Hizi ndiyo Kazi zinazowafanya watu wasiwe na furaha zaidi nchini Marekani

Hizi ndiyo Kazi zinazowafanya watu wasiwe na furaha zaidi nchini Marekani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kuridhika na kazi si swala la mshahara pekee. Tafiti mbalimbali zimeendelea kuonesha kuwa mambo kama vile viwango vya msongo wa mawazo, usawa kati ya kazi na maisha binafsi, ubora wa uongozi, na mazingira ya kila siku ya kufanyia kazi mara nyingi huchangia kwa kiasi kikubwa zaidi katika kuamua jinsi gani wafanyakazi wanajisikia wenye furaha na amani wanapotekeleza majukumu yao.

1782108958431.png

Kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2025 uliofanywa na Jukwaa la usimamizi wa wafanyakazi, Deputy, kupitia ripoti yake ya mwaka ya Shift Pulse, wafanyakazi wa maduka ya dawa (pharmacies) ndiyo wasio na furaha zaidi kazini nchini Marekani. Utafiti huo ulichambua zaidi ya matokeo milioni 1.5 yaliyokusanywa kati ya Aprili 2024 na Aprili 2025.

Kazi nyingi nchini Marekani ambazo haziridhishi kabisa zina changamoto zinazofanana. Waajiriwa mara nyingi huripoti kufanya kazi kwa masaa mengi, kukabiliana na wateja wasio na adabu au wenye madai makubwa, majukumu ya kujirudia rudia, fursa finyu za kujiendeleza, na viwango vya juu vya shinikizo. Katika baadhi ya taaluma, wafanyakazi pia hukabiliwa na uchovu wa kihisia, kuishiwa nguvu (burnout), na upungufu wa watumishi unaoweza kufanya kazi ambazo tayari ni ngumu kuwa ngumu zaidi.

Wafanyakazi wa madukani, walinzi wa magereza, wahudumu wa vituo vya simu, madereva wa malori na wale wa kusambaza mizigo ni miongoni mwa makundi yanayotajwa mara kwa mara kukabiliwa na viwango vya chini vya kuridhika kazini. Hali hii inajumuisha pia walimu, maafisa wa polisi, wasaidizi wa wauguzi, walinzi, watunza kasiki (cashiers), pamoja na wafanyakazi wa usafi wa majengo (janitors), hoteli, na migahawa ya chakula cha haraka ni miongoni mwa makundi yanayotajwa mara kwa mara kukabiliwa na viwango vya chini vya kuridhika kazini.

Licha ya changamoto za kipekee za kila sekta, wafanyakazi wengi katika maeneo haya wanaripoti kujihisi kutothaminiwa na jamii, ingawa wanatekeleza majukumu ya msingi na muhimu sana yanayofanya maisha ya kila siku yaendane vizuri.

Zaidi ya hayo, kazi hizi bado zinatoa vipato vya uhakika na ujuzi wa thamani uliosaidia mamilioni ya watu kuziendesha familia zao, ikithibitisha kuwa kila taaluma ina pande zote mbili, chanya na hasi.

Je, ni kazi ipi kwenye orodha hii imekushangaza zaidi?

========

One industry has taken the crown for the most miserable job sector in the United States, a new study finds.

Known workforce management platform Deputy released its third annual Shift Pulse Report last month, analyzing more than 1.5 million survey results from data collected between April 2024 and April 2025.

The study included a new metric called the Net Happiness Score, which was determined by asking workers to share their personal sentiments about their respective jobs.

Respondents were able to share if they felt "good" or "amazing" about their work or if they were unhappy with their current setup, for one reason or another.

One job sector stood above the rest as the "unhappiest" in America. Results pointed to those working in pharmacies as having the worst Net Happiness Score, with just 13.94 percent of pharmacy workers giving a positive assessment.

The next three on the unhappiest list were those who worked in delivery and postal services, animal health, and medical clinics.

Conversely, the happiest workers were those who worked in tobacco, e-cigarette and marijuana stores. The industry got a phenomenal happiness score of 91.87 percent.

Other job sectors ranking high in the Net Happiness Score were catering businesses, coffee shops and, surprisingly, dental work.

The data also identified the happiest workers by state.

South Carolina, Virginia, and Utah were the top three in that regard. On the other hand, those working in North Dakota, New Mexico and Vermont gave the lowest scores.
 
Back
Top Bottom