA sijui wapi hyo milion mbili na kitu si mishahara ya Senior wa zaidi ya miaka kumi na tano kazini
Organization gani madam? Sehemu pekee ambayo kuna mishahara ya kufa mtu ni kwenye international NGO’s tu! Tena unapo sign contract tu straight away hamna cha kupoteza miaka.

Huko ndio kulipwa 4-10M ni mishahara ya kawaida kwa cadre zote.

Ila private zetu za akina Gurjit au Premsingh huko mwendo wa laki 2 tu before makato. Ukienda tena kwa akina Wu Jin Hao ama Sheng Dong ndio utasogezwa kwenye laki 4 hapo! Ni huzuni kwa kweli
 
Pesa ya kawaida wakati mtu mwenye diploma tu anakula 2M+ we unaiita hela ya kawaida hio kwa level ya mishahara ya kibongo?
Mkuu, hii mishahara ya wanajeshi mnayoweka hapa mnaitoa wapi aisee?

Kwanza Jeshini hawalipi kwa Elimu.

Elimu Jeshini inakusaidia tu kupanda cheo baada ya kufanya kozi, hicho cheo ndio Chenye mshahara.

Mkuu sikudanganyi, Mimi ninao washkaji zangu nimemaliza na form 4 wengi sana wako Jeshini. Kuanzia Lugalo, Makongo, Kunduchi, Navy Kigamboni, Abdallah Twalipo Kurasini kote hakuna sehemu Sina jamaa niliyesoama naye. Police na magereza ndio usiseme.

Mimi sikupenda tu kuwa Askari.

Tena wengine wanna degree kabisa.

Mishahara ya Askari Ni ya kawaida kabisa. Na kibaya zaidi hawana Uhuru, wako busy mnooo.

Kitu pekee unachoweza kufaidi ukiwa Jeshini labda uende mission nje ya nchi.

Kuna ndugu yangu ( naye nimesoma naye) alienda Sudan akarudi na 30M hadi akataka kuacha kazi.

Sasa hivi imeisha anatamani kwenda tena.
 
Mkuu, hii mishahara ya wanaishi mnayoweka hapa mnaitoa wapi aisee?

Kwanza Jeshini hawalipi kwa Elimu.

Elimu Jeshini inakusaidia tu kupanda cheo baada ya kufanya kozi, hicho cheo ndio Chenye mshahara.

Mkuu sikudanganyi, Mimi ninao washkaji zangu nimemaliza na form 4 wengi sana wako Jeshini. Kuanzia Lugalo, Makongo, Kunduchi, Navy Kigamboni, Abdallah Twalipo Kurasini kote hakuna sehemu Sina jamaa niliyesoama naye. Police na magereza ndio usiseme.

Mimi sikupenda tu kuwa Askari.

Tena wengine wanna degree kabisa.

Mishahara ya Askari Ni ya kawaida kabisa. Na kibaya zaidi hawana Uhuru, wako busy mnooo.
Duh wanajeshi nao mishahara yao ya laki 4?
 
2.340M ni entry level kwa mtu mwenye Degree na overtime ya 234000 ambayo hutalipwa kama upo likizo tuuu so entry level ni kama 2.6M kwa bachelor Diploma ni 1.856M Mama Junior akiongeza May inaweza kuwa taasisi inayolipa vizuri zaidi.
Hio mishahara ni mikubwa ukifanya average ya mishahara ya watumishi anaelipwa 2.6M anaishi maisha comfortably sana. Gari utaendesha na kodi utalipa ya nyumba standard na nzuri tu.

Ukiwa mchumi mzuri unaweza kuwekeza kabisa ukawa na biashara zinazokuingizia pesa kama extra.

Mishahara midogo ni ya less than 1.2M hasa kwa hali ya uchumi ya sasa.
 
Duh wanajeshi nao mishahara yao ya laki 4?
Nakumbuka mwaka 2010 nilikuwa naishi na jamaa yangu Askari Magereza ( Warder) alikuwa analipwa Tsh 119,000 basic na ration ya 100,000.

Mpaka naondoka 2012 basic yake ilikuwa Ni 175,000 na ration ya 100,000.

Baadaye Kikwete aliongeza mishahara ya Watumishi nahsis atakuwa kwenye 400,000 au 500,000.

Kuna mwingine JWTZ yeye alikuwa anapata 500,000 basic. Baadaye akaenda kufanya kozi ya MP akaongezewa 35,000 na ana degree.

Jamani mishahara ya serikali Ni midogo mno, labda uwe kwenye mashirika ya umma yanayokusanya mapato ndio mnaweza kujipangia per diem na mishahara.
 
Mkuu hao TPDC ni mwisho kuna mdau yupo pale mwaka mmoja tu ila loan bord kashamalizana nao mapema na mijengo ya maaana
Hahahah af watu wanasema serikalini hamna ishu! Inategemea upo wapi mkuu!

Private ofisi gani ya mwafrika itakulipa 2M+ ukianza kazi tu? Jibu ni hapana labda iwe ni NGO ya kimataifa ya mzungu. Na hapo wabongo wasipewe usimamizi maana mshahara hata kama ulikuwa ni 4M mtalipwa 2M ili hio 2M waipige wao!😅
 
Sajent darasa la Saba au form four ila mishahara yao utafananisha na msomi wa kada nyingine na mwenye ujuzi, bado mwenye nyota kwenda juu.
Tatizo watu wakisikia jeshi wanawaza vile vyeo vya chini tu! Kuna jamaa mmoja ni sajenti alikuwa anawaambia raia eti wasiwashadadie sana maofisa na kuwadharau wao maaskari!

Sababu hao maofisa wengi huwa wanapenda starehe na anasa hawajui kutumia pesa zao vizuri! Na wakati mwingine wakifulia wanawakopa maaskari ambao raia wanawadharau!

Akawa anaelezea mafanikio yake kibiashara pamoja na kwamba ni mwanajeshi wa cheo cha chini! So unaona kabisa kwamba tatizo siyo mshahara bali ni matumizi ya mtu binafsi!
Kuna captain wa jeshi leo kanikopa elfu 20,sasa sijui huo mshahara wake huwa haumtoshi au vipi?
Wanajeshi wanapaishwa sana mishahara yao sio mikubwa kama watu mnavyosema humu ndani.
Tatizo humu watu wanachanganya vitu mada imeelezea taasisi zenye mishahara mikubwa yaani ni entry level ikimaanisha kwamba huo ni mshahara wa degree ambae ndo anaanza kazi kwa mara ya kwanza kwenye hio taasisi.
Sasa watu mnaanza kusema kuna masajenti wanalipwa zaidi ya hizo amount zilizotajwa hapo na kuwa hao masajenti level yao ni form four hivi mnajua huyo mtu mpaka kuwa sajenti imemchukua miaka mingap ???
Na je tukichukulia mtu ambae yupo ega na ana elimu sawa na huyo sajenti na wote wamekaa kazini kwa muda sawa unafikiri nani atakuwa na mshahara mkubwa kumzidi mwenzake ???

Kwa tanzania wanajeshi bado hawajazidi hizo scale tajwa hapo juu
Mfano mwepesi tu kuwe na HR wawili wote wasome chuo kimoja halafu wote waajiliwe kwa pamoja mmoja jeshini mwingine eGA kwa mshahara wa kuanzia lazima huyu wa eGa utakuwa juu zaidi kuliko wa mwanajeshi kwa hiyo wanajeshi msiwatukuze sana mishshara yao ni ya kawaida.
 
Tra ndio maana inapendwa sana na graduates wanatangaza nafasi 7 watu wanaomba zaidi ya 3900, maana yake tra inaonyesha pengine labda kuna pesa.
Ndio maanaake mzee, hapo hata jamaa yako mliekuwa mkishinda kijiweni akiajiriwa ndani ya mwaka tu utashangaa anatembelea premio T 723 ESF na kiwanja kanunua Goba ukianza mwaka mpya anaanza ujenzi ndani ya miezi 6 tu..Hujakaa sawa na mishe mishe za kuoa zinaanza😅! TRA paacheni tu kuna mengi mazuri!

Kwa hali kama hio unategemea kwanini nafasi ikitoka msiigombanie tu?
 
Kwenye kila Kampuni kuna range ya mishahara kuanzia ya chini mpaka ya juu!! Hivi vikampuni vidogo vidogo ndio vinavyolipa mishahara minono sana kuliko mijikampuni yenye majina makubwa!! Kuna Dogo wa kitaani ameajiriwa kampuni ndogo to anakunja "MIGUU SITA" aka MILIO 6 aka Meter 6 hiyo inayoingia BANKWA.
Hio kampuni head lazma awe mzungu tu na kampuni ya madini labda au Supplies Co. inayofanya kazi na kampuni kubwa ama serikali.

Vinginevyo hamna namna HR wala CEO mtanzania mwenzio atakulipa 6M kaka tusidangayane. Top lazma awe mzungu au mfaransa hapo tutaelewana.
 
A

fiSa II wa TRA yoyote anaanzia 2.7 hiyo ndo tra scale ya sasa 4.1 scale, unakatwa laki 4 ya tra hapo hpo, inabaki 2.3 nfo makato mengine yanafuata baada ya makato ni around 1.68 mil take home hiyo, naongea nikiwa nasoma mkataba wa mwaka huu wa mshikaji wangu wa karibu sana.

Tuzidi kusaidiana kwa data zaidi ili tuujue ukweli, jamani nataka kujua kuhusu hawa NAOT najua mshahara tgs E ni wq kawaiiida sana, vip posho zip jamani mwenye data halisi tusaidiane ikiwezekana nataka nitoke private nalipwa 900,000 niingile setikalin database audit, kabla sijaanza kujiumiza na hizi interview ningependa nipate data kwa wazalendo wenzangu kutoka kwenye hii forum.
Watu basi wanazungumziaga gross salaries! Ndio maana inaonekana kama udanganyifu.
 
Kwa Ifficer 2 hii ndio gross salary zao in accordance with the row
1. TPDC​
1.8m​
2. TCRA​
3.5m​
4. Ngorongoro​
1.8m​
3. Ewura​
1.8m​
4. WCF​
2.0m​
5. TBS​
1.8m​
5. TANAPA​
1.8m​
5. Tume ya madini​
hawa below 1.5m​
6. Mamlaka ya chakula na dawa​
1.7m​
7. SSRA​
2m​
8. NSSF/PSSSF​
2m​
9. BOT​
1.8m​
9. Bunge​
Hawa below 1m​
9. Ofisi ya mkemia mkuu wa serikali​
Hawa sijajua​
10. TASAC​
2m​
10. TRA​
2.3m​
11. MSD​
1.8m​
11. TAKUKURU​
Sijajua bado​
11. EGA​
3.07m​
12. NHIF​
1.7m​
13. TPA​
1.6m​
13. TIC​
Sijui bado​
14. KADCO​
hawa below 1.5m​
15. TANESCO​
1.2m​
16. TANROAD​
Sijui bado​
17. TAA​
1.35m​
Uko sahihi mkuu.. kuna taasisi kama 7 nafahamu hizo ndo salary zake hapo
 
Niliajiriwa kampuni moja, nilikuwa nalipwa hela kiduchu tu na degree yangu(600k) take home plus accommodation (nyumba,chakula,umeme, maji)

Hiyo sio story wadau!!

Aisee nilikuta kuna jamaa wanavuta mpunga mrefu sana na wengi wabongo tu....Nilibahatika kuwa rafiki na human resources manager alikuwa ananihamasisha sana... Alivunja maadili ya kazi yake na kuniambia mishahara ya wadau nilichoka kuna mbongo tulikuwa naye alikuwa anavuta dola elfu 10.

Huyu boss wangu mwenyewe alikuwa anavuta 8m alikuw na Masters by then na akawa ameomba kupiga PhD. Na hiyo 8m sio kwamba ni mkongwe kazini hapana alikuwa na kama mwaka tu alikuja pale kwenye kampuni akitokea Barrick.

Hatimaye mkataba ulipoisha niliamua kutembea. Kikubwa nilichojifunza kwa boss wangu ili ulipwe vizuri inabidi uwe na qualifications konki, wakati naondoka alinisisitiza sana sana nisome [emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna maeneo kadri ukiwa na elimu ndio mishahara inakuwa mikubwa ila its worthless kama upo nje ya mfumo!

Binafsi naona serikalini ndio pazuri kufanya hio aina ya investment ya muda na akili. Private unaweza soma kisha ukatimuliwa unaenda kuwa machinga mwenye phd
 
Katika degree zote hapa Tanzania degree yenye mshahara mkubwa mkiajiriwa serikalini ni udaktari ndo inaongoza

Kuna Md,Dds,Dvm then wanafuata manesi(bsc nursing) na engineers

Hii ni kwa sabab serikalini scale ya mshahara ya kuanzia huwa wanaangalia degree uliyosoma ni ya miaka mingap
Ndo maana madaktari( Md,Dds na Dvm) ndo huwa wana mshahara Mkubwa kuliko degree zingine kama engineers ambazo ni miaka minne

So kama daktari na engineer wataajiriwa sehem moja kwa wakat mmoja ie halmashauri daktari atakuwa na mshahara mkubwa kidogo kuliko mhandisi


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mshahara mkubwa ndio hio 1.5m? Hebu kuwa serious kidogo basi mkuu...Toka naskia habari za hawa MD sijawahi kuona mahali imeandikwa hata wanalipwa 2M
 
Back
Top Bottom