Pamoja na kwamba UZI ni wa siku nyingi na baadhi ya taasisi hazipo tena (SSRA being one of them ) lakini nimeangalia kwa HARAKA HARAKA (kama mleta uzi amefanya utafiti wake vizuri ) over 90% ya hizo taasisi ni service providers, sio production institutes, yaan zinategemea kuchukua either ruzuku au kuchuna sehemu ndio zilipane, mfano SSRA, EWURA nk. Tunawalipa kidogo watu wa muhimu (madaktari, walimu ) halafu tunalipa pesa nyingi kwa taasisi ambazo hata zikifutwa leo wala hazina impact yoyote kwa nchi. Natolea mfano mmoja wa kijinga; hivi mnafahamu over 10 years nauli za mabasi zipo chini zaidi kuliko bei elekezi ya serikali? Lingine fanya hili, tumia tu simu yako ya mkononi, uliza bei za mafuta sehemu uliopo, angalia bei elekezi ya EWURA halafu tembelea baadhi tu ya vituo vya mafuta, utagundua kwamba bei wanayo UZA ipo chini na bei pendekezwa; sababu ya hayo yote ni moja tu, ushindani wa soko unasababisha only wenye mitaji mikubwa kuendelea ku savaivu so why are we paying all of that salaries to those people? I am not saying wafutwe but tuangalie umuhimu wa sekta.