Uchaguzi 2020 Hizi ndiyo sababu zilizompa Dkt. Magufuli ushindi wa kishindo

Uchaguzi 2020 Hizi ndiyo sababu zilizompa Dkt. Magufuli ushindi wa kishindo

Una mtazamo kama wangu kabisa. Nahisi unaongea niliyoyaona hata kabla ya uchaguzi...ukiingia twitter utahisi upo nchi tofauti kabisa. Mpaka nimeamua kujitoa kabisa mana ni chuki tu zinapandikizwa👏👏👏
Umekimbia ukweli
 
MAGUFULI HAKUSHINDA


NIONYESHE MTU MMOJA ALIYESHANGILIA AU KUNDI USHINDI HUO


USHINDI GANI NCHI KAMA INA MSIBA
 
Kwanza natoa pale kwa upinzani hasa CHADEMA kuwa uchaguzi huu sio kama 2015 ambapo kila mtanzania alikuwa amechoshwa na CCM.

Na kila raia alikua tayari kwa lolote ikisubiriwa kauli tu kwamba sasa tuingie barabarani tukichafue.

1. Baada ya Magufuli kuingia 2015 akafuta kazi migambo wote. Hapa wale vijana wasiokuwa na ajira walijiajiri na kufanya kazi kwa uhuru bila bugdha(2015 walikuwa tayari hawa n ni wengi mno)

2. Amefanikiwa kudhibiti matumizi makubwa ya serikali na kubana matumizi.

3. Kuanzisha miradi mingi ya maendeleo. Reli,anga,kuhamia Dodoma, ujenzi wa barabara nyingi

4. Kuondoa baadhi ya urasimu katika ofisi za serikali pamoja na kuwa karibu wananchi. Hii imemfanya aonekane raisi wa wanyonge kweli kweli.

5. Kuleta heshima serikalini,hakuna tena mambo ya "unanijua mm ni nani"? Kila ofisi ya umma unayoenda unapata heshima na kuthaminiwa kuwa ww ndio boss.

6. Kuwapa watu uhuru wa kufanya biashara popote bila shida( ukikimbizwa na 🐕 rusha mifupa kwa nyuma) kwa sasa hakuna vijana wengi wasio na kazi mtaani kama zamani,kila mtu ana mishe zake utamwambia nani aandamane akusikilize?

Suala la kuandamana linahitaji watu wengi wenye hasira kweli kweli.

MY TAKE:
Magufuli sio malaika au Mungu kwa hiyo ana mapungufu yake. Mapungufu yake hayamnyimi heshima yake ya kuongoza awamu ya pili. Vijana wengi kwa sasa wako huru kufanya kazi au biashara zao bila bugdha yeyote toka serikalini kwanini wahangaike na kuandamana?

Ana mke ana majukumu mbalimbali anawaza kuhusu kesho yake akipigwa kwenye maandamano? Uhalisia wa maisha ya mtanzania ni mitaani na sio kwenye mitandao. Mtu anaishi US eti ana hasira na utawala 🤪! Umemkosea nini

"Wizi" kama sababu imo?

Mkuu naomba kuuliza kwanza hilo kabla sijasoma hii makala yako ndefu.
 
Kuapishwa kwake sio kwamba ataongoza taifa kama Mfalme wa miaka 5 iliopita, kashikashi ya vikwazo na vitimbi vipo "LOADING".

Msione wapinzani na mabeberu wapo kimya, wanatunga sheria za kuujeruhi vibaya huu utawala wa kifalme.

Kwa mwenye akili timamu lazima atambue, mabeberu kamwe hawapotezei "DHARAU na DHIHAKA" wanapofanyiwa, hasa kwa nchi hohehae. So kitakacho fuata ni "VIKWAZO" mpaka bei ya chumvi ifike hata elfu sabini au tisini. Ili sisi wananchi akili itusogee tutambue makosa yetu.

1) Upumbavu wetu wa kutokudai "TUME HURU NA KATIBA".

2) Nyinyi wana lumumba mtambue makosa yenu ya "KUUNGA MKONO KILA KITU". Maana hata mgeambiwa mtoe wake zenu sadaka au mvue suruali, mgeunga mkono.
Kama wewe unavyounga mkono upinzani na mabeberu wao.
 
Nitafanyaje wakati mkuu wa majeshi ni msukuma mwenzake na mkuu wa polisi wote Kanda ya ziwa pia na mkuu wa TISS. Yeye kuua anaona kitu Cha kawaida kwa ajiri ya madaraka halafu anaona mungu ni binamu yake
Mbona na wewe ni kanda ya ziwa au unadhani hatukujui..tunaona hizo rrrrrr siyo za popote zaidi ya Mara na huko ndiyo kumejaa upinzani ingawaje kila mara Mbowe anawapiga chini. Ninyi mnamsema Magufuli kuhusu Lissu mbona mnamsahau Chacha Wangwe kuhusu Mbowe. Ulimwengu mzima unajuwa jinsi Mbowe alivyohusika na kifo cha Chacha Wangwe.
 
1.NEC
2.NEC
3.NEC

Usalama/Police hao ni Subset ya hapo juu.
 
Kawakosea nini hao mabeberu mpaka wampe kikwazo? Hii ni tofauti na Zimbabwe bob. Tuna mali nyingi sana nchii ambazo mabeberu wanazitaka,waweke vikwazo tukimbilie China na Urusi.
Now it's all about diplomatic win win situation
Wakiweka vikwazo watapata wapi izo malighafi
 
Usitudanganye bwana. Sababu zilizompa ushindi wa kishindo ni wizi na kuingiza mabox ya Kura vituoni tayari yameshapigwa Kura kwake. Na pia sababu nyingine ni kuwaengua au kuwatoa mawakala almost asipimia tisini vituo vya kupigia kura na kuwaacha mawakala pekee wa ccm. Tatu sababu nyingine ni kuzima mitandao ya kijamii ili wizi ufanyike kirahisi bila watu kujua kinachoendelea. Nayo mwabhatama.
Uwongo mtupu but skulaumu mana mfa maji haishi kutapatapa
 
Back
Top Bottom