Hizi ndizo noti zitakazoondolewa kwenye mzunguko kuanzia Januari 06 hadi Aprili 05 mwaka huu

Hizi ndizo noti zitakazoondolewa kwenye mzunguko kuanzia Januari 06 hadi Aprili 05 mwaka huu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka watanzania kuziwasilisha noti za zamani za shilingi ya Tanzania katika ofisi za BoT pamoja na benki zote za biashara na kupatiwa malipo yenye thamani ya kiasi kitakachowasilishwa katika zoezi linalotarajiwa kuanza Januari 6, 2025 hadi Aprili 5, 2025.

Zoezi la kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani linahusisha shilingi Ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1,000), elfu mbili (2,000), elfu tano (5,000), elfu kumi (10,000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi 2003 pamoja na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010.
IMG_2220.jpeg
 
Kuna harufu ya kutakatisha fedha hapa.

Chukulia kuna mtu alizitunza hizi hela akashindwa ziingiza kwenye mzunguka(labda hazikuwa halali ikawa ngunu kuziweka bank) akazichimbia tuu ndan. Muda wa matumizi ukaisha .Zikakosa thamani.

Wataalamu wakaleta tangazo zinakusanywa maana ake alizokuwa nazo anazipeleka benk anapewa hela zinazotumika sa hivi( Hivyo fedha zilizokosa thamani mwazo zinarudi kuwa na thamani upya).

Swali la kujiuliza Ni nani unadhan hizi noti anazo na ikawaje akawa nazo wakati tushazisahau labda kwacudogo hiyo miatano hapo , Ila hizo zingine zote ukimkuta mtu yuko nayo ni kama urembo. Hivyo kuna ka harufu nakanusa hapa sio kazuri
 
Kuna harufu ya kutakatisha fedha hapa.
Chukulia kuna mtu alizitunza hizi hela akashindwa ziingiza kwenye mzunguka akazichimbia tuu ndan. Muda wa matumizi ukaisha .Zikakosa dhamani.

Wataalamu wakaleta tangazo zinakusanywa maana ake alizokuwa nazo anazipeleka benk anapewa hela zinazotumika sa hivi( Hivyo fedha zilizokosa dhamani mwazo zinarudi kuwa na dhamani upya).

Swali la kujiuliza Ni nan unadhan hizi noti anazo na ikawaje akaw nazo wakati tushazisahau labda hiyo kidogo miatano hapo , ila hizo zingine zote ukimkuta mtu yuko nayo ni kama urembo. Hivyo kuna ka harufu nakanusa hapa sio kazuri
Kwamba wanataka kubebana?
 
Jua Kuna wastaafu wa miaka hiyo Wana hizo pesa. Hivyo Tulia
Umewaza kwa akili Ila Tulia hakuna namna
 
Hizo noti za miaka 90 ina maana zilikuwa kwenye mzunguko bado? Mbona watu walishazisahau?

Au wanatafuta kitu kipi?

Hii ni dalili ya wazi ya kuwepo kwa harufu ya ufisadi kwenye suala hili. Kwa nini Benki Kuu inataka kukusanya noti za Fedha ambazo hazipo kwenye mzunguko? Ni Mwanchi gani huko uraiani ambaye bado anamiliki Fedha hizo?
 
Jua Kuna wastaafu wa miaka hiyo Wana hizo pesa. Hivyo Tulia
Umewaza kwa akili Ila Tulia hakuna namna
You are completely wrong.

Fedha hizo tayari zilishaondolewa kutoka kwenye mzunguko kwa Tangazo maalumu la Serikali (Government Notice, GN) ambalo ni Sheria ya nchi kwa mujibu wa Katiba. Kama kuna Mtu ambaye bado anaendelea kumiliki noti hizo basi anafanya hivyo kinyume kabisa na Sheria za nchi, ni Kitendo cha uvunjaji wa Sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom