Ujamaa haukumuangusha bali kilichomuangusha ni kujitolea sana kuzisaidia nchi zingine zijitawale na baadaye ile vita na Iddi Amin ikahitimisha!
Mwalimu alianza vizuri sana, and I'll always respect him for that lakini ni yeye mwenyewe ndie alikuja kuyavuruga yale ambayo alikuwa ameyaanzisha!!
Hakika, sumu kubwa ya uongozi ni kubaki madarakani muda mrefu!
Lau kama Mwalimu angeanzisha mfumo wa kisiasa ambao, let's say angetoa miaka 5 ya mpito, na bada ya hapo ikaanza 5 to 10 years terms, basi angetoka madarakani akiwa ameacha heshima kubwa sana kiuchumi!
Na kwa upande mwingine, Ujamaa ulimwangusha kwa sababu Ujamaa unahitaji ubabe kwa wanaochezea mali za umma wakati Mwalimu ubabe wake aliufanya kwa wale waliomchezea kisiasa!
Haya mambo ya anayeharibu hapa anahamishiwa kule yalianza tangu enzi za Mwalimu, matokeo yake, hadi anatoka madarakani mashirika yote aliyokuwa ameanzisha yalishakuwa ICU!
Matatizo yakaanzia hapo baada ya wakubwa huko Duniani kumlazimisha Mwalimu ashushe thamani ya pesa ya Tanzania ndio wakubali Nchi ikopeshwe na IMF na World Bank hapo Mwalimu akakataa
Alikataa bila kuwa na sababu za kiuchumi kwa sababu ni kweli shilingi yetu ilikuwa overvalued!
Nchi haikuwa na uwezo hata wa kuwa na viberiti, inaanzaje kuwa na currency yenye thamani kubwa kama ile?! Tulikuwa tuna-export nini cha ku-influence stability ya sarafu yetu?
ndipo matatizo yaongezeka!!
Matatizo yalishaanza kitambo na ndo maana Bretton Woods wakataka kutunasua kwa mikopo!
Lakini kabla ya hapo maisha yalikuwa mazuri na rahisi sana !!
Unazungumzia wakati gani?!
Kwanza, moja ya sababu ambazo zilianza kuvuruga kabisa uchumi wetu ni Vita vya Kagera! Ukiifuatilia vizuri Vita vya Kagera utaona wazi kama Mwalimu asingekuwa na mahaba ya wazi kwa Obotte basi ile vita wala isingetokea!
Lakini kwavile alimuona Amin ni muhuni asiyefaa kuongoza nchi, na kwahiyo Obotte alistahili kurudishwa madarakani, hapo ndipo Mwalimu "akanunua" ugomvi ambao wala haukutuhusu!
Sisi tulikuwepo lakini ninyi wengi mnahadithiwa tu !!
Ina maana huwezi kuuelezea Mkutano wa Berlin kwa usahihi kwa sababu tu wakati huo hukuwepo?!