Hizi ndizo changamoto kuu mbili mradi wa treni ya mwendokasi Dar ~ Moro

Hizi ndizo changamoto kuu mbili mradi wa treni ya mwendokasi Dar ~ Moro

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Serikali ina wazo zuri.

Serikali imeamua kuleta maendeleo hasa miundombinu ya usafiri.

Mradi wa treni ya mwendokasi Dar Moro ambayo itakuwa inasafiri kwa speed ya 160 km/hr ni idea nzuri sana.Tatizo la mradi huu ni :-

1. Umeme wa uhakika muda wote treni iwapo kazini (?)

2. Reli zetu haziko secured huko maporini.Raia wengi huchezea ama kwa kunyofoa vyuma vya reli au kutakua au kugongo-gonga. Hasa wafugaji wakiwa na mbuzi zao huko porini reli inakokatiza.

Serikali ijipange kushughulikia mambo haya makubwa mawili. Otherwise treni inaweza safiri kwa hiyo speed then katikati ya pori unakuta wamasai wamenyofoa vyuma vya reli. Au hata mafuriko tu kama kule Godegode Kongwa.

Ambao mmesafiri nchi za Ulaya mtakuwa mmeona namna reli za wenzetu zinavyochekiwa mara kwa mara kwa sensors na pia zimekuwa protected ili zisiingiliwe na wavamizi.
 
Kuhusu usalama wa reli kuna haja ya kuwa na sheria kali kwa ajili hiyo; aomething like Critical Infrastructute Protection Act. Ukikamatwa na hata nati ya miundombinu ya reli adhabu yake ni kifo. Bila hivyo tutakuwa hatutoboi.
 
Kiwanda ni kiwander huo umeme sio kiwander
 
Kuzuia wanyama na watu inaweza kuwekwa fensi - hii ni lazima kwa treni za kasi. Wizi ni patrols na technologia za security. Kuhusu umeme - railway itakua na grid yake na inapewa kipaumbele kama kuna mgao na pia zina weza kuwepo emergency generators kila station kutoa umeme wa dharura au kuweka vichwa vya diesel kila station kuvuta mabehewa mpaka station unapokatika umeme.
 
Hakuna mkakati wa kuimarisha shughuli za kiuchumi reli inakopita ili reli hiyo ipate mzigo wa kubeba ijiendeshe kibiashara
 
Mi naomba niongezee swali
Je kinachotushinda kuiendesha TAZARA kwa ufanisi kimepata ufumbuzi na kwamba changamoto za TAZARA hazita kuwepo kwa hiyo ya umeme?
Tatizo la Tazara ni ownership structure ndio inayosumbua ktk mgt.

Tatizo la TRL ni kuwa hakuna uzalendo
 
Mi naomba niongezee swali
Je kinachotushinda kuiendesha TAZARA kwa ufanisi kimepata ufumbuzi na kwamba changamoto za TAZARA hazita kuwepo kwa hiyo ya umeme?

Mfumo wa kuendesha TAZARA ni mgumu kwani wa Zambia ndiyo huwa on top na Tanzania wanabaki wasaidizi. Lazima wskubaliane mikataba ibadilishwe kwanza
 
Reli hii ni tofauti sana na ile ya zamani.Reli hii najua itachomewa (welded) kwenye maungio huta sikia yale makelele kama hiyo ya sas.Na pia itazungushiwa uzio njia yote.Zitawekwa sehemu za wavuka kwa miguu,magari,wanyama na mambo mengine
 
Mawazo yako na hofu zako ni Nzuri Mkuu

kwa uelewa wangu mdogo ni:

1.Mradi wa umeme wa Stigliers gorge 2100MW ukikamilika ambao ni sAMBAMBA NA Ujenzi wa reli tatizo la umeme kukatika linaweza kuwa solved kwa kiasi fulani,

pili nafikiri sensor zaweza tumika katika kulinda reli na njia yake ,pia wajenzi lazima waweke/namna ya kuzuia hayo...hiyo inaweza kuwepo kwenye TOR...Terms of reference ya tender kabla mzabuni hajapata kazi.
 
Mfumo wa kuendesha TAZARA ni mgumu kwani wa Zambia ndiyo huwa on top na Tanzania wanabaki wasaidizi. Lazima wskubaliane mikataba ibadilishwe kwanza
Na TRL ambayo tunaimiliki 100% mbona nayo hali yake ni tia maji tia maji?
 
Tatizo la Tazara ni ownership structure ndio inayosumbua ktk mgt.

Tatizo la TRL ni kuwa hakuna uzalendo
Kama TRL hakuna wazalendo; serikali itapata wapi wazalendo wa kuendesha hiyo ya umeme? Au itakodi wazalendo toka nje ya nchi?
 
Serikali ina wazo zuri.

Serikali imeamua kuleta maendeleo hasa miundombinu ya usafiri.

Mradi wa treni ya mwendokasi Dar Moro ambayo itakuwa inasafiri kwa speed ya 160 km/hr ni idea nzuri sana.Tatizo la mradi huu ni :-

1. Umeme wa uhakika muda wote treni iwapo kazini (????)

2. Reli zetu haziko secured huko maporini.Raia wengi huchezea ama kwa kunyofoa vyuma vya reli au kutakua au kugongo-gonga. Hasa wafugaji wakiwa na mbuzi zao huko porini reli inakokatiza.

Serikali ijipange kushughulikia mambo haya makubwa mawili. Otherwise treni inaweza safiri kwa hiyo speed then katikati ya pori unakuta wamasai wamenyofoa vyuma vya reli.Au hata mafuriko tu kama kule Godegode Kongwa.

Ambao mmesafiri nchi za Ulaya mtakuwa mmeona namna reli za wenzetu zinavyochekiwa mara kwa mara kwa sensors na pia zimekuwa protected ili zisiingiliwe na wavamizi.
Kwanza umedhalilisha kabila la wamasai kana kwamba ndo wafugaji peke yao, pili umelinganisha dunia ya tatu na nchi zilizoendelea kwenye mambo ya reli. Kumbuka kila mahali ambapo kuna reli nchi za wenzetu kuna daraja kama flyover ambayo wenda kwa mguu au magari yanapita juu yake au chini ya daraja. Je sisi tumeshaandaa haya? Mtu unatenganishwa na shamba lako na hujajengewa daraja la kuvuka utafanyaje? Waandae miundo rafiki kwa kila mtu wafugaji, waenda kwa mguu, magari ili reli ibaki salama na taa zisisahaulike.
 
Back
Top Bottom