Hizi ndio Taasisi zenye mishahara minono Tanzania

Una maanisha JWTZ?? Kama ndio hivyo haipo mzee.. Jamaa wanalipwa pesa ya kawaida tu.
Pesa ya kawaida wakati mtu mwenye diploma tu anakula 2M+ we unaiita hela ya kawaida hio kwa level ya mishahara ya kibongo?
 
Tena kwa organization mtu wa bachelor anakula hata zaidi ya milion tano kumzidi Prof wa chuo kikuu usishangae tembea uone. Hata huko sijui TRA sijui wapi hyo milion mbili na kitu si mishahara ya Senior wa zaidi ya miaka kumi na tano kazini
Organization gani madam? Sehemu pekee ambayo kuna mishahara ya kufa mtu ni kwenye international NGO’s tu! Tena unapo sign contract tu straight away hamna cha kupoteza miaka.

Huko ndio kulipwa 4-10M ni mishahara ya kawaida kwa cadre zote.

Ila private zetu za akina Gurjit au Premsingh huko mwendo wa laki 2 tu before makato. Ukienda tena kwa akina Wu Jin Hao ama Sheng Dong ndio utasogezwa kwenye laki 4 hapo! Ni huzuni kwa kweli
 
Pesa ya kawaida wakati mtu mwenye diploma tu anakula 2M+ we unaiita hela ya kawaida hio kwa level ya mishahara ya kibongo?
Mkuu, hii mishahara ya wanajeshi mnayoweka hapa mnaitoa wapi aisee?

Kwanza Jeshini hawalipi kwa Elimu.

Elimu Jeshini inakusaidia tu kupanda cheo baada ya kufanya kozi, hicho cheo ndio Chenye mshahara.

Mkuu sikudanganyi, Mimi ninao washkaji zangu nimemaliza na form 4 wengi sana wako Jeshini. Kuanzia Lugalo, Makongo, Kunduchi, Navy Kigamboni, Abdallah Twalipo Kurasini kote hakuna sehemu Sina jamaa niliyesoama naye. Police na magereza ndio usiseme.

Mimi sikupenda tu kuwa Askari.

Tena wengine wanna degree kabisa.

Mishahara ya Askari Ni ya kawaida kabisa. Na kibaya zaidi hawana Uhuru, wako busy mnooo.

Kitu pekee unachoweza kufaidi ukiwa Jeshini labda uende mission nje ya nchi.

Kuna ndugu yangu ( naye nimesoma naye) alienda Sudan akarudi na 30M hadi akataka kuacha kazi.

Sasa hivi imeisha anatamani kwenda tena.
 
Duh wanajeshi nao mishahara yao ya laki 4?
 
2.340M ni entry level kwa mtu mwenye Degree na overtime ya 234000 ambayo hutalipwa kama upo likizo tuuu so entry level ni kama 2.6M kwa bachelor Diploma ni 1.856M Mama Junior akiongeza May inaweza kuwa taasisi inayolipa vizuri zaidi.
Hio mishahara ni mikubwa ukifanya average ya mishahara ya watumishi anaelipwa 2.6M anaishi maisha comfortably sana. Gari utaendesha na kodi utalipa ya nyumba standard na nzuri tu.

Ukiwa mchumi mzuri unaweza kuwekeza kabisa ukawa na biashara zinazokuingizia pesa kama extra.

Mishahara midogo ni ya less than 1.2M hasa kwa hali ya uchumi ya sasa.
 
Duh wanajeshi nao mishahara yao ya laki 4?
Nakumbuka mwaka 2010 nilikuwa naishi na jamaa yangu Askari Magereza ( Warder) alikuwa analipwa Tsh 119,000 basic na ration ya 100,000.

Mpaka naondoka 2012 basic yake ilikuwa Ni 175,000 na ration ya 100,000.

Baadaye Kikwete aliongeza mishahara ya Watumishi nahsis atakuwa kwenye 400,000 au 500,000.

Kuna mwingine JWTZ yeye alikuwa anapata 500,000 basic. Baadaye akaenda kufanya kozi ya MP akaongezewa 35,000 na ana degree.

Jamani mishahara ya serikali Ni midogo mno, labda uwe kwenye mashirika ya umma yanayokusanya mapato ndio mnaweza kujipangia per diem na mishahara.
 
Mkuu hao TPDC ni mwisho kuna mdau yupo pale mwaka mmoja tu ila loan bord kashamalizana nao mapema na mijengo ya maaana
Hahahah af watu wanasema serikalini hamna ishu! Inategemea upo wapi mkuu!

Private ofisi gani ya mwafrika itakulipa 2M+ ukianza kazi tu? Jibu ni hapana labda iwe ni NGO ya kimataifa ya mzungu. Na hapo wabongo wasipewe usimamizi maana mshahara hata kama ulikuwa ni 4M mtalipwa 2M ili hio 2M waipige wao!😅
 
Sajent darasa la Saba au form four ila mishahara yao utafananisha na msomi wa kada nyingine na mwenye ujuzi, bado mwenye nyota kwenda juu.
Kuna captain wa jeshi leo kanikopa elfu 20,sasa sijui huo mshahara wake huwa haumtoshi au vipi?
Wanajeshi wanapaishwa sana mishahara yao sio mikubwa kama watu mnavyosema humu ndani.
Tatizo humu watu wanachanganya vitu mada imeelezea taasisi zenye mishahara mikubwa yaani ni entry level ikimaanisha kwamba huo ni mshahara wa degree ambae ndo anaanza kazi kwa mara ya kwanza kwenye hio taasisi.
Sasa watu mnaanza kusema kuna masajenti wanalipwa zaidi ya hizo amount zilizotajwa hapo na kuwa hao masajenti level yao ni form four hivi mnajua huyo mtu mpaka kuwa sajenti imemchukua miaka mingap ???
Na je tukichukulia mtu ambae yupo ega na ana elimu sawa na huyo sajenti na wote wamekaa kazini kwa muda sawa unafikiri nani atakuwa na mshahara mkubwa kumzidi mwenzake ???

Kwa tanzania wanajeshi bado hawajazidi hizo scale tajwa hapo juu
Mfano mwepesi tu kuwe na HR wawili wote wasome chuo kimoja halafu wote waajiliwe kwa pamoja mmoja jeshini mwingine eGA kwa mshahara wa kuanzia lazima huyu wa eGa utakuwa juu zaidi kuliko wa mwanajeshi kwa hiyo wanajeshi msiwatukuze sana mishshara yao ni ya kawaida.
 
Tra ndio maana inapendwa sana na graduates wanatangaza nafasi 7 watu wanaomba zaidi ya 3900, maana yake tra inaonyesha pengine labda kuna pesa.
Ndio maanaake mzee, hapo hata jamaa yako mliekuwa mkishinda kijiweni akiajiriwa ndani ya mwaka tu utashangaa anatembelea premio T 723 ESF na kiwanja kanunua Goba ukianza mwaka mpya anaanza ujenzi ndani ya miezi 6 tu..Hujakaa sawa na mishe mishe za kuoa zinaanza😅! TRA paacheni tu kuna mengi mazuri!

Kwa hali kama hio unategemea kwanini nafasi ikitoka msiigombanie tu?
 
Hio kampuni head lazma awe mzungu tu na kampuni ya madini labda au Supplies Co. inayofanya kazi na kampuni kubwa ama serikali.

Vinginevyo hamna namna HR wala CEO mtanzania mwenzio atakulipa 6M kaka tusidangayane. Top lazma awe mzungu au mfaransa hapo tutaelewana.
 
Watu basi wanazungumziaga gross salaries! Ndio maana inaonekana kama udanganyifu.
 
Uko sahihi mkuu.. kuna taasisi kama 7 nafahamu hizo ndo salary zake hapo
 
Kuna maeneo kadri ukiwa na elimu ndio mishahara inakuwa mikubwa ila its worthless kama upo nje ya mfumo!

Binafsi naona serikalini ndio pazuri kufanya hio aina ya investment ya muda na akili. Private unaweza soma kisha ukatimuliwa unaenda kuwa machinga mwenye phd
 
Mshahara mkubwa ndio hio 1.5m? Hebu kuwa serious kidogo basi mkuu...Toka naskia habari za hawa MD sijawahi kuona mahali imeandikwa hata wanalipwa 2M
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…