Yap, hao jamaa wanapata mishahara minono sana. ni kitu kizuri kupata pesa na ni baraka kupata pesa, namshukuru Mungu mimi pia Mungu amenipa pesa na heshima kubwa. Jina la Bwana libarikiwe.
hata hivyo, hatutakiwi kujisahau, wakati wa Nuhu ilikuwa hivihivi, watu walikuwa wanakula bata, walikuwa wanaoa na kuolewa (wala sio kitu kibaya), wakiuza na kununua (wala si kitu kibaya kufanya hivyo) walikuwa wanatafuta pesa na maisha na wanafanya anasa na pesa hizo. hivyo hivyo na wakati wa Lutu kabla ya moto kuwaka, walipewa nafasi ya kutubu ila waliendelea kutegemea mambo ya dunia kuliko kumweka Mungu wa kwanza. mwisho wao sote tunaujua. Yesu alionya sana kizazi hiki kisijisahau katika shughuli zake.
Luka 17:26 – 37: YESU AKAWAAMBIA; Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. Watu walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka, ikawaangamiza wote.
Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za LUtu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga; lakini siku ile LUtu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.
Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu. Katika siku ile, aliye juu ya dari, na vyombo vyake vimo ndani ya nyumba, asishuke ili kuvitwaa; na kadhalika, aliye shambani asirejee nyuma. Mkumbukeni mkewe Lutu. Mtu yeyote atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza; na yeyote atakayeiangamiza ataiponya. Nawaambia, usiku huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Wanawake wawili watakuwa wakisaga pamoja, mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa. Watu wawili watakuwa shambani, mmoja atatwaliwa mmoja ataachwa. Wakajibu wakamwuliza, wapi Bwana? Akawaambia, ulipo mzoga ndipo watakapokutanika tai.
Soma pia Mathayo 24:37.- 38 37 Kama ilivyokuwa wakati wa Nuhu, ndivyo itakavyokuwa atakaporudi Mwana wa Adamu. 38 Kwa maana siku zile kabla ya gharika, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka siku ile Nuhu alipoingia kwenye safina.
NAKUSHAURI KWA JINA LA YESU, MPE YESU MAISHA YAKO, OKOKA LEO, MUDA UMEISHA, DUNIA ITAISHA MUDA WOWOTE, pia kama una shida, mtwike yeye shida zako uone kama hatakusaidia,Mungu anakuhitaji sana umgeukie, nafasi hii usiipoteze kwasababu hujui lini mlango utafungwa kwako. Ubarikiwe!