Hizi ndizo Shahada za Heshima na Tuzo alizotunukiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Nyerere alikua mwanadamu First Class kwakweli, wakati Mungu anamuumba alifanya kazi ya ziada. Alikua tofauti na binaadamu wengi hasa wa afrika. Natumaini anakula zake bata Peponi huko.
 
The cooked history!!---Koloni la Tanganyika baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia lilikabidhiwa kwa Waingereza kutoka kwa Wajerumani ni likaitwa the British protectorate ili baadaye tujekupewa uhuru wetu hii ni tofauti na Kenya na uganda ambao Wao walikuwa ni British colonies, Nyerere aka take advantage hiyo na mchakato ukafanyika wa kwenda UNO nk, na akapewa nchi kiulaini tofauti na wenzetu Kenya nk, waliomwaga damu kupigania uhuru wao, sasa Utasemaje Nyerere alipigania Uhuru, kupigana unakujua??!🤣
Inabidi urudi primary school ujifunze historia na kiswahili kwanza. Kupigania uhuru haimaanishi kushika silaha tu. Huko UNO nani alienda kudai uhuru? Nani aliigeuza TAA kuwa TANU? Nani aliongoza harakati za kuwaunganisha watanganyika kudai uhuru? Yote hayo alifanya Nyerere. Nyerere huyo unayembeza aliacha kazi ya heshima ya ualimu ili aongoze harakati za kudai uhuru, baba/ babu yako aliyekuwepo wakati huo alitoa mchango gani? Hata kqdi ya TANU aliogopa kukata. Aliyeongoza watanganyika kushiriki uchaguzi wa kwanza wa kura tatu ambapo TANU ilizoa viti vyote kasoro kimoja alikuwa Nyerere. Unadhani uhuru ulikuja mezani kama sahani ya wali!.

Namibia ilikuwa koloni la Ujerumani pia mbona hawakupata uhuru hadi SWAPO iliposhika silaha na kuendesha mapambano kwa muda mrefu?

Uganda, Ghana na Zambia hawakuwa ptotectorate bali koloni mbona walupata uhuru bila ya kumwaga damu.

Nyerere tangu mwanzo alichagua kudai uhuru kwa njia ya amani.

Kama unapenda kujua mambo tenga muda kidogo upitie nyaraka na hoja za wataalamu mbalimbali ili kujijengea uelewa kabla ya kuqndika.

Hili jukwaa lilikusudiwa kuwa mahali pa fikra pevu sio uwanja wa kutema chuki.
 
Nyerere hakuiacha nchi kwenye umaskini mkubwa kuliko huu ulioko sasa. Wacha wanachanganya kwani wakati ule mambo kwa nchi zote yalikuwa ni tofauti na sasa. Wakati wa Nyerere watu walikuwa wanasoma bure, wanatibiwa bure na kulikuwa na nyumba za National housing kwa wafanyakazi. Wanafunzi walikuwa wanasafiri bure kwa kutumia ''warrant''. Tulikuwa na mashirika ya umma mengi. Watoto wa maskini walikuwa wanasoma bure na kugombea nafasi za kiasiasa hakuhitaji uwe na fedha. Kiwango cha elimu kilikuwa juu ukilinganisha na sasa.
Unazungumzia enzi zipi hizo?!

Yaani unatumia kigezo cha elimu bure wakati waliokuwa wanapata fursa yenyewe ya elimu walikuwa wachache sana kutokana na kutokuwa na shule za kutosha!!

Ni vijiji vingapi vilikuwa na vituo vya afya?!

Leo hii tuna mgao wa umeme lakini wakati ule kulikuwa na mgao wa kupata sabuni na sukari!

Na enzi zile hakukuwa na matatizo ya umeme sio kwa sababu tulikuwa na umeme mwingi bali Watanzania hatukuwa na access na vifaa vinavyohitaji matumizi ya umeme!

Mwalimu wa shule enzi zile aliheshimika sio kwa sababu alikuwa analipwa vizuri bali kwa sababu, mtaani ungekuta ni Mwalimu pekee ndie mwenye kipato cha uhakika!

Nenda hata Uswahilini kisha uliza watoto 10 randomly "kiraka ni nini"! Usishangae ukakuta wengine hawajui kiraka ni nini!!

Hivi enzi za Mwalimu kuna mtoto ambae alikuwa hajui kiraka ni nini wakati majority walikuwa wanavaa nguo zenye viraka?!
 
Inashangaza Mwalimu kupata shahada zote hizo za heshima, na bado hakuwahi kujiita Dokta!

Sasa hawa wenzangu na mimi, kashahada kamoja tu ka heshima; tayari mtaani hakukaliki.
Msukuma yeye alununua kwa matapeli wa kinaigeria, hawa wengine wanapewa kisiasa tu ndio maana tunaona ni University za tz tu ndizo zinazotunuku hizo shahada
 
Unazungumzia enzi zipi hizo?!

Yaani unatumia kigezo cha elimu bure wakati waliokuwa wanapata fursa yenyewe ya elimu walikuwa wachache sana kutokana na kutokuwa na shule za kutosha!!

Ni vijiji vingapi vilikuwa na vituo vya afya?!

Leo hii tuna mgao wa umeme lakini wakati ule kulikuwa na mgao wa kupata sabuni na sukari!

Na enzi zile hakukuwa na matatizo ya umeme sio kwa sababu tulikuwa na umeme mwingi bali Watanzania hatukuwa na access na vifaa vinavyohitaji matumizi ya umeme!

Mwalimu wa shule enzi zile aliheshimika sio kwa sababu alikuwa analipwa vizuri bali kwa sababu, mtaani ungekuta ni Mwalimu pekee ndie mwenye kipato cha uhakika!

Nenda hata Uswahilini kisha uliza watoto 10 randomly "kiraka ni nini"! Usishangae ukakuta wengine hawajui kiraka ni nini!!

Hivi enzi za Mwalimu kuna mtoto ambae alikuwa hajui kiraka ni nini wakati majority walikuwa wanavaa nguo zenye viraka?!
Ndiyo. walikuwa wanapata elimu walikuwa wachache lakini nchi ilikuwa na watu wachache pia. Pia walipa kodi na vyanzo vya kodi vilikuwa vichache. Tuache visingizio.
 
Vita inasingiziwa
Ila ndo Ukweli, maka michache toka nchi ipate Uhuru, Nchi inaingia Vitani, na Vita inayumbisha Uchumi wa Nchi!

Nyerere anaweza kulaumiwa kwa Vitu vingine kama Vijiji vya Ujamaa, japo kama ilivyo kwa Baba wa Familia, unajaribu kufanya hili ama lile ili Familia iweze kupata uhakika wa Maisha mazuri, japo kuna wakati mambo yanaharibika unajaribu mipango mingine.
 
Ndiyo. walikuwa wanapata elimu walikuwa wachache lakini nchi ilikuwa na watu wachache pia. Pia walipa kodi na vyanzo vya kodi vilikuwa vichache. Tuache visingizio.
Hivi huoni wewe ndo unaleta visingizio?!

Kwamba nchi ilikuwa na watu wachache ndo maana waliokuwa wanapata elimu ni wachache?! SERIOUSLY?!

Be honest, hata kwa kukisikia tu, na asilimia ngapi ya wanafunzi waliokuwa wanavuka Darasa la VII na kuingia Form I?!

Mikoani sifahamu lakini wakati nikiwa na akili zangu timamu, Dar es salaam kulikuwa na Tambaza, Azania, Jangwani, Zanaki, Kisutu, Kibasila, Forodhani, na Kibasila!

Yaani Temeke YOTE kulikuwa na Kibasila TU! Hivi Kinondoni kulikuwa na shule ya sekondari?! Au nimesahau!!

Kwenye mkoa wako wa asili kulikuwa na shule ngapi za serikali za sekondari?

Hivi hata kama population ilikuwa ndogo, hapo kulikuwa na uwiano wowote kati ya idadi ya shule na watu?!

Hivi nchi haikuwa na bidhaa muhimu kwa sababu vyanzo vya kodi na walipa kodi walikuwa wachache au tulikuwa na mfumo mbovu wa kiuchumi ambao ulitegemea mashirika ya umma ambayo baadae yalikosa efficiency na kuwa less productive?
 
Pumba
 
Nilibahatika kutembea nchi za Scandinavia hususani Finland na Norway. Nilichogundua ni kuwa mfumo wao wa maisha hauna tofauti kubwa sana na ule ambao Nyerere alikuwa ameujenga. Kwa mfano nchi kuwa na mashirika na viwanda vya umma, kuhakikisha wananchi hawapishani sana kwa vipato hivyo nchi kutokuwa na matabaka ya matajiri sana na mafukara sana. Tangu kipindi hicho nimekuwa najiuliza: yale mashirika ya umma na viwanda vyote alivyoanzisha Mwalim mbona vilikufa lakini huku vina maendeleo mazuri? Inawezekana tatizo likawa ni watu na siyo mfumo? Kwamba sisi waafrika, hususan watanzania, hatuna uwezo wa kujitawala hivyo chochote tunachaanzisha hakidumu? Mbona basi nchi za Scandinavia wamefanikiwa? Je, ni sahihi kumlamu aliyeanzisha wakati sisi ndiyo tuliharibu?
Tatizo Nyerere alitaka utawala wa mtu mmoja asiyehojiwa wala kukosolewa. Tena alikuwa na mpango wa kutawala “milele”. Hivyo alihakikisha mhimili wake wa uRais ndio final. Shida ya mfumo wa aina hiyo unategemea sana UTII USIOHOJI (UNQUESTIONING LOYALTY) wa viongozi na watendaji serikalini na kwenye vyombo vya dola. Kuwa na wasaidizi/wafuasi modeli ya RM Kawawa.

Sasa watu wa aina hiyo sifa yao kuu ni uchawa. Na wengi ni mafisadi. Hawana au hawatumii taaluma na weledi. Wao ni kucheza na akili ya bosi tu. Ndio Nyerere aliowajaza kwenye uongozi wa serikali na mashirika ya umma. Watu kama kina Mtei aliwaona vibaraka wa mabeberu na hatari kwa utawala wake. Hao machawa alikuwa akiwafungamanisha na siasa za TANU/CCM na hakuwa namna ya kuwadhibiti.

Nchi za Scandinavia zilikuwa zinafuata itikadi ya social democracy. Zilikuwa na mifumo thabiti ya kiuongozi, kisiasa, kiuchumi, kijamii, n.k. Ufuatiliaji na usimamizi wa mashirika ya umma ulikuwa wa uhakika. Hautegemei mtu mmoja. Walikuwa na mabunge makini na taasisi imara za kodi, fedha, na udhibiti.

Nyerere alishindwa hata ku-define “Ujamaa” ni itikadi gani? Alidai haina tafsiri. Actually ilikuwa ni ukomunisti uliovishwa joho la social democracy. Hakuwa tayari kujibu maswali ya wadau wa kimataifa kuthibitisha itikadi anayoifuata.

MUHIMU zaidi alikuwa na nia ya dhati ya kuiendeleza Tanzania. Na aliamini anaweza kufanya hivyo peke yake (single handedly) na kubeba utukufu wote kama alivyotuaminisha kwenye “kuleta uhuru 1961”! Hakuwa mwizi wala fisadi. Alihakikisha kila senti inaenda kuhudumia uchumi na wananchi. Ndipo heshima yake ya kipekee ilipo. Alifeli pakubwa katika kujenga nchi imara; akaishia kutuachia zimwi la CCM tunalohangaika nalo leo hii.
 
Umenena vyema. Mwalimu aliamini ujamaa wake. Bahati mbaya hakupata waumini wenzake. Waliomzunguka walikuwa wakisubiri fursa ya kutekeleza nia zao ovu.
Kichekesho wote wanadai kumuenzi.
 
Mwalimu mpaka leo amebakia kuwa proud ‘Edinburgh University’ alumni kila baada ya miaka kadhaa chuo kinaandaa sherehe za Nyerere day.

On his day students and guest scholars wa African studies wanazungumzia his political philosophy and legacy (ya mwisho imefanyika week chache tu nyuma).

Hata asingepewa hizo Doctorates za heshima bado uwezi kuondoa his reasoning ability.

Hizi Doctorates za JK, Samia, Msukuma et al ni sawa na paka wa ndani kupewa jina la simba tu; atabaki kuwa paka. Hao watu hawana reasonability ya kuitwa Drs atawakitunukiwa na vyuo mia.

Kumwita bi tozo, Dr Samia akubadili uwezo wake wa kufikiri.
 
Tatizo Nyerere alitaka utawala wa mtu mmoja asiyehojiwa wala kukosolewa. Tena alikuwa na mpango wa kutawala “milele”. Hivyo alihakikisha mhimili wake wa uRais ndio final. Shida ya mfumo wa aina hiyo unategemea sana UTII USIOHOJI (UNQUESTIONING LOYALTY) wa viongozi na watendaji serikalini na kwenye vyombo vya dola. Kuwa na wasaidizi/wafuasi modeli ya RM Kawawa.

Sasa watu wa aina hiyo sifa yao kuu ni uchawa. Na wengi ni mafisadi. Hawana au hawatumii taaluma na weledi. Wao ni kucheza na akili ya bosi tu. Ndio Nyerere aliowajaza kwenye uongozi wa serikali na mashirika ya umma. Watu kama kina Mtei aliwaona vibaraka wa mabeberu na hatari kwa utawala wake. Hao machawa alikuwa akiwafungamanisha na siasa za TANU/CCM na hakuwa namna ya kuwadhibiti.

Nchi za Scandinavia zilikuwa zinafuata itikadi ya social democracy. Zilikuwa na mifumo thabiti ya kiuongozi, kisiasa, kiuchumi, kijamii, n.k. Ufuatiliaji na usimamizi wa mashirika ya umma ulikuwa wa uhakika. Hautegemei mtu mmoja. Walikuwa na mabunge makini na taasisi imara za kodi, fedha, na udhibiti.

Nyerere alishindwa hata ku-define “Ujamaa” ni itikadi gani? Alidai haina tafsiri. Actually ilikuwa ni ukomunisti uliovishwa joho la social democracy. Hakuwa tayari kujibu maswali ya wadau wa kimataifa kuthibitisha itikadi anayoifuata.

MUHIMU zaidi alikuwa na nia ya dhati ya kuiendeleza Tanzania. Na aliamini anaweza kufanya hivyo peke yake (single handedly) na kubeba utukufu wote kama alivyotuaminisha kwenye “kuleta uhuru 1961”! Hakuwa mwizi wala fisadi. Alihakikisha kila senti inaenda kuhudumia uchumi na wananchi. Ndipo heshima yake ya kipekee ilipo. Alifeli pakubwa katika kujenga nchi imara; akaishia kutuachia zimwi la CCM tunalohangaika nalo leo hii.
Intereting. Kwa nini basi tusiliondoa hilo zimwi wakati alifariki 1999? I mean kwanini tunakubali kuendela kuishi na zimwi kwa miaka yote hiyo wakati mwenyewe hayupo?
 
Mwalimu mpaka leo amebakia kuwa proud ‘Edinburgh University’ alumni kila baada ya miaka kadhaa chuo kinaandaa sherehe za Nyerere day.

On his day students and guest scholars wa African studies wanazungumzia his political philosophy and legacy (ya mwisho imefanyika week chache tu nyuma).

Hata asingepewa hizo Doctorates za heshima bado uwezi kuondoa his reasoning ability.

Hizi Doctorates za JK, Samia, Msukuma et al ni sawa na paka wa ndani kupewa jina la simba tu; atabaki kuwa paka. Hao watu hawana reasonability ya kuitwa Drs atawakitunukiwa na vyuo mia.

Kumwita bi tozo, Dr Samia akubadili uwezo wake wa kufikiri.
Ndiyo maana mimi binafsi nashangaa ilikuwaje pamoja na reasoning ability kubwa ameasisi kitu ambacho kinalalamikiwa na kila upande. Nakusudia mfumo wa muungano wetu.
 
Intereting. Kwa nini basi tusiliondoa hilo zimwi wakati alifariki 1999? I mean kwanini tunakubali kuendela kuishi na zimwi kwa miaka yote hiyo wakati mwenyewe hayupo?
Nyerere hayupo lakini kaacha chama chini ya warithi wenye maslahi makubwa na chama hicho. Aliowaachia madaraka wmejifunza mbinu za kuendelea kutawala kwa kutumia udikteta wa dola (state dictatorship).

Wameigeuza CCM kuwa chama dola kikamilifu (state party). Wanatumia ugaidi wa dola (state terrorism) dhidi ya wakosoaji na wapinzani, wanagawa vyeo na maslahi kwa patronage, na wako tayari hata kuua mtu yeyote anayehatarisha maslahi ya chama dola. It’s a police state.

Lengo kuu sio tu kuitoa CCM madarakani bali kuweka utawala wa demokrasia nchini. Of course CCM kama ilivyo lazima ipanguliwe. Bila shaka juhudi za katiba mpya zinalenga huko. Bila mapambano ya kumwaga damu Nina shaka sana kama mabadiliko hayo yatawezekana. The stakes are quite high. Ndio maana nimesema Nyerere alituachia zimwi la CCM. Hiyo ndiyo failure yake kubwa sana. Mgogoro unaolitesa taifa bila mwisho kuonekana!
 
Ni halali hata asiwe na tamaa ya kuiba wala kufanya ubadhirifu wa mali ya uma hadi familia inajuta baba kuwa rais

Vyeti vikiwa vingi mali haifai kitu
 
Ujamaa haukumuangusha bali kilichomuangusha ni kujitolea sana kuzisaidia nchi zingine zijitawale na baadaye ile vita na Iddi Amin ikahitimisha ! Matatizo yakaanzia hapo baada ya wakubwa huko Duniani kumlazimisha Mwalimu ashushe thamani ya pesa ya Tanzania ndio wakubali Nchi ikopeshwe na IMF na World Bank hapo Mwalimu akakataa ndipo matatizo yaongezeka !! Lakini kabla ya hapo maisha yalikuwa mazuri na rahisi sana !! Sisi tulikuwepo lakini ninyi wengi mnahadithiwa tu !!
Kwa ujumla kiuchumi tulikuwabora zaidi wakati wa Mwalimu kuliko sasa.

Tulikuwa mpaka na viwanda vya kuunganisha magari makubwa na matrekta.

Tulikuwa na kiwanda cha kutengeneza baiskeli aina ya swala, baiskeli nzuri kabisa

Kiwabda chaa matairi bora kabisa, siyo hizi takataka za China.

Viwanda vya nguo nzuri kabisa, siyo hizi takataka za China.

Kiwanda cha viatu vya ngozi, safi kabisa, siyo hizi takataka za China.

n.k. n.k.

Na sarafu yetu kabla ya 1982 ilikuwa shilingi 1 dola 5, pauni 20.
 
Duh, maphd yote haya, kweli Nyerere alipendwa huo duniani
Nyerere hata ungemchukia, usingeweza kuidhihaki au kuikataa intelligence yake. Katika marais wote tuliowahi kuwa nao, kwa kipimo chochote kile, hakuna aliyeukaribia uwezo wa akili yake. He was super intelligent.
 
Back
Top Bottom