Sijakuunga mkono bali nimekupa fact, Namibia ilikuwa koloni la Ujerumani na ilikuwa chini ya udhamini kama Tanganyija lakini mbona walipigana vita virefu kudai uhuru, Ghana uganda na Zambia walikuwa makoloni lakini wakipata uhuru kwa amani kana Tanganyika hapo unasemaje.
Nyerere huyo unayembeza alihukumiwa kwa uchochezi, alikuwa anatembea kwa miguu toka shule ya sekondari Pugu hadi Lumumba kushughulikia masuala ya TANU na kurudi jioni, pugu ya wakati ule ilikuwa misitu yenye simba sio kama unavyoiona leo. Uchaguzi wa kura tatu ulikuwa mgumu kwa TANU kwa sabqbu mkoloni alijua kuwa Tanu hata ikifanya vizuri itaambulia theluthi ya viti ambqvyo ni vya weusi tu lakini Tanu chini ya Nyerere waliunga mkono wagombea wao wazungu na waasia na kupata ushindi uliomshangaza mkoloni halafu unasema uhuru ulipatikana kirahisi!. Kwa taarifa yako mkoloni alitengeneza scheme ili Tanganyika iwe kama Rhodesia.