Hizi ndiyo sababu kuu maalumu zinazowafanya mashabiki wa Simba SC kugomea kununua tiketi za mchezo wa Simba SC dhidi ya Asec

Hizi ndiyo sababu kuu maalumu zinazowafanya mashabiki wa Simba SC kugomea kununua tiketi za mchezo wa Simba SC dhidi ya Asec

Zile 5 si mlisema hivyo hivyo leo kikiwapi mnavurugana hata hamjielewi. Wakifungwa nitaenjoy maana kuna vioja vitazuka
Endelea kusubiria meli airport, wakati una kimeo chako hapo kwa Waarabu.
 
Endelea kusubiria meli airport, wakati una kimeo chako hapo kwa Waarabu.
Hahahah sina ushabiki na timu yoyote hapa bongo zaidi nafurahia vibweka vinavyojitokeza kwenye hizi timu sio kila anaechangia kuhusu simba basi ni yanga au kila anaeiponda yanga ni simba usikariri. Akili kisoda
 
Simba wamefungwa mechi moja tuu wanataka kuvunja Team hawajui kuwa huo ni mpira una matokeo ya kikatili sana walifungwa Real Madrid tano wakiwa na wakina Cr 7 nyinyi mkiwa na Boko mnakula Tano mnataka kuandamana aisee...
 
Nafurahi sana kuona ndugu zetu wakiteseka
Hahahaha kutesa kwa zamu. Umesahau juzi tu hapo Mlikuwa mnachangishana kwenye vibakuli?! Mshukuruni GSM Tajiri wa vitendo sio kama huyu Mwamedi blaah blaaah kibao. Mara timu inamvunja moyo mara Timu inatengeneza deficit tu.Pathetic
 
Ukweli usemwe japokuwa ni mchungu, hamasa imekua kubwa sana katika kuwahamsisha mashabiki wa Simba sc lakini mwitikio sifuri.

Zimesambazwa tickets za bure kwenye matawi, viongozi wa Simba sc wanadai kuwa wameshusha kiingilio mpaka elfu 3000 kwa mzunguko Lakini nyuma ya pazia ni bure.

NALIA NGWENA nawapa sababu za mashabiki wa Simba sc kususia kununua tickets za mchezo wa Asec mimos utakaopigwa tare 25/11.

Mosi, kipigo kitakatifu (mbwa mwizi) walichokishuhudia mashabiki wa Simba sc dhidi ya mtani wao, hii imewanyong'onyesha sana mashabiki na kujiona kuwa hawana timu.

Pili, Matokeo mabovu ya Simba sc kwenye mechi za kimataifa, mashabiki wanajua kuwa hata wakihudhuria matokeo mazuri kwao ni sale tu tofauti na hapo labda wachezee kichapo.

Ikumbukwe toka Simba sc ianze kushiriki michuano hii ya kimataifa msimu huu haijawahi kushinda Bali imetoka sale michezo yote mpaka kufuzu makundi.

Tatu, mashabiki hawana Imani na kocha Cadena na msaidizi Wake Suleimani matola, mashabiki wanaamini makocha Hawa walioachiwa timu kwa muda mfupi hawana mbinu za kumfunga Asec.

Nne, uongo wa viongozi wa Simba sc akiwemo msemaji wao Ahmedy ally, kiufupi mashabiki wamechoka na wamemzoea kwa porojo zake zisizo na mashiko ukija kwenye uhalisia hakuna kitu.

Tano, kikosi kibovu Cha Simba sc hili lipo wazi haina kikosi Cha kuwafurahisha Wana Simba sc Bali Wana kikosi Cha kuwapa presha mashabiki wa Simba hii NI moja ya sababu kuu inayoifanya mashabiki wasiende uwanjani.

Maoni Yangu: yakifanyiwa kazi hayo, mashabiki watakuja uwanjani pasipo kufanyiwa hamasa ya visipika.

Nawasilisha hoja.
Chanzo ni hiki kwenye Picha,hayo mengine ni magonjwa nyemelezi tu
IMG-20231124-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom