Hizi ndizo Shahada za Heshima na Tuzo alizotunukiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hizi ndizo Shahada za Heshima na Tuzo alizotunukiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Ujamaa haukumuangusha bali kilichomuangusha ni kujitolea sana kuzisaidia nchi zingine zijitawale na baadaye ile vita na Iddi Amin ikahitimisha ! Matatizo yakaanzia hapo baada ya wakubwa huko Duniani kumlazimisha Mwalimu ashushe thamani ya pesa ya Tanzania ndio wakubali Nchi ikopeshwe na IMF na World Bank hapo Mwalimu akakataa ndipo matatizo yaongezeka !! Lakini kabla ya hapo maisha yalikuwa mazuri na rahisi sana !! Sisi tulikuwepo lakini ninyi wengi mnahadithiwa tu !!
Angalau nimekumbuka, shuleni walikuwa wanatugawia daftari, penseli, kifutio, kichingeo, rula na hakuna ada
 
Nyerere hata ungemchukia, usingeweza kuidhihaki au kuikataa intelligence yake. Katika marais wote tuliowahi kuwa nao, kwa kipimo chochote kile, hakuna aliyeukabia uwezo wa akili yake. He was supwr intelligent.
Kwanini alikuwa hajiiti Dr?
 
Inashangaza Mwalimu kupata shahada zote hizo za heshima, na bado hakuwahi kujiita Dokta!

Sasa hawa wenzangu na mimi, kashahada kamoja tu ka heshima; tayari mtaani hakukaliki.
Nyerere hakuwa na tamaa za kipuuzi ndiyo maana hakuwahi kuitwa Mhe au Dr
 
Kama wasovieti wangekuwa wanampa pesa nyingi asingelazimika kwenda kuomba mkopo wa IMF na World Bank na ndicho kilichopelekea yeye kuachia madaraka kuliko kukubali masharti aliyopewa ya kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania. !!
Mwl.alisoma na kuelewa dalili za nyakati hakuona wapi atapata msaada alichagua kuto kubaliana na masharti ya taasisi za fedha ya nayo endeshwa na mataifa ya kibepari, mwl, aliamini kuyakubali masharti ya kibepari ktk nchi nikulipeleka taifa shimoni ni bora kutakata na kuamua kung'atuka madarakani.maamuzi ya mwl, Nyerere kung'atuka na kuliacha gari bovu liwaangukie wengine ni maamuzi ya HOFU.
 
Inabidi urudi primary school ujifunze historia na kiswahili kwanza. Kupigania uhuru haimaanishi kushika silaha tu. Huko UNO nani alienda kudai uhuru? Nani aliigeuza TAA kuwa TANU? Nani aliongoza harakati za kuwaunganisha watanganyika kudai uhuru? Yote hayo alifanya Nyerere. Nyerere huyo unayembeza aliacha kazi ya heshima ya ualimu ili aongoze harakati za kudai uhuru, baba/ babu yako aliyekuwepo wakati huo alitoa mchango gani? Hata kqdi ya TANU aliogopa kukata. Aliyeongoza watanganyika kushiriki uchaguzi wa kwanza wa kura tatu ambapo TANU ilizoa viti vyote kasoro kimoja alikuwa Nyerere. Unadhani uhuru ulikuja mezani kama sahani ya wali!.

Namibia ilikuwa koloni la Ujerumani pia mbona hawakupata uhuru hadi SWAPO iliposhika silaha na kuendesha mapambano kwa muda mrefu?

Uganda, Ghana na Zambia hawakuwa ptotectorate bali koloni mbona walupata uhuru bila ya kumwaga damu.

Nyerere tangu mwanzo alichagua kudai uhuru kwa njia ya amani.

Kama unapenda kujua mambo tenga muda kidogo upitie nyaraka na hoja za wataalamu mbalimbali ili kujijengea uelewa kabla ya kuqndika.

Hili jukwaa lilikusudiwa kuwa mahali pa fikra pevu sio uwanja wa kutema chuki.


Mimi sitemi chuki bali natema ukweli na ndio maana hata wewe umeniunga mkono ninaposema Nyerere hakupigania uhuru wa nchi hii na umeniunga mkono unaposema Nyerere alidai uhuru wa nchi hii, kumbuka kuna tofauti kati ya kudai na kupigania, Nyerere alienda UNO kudai uhuru wetu kutoka kwa Waingereza, uhuru wetu Muingereza alikabidhiwa na League of Nations kutoka kwa mjerumani, Kenya ndio ilipigania uhuru wake kutoka kwa Muingereza, unakumbuka vita vya maumau??.

Sina chuki na yeyote bali nasema kweli yote na ukweli utakuweka huru.
 
Kwanini alikuwa hajiiti Dr?
Nimefanya kazi na hawa wenzetu weupe kutoka mataifa yaliyoendelea, unaweza kuwa unafanya naye kwa miaka kadhaa na wala usijue hata ana PhD. Sisi huku kwetu, mtu hata akapata PhD kwa kubumba, kila akijitambulisha utasikia, mimi naitwa Doctor ......

Kuna ule msemo wa lugha yetu ya Kiswahili: Maskini akipata matko hulia mbwata.

Na mwingine ufananao:

Debe tupu halikose kupiga kelele.
 
Viongozi wanaojielewa hawapendi tukuzwa
 
Nimefanya kazi na hawa wenzetu weupe kutoka mataifa yaliyoendelea, unaweza kuwa unafanya naye kwa miaka kadhaa na wala usijue hata ana PhD. Sisi huku kwetu, mtu hata akapata PhD kwa kubumba, kila akijitambulisha utasikia, mimi naitwa Doctor ......

Kuna ule msemo wa lugha yetu ya Kiswahili: Maskini akipata matko hulia mbwata.

Na mwingine ufananao:

Debe tupu halikose kupiga kelele.
Wengi ni maprof lakini hawajiiti hata kidogo
 
Ndiyo maana mimi binafsi nashangaa ilikuwaje pamoja na reasoning ability kubwa ameasisi kitu ambacho kinalalamikiwa na kila upande. Nakusudia mfumo wa muungano wetu.
Ni model ya muungano wa aliposemea UK; kautoa huko.
 
Lakini akaiacha Nchi kwenye umaskini mkubwa
Siyo kweli, Nyerere ameiacha nchi na viwanda vya kuzalisha kila kinachoagizwa china leo. Saab scania ilianzishwa mwaka mmoja na iliyoanzishwa Brazil leo Brazil wanaunda scania 95% only 5% wanaagiza Sweden.
Idadi ya mainjinia tulionao leo kubwa sana na ni ajabu bado tuwategemea wachina ambao anayesimamia project ni diploma holder wakujengee madaraja, barabara na majumba.
Niliwahi kufika Mwanza wakati wanajenga Rocky city malls,niliwakuta wachina hata safety gears walizonazo utashangaa,ni viraba vya kucheza Kung Fu.
Tuna tatizo kubwa sana kwenye mifumo ya elimu zetu na haswa kipindi hiki, mtu anajisikia sifa kuitwa engineer sasa nenda kaone kazi zake Sasa!!
Nimewahi kuona mashine ya kuchonga vyuma iliyoundwa Mang'ula machine tools mpaka leo inafanya kazi.
Leo kila project 90% contractors Toka nje.
 
Wengi ni maprof lakini hawajiiti hata kidogo
Ni kweli kabisa.

Wenzetu wanajali sana kile ambacho mtu anaweza kukifanya.

Sisi hapa kwetu unamsikia mtu anajiita ni doctor wa uhandisi mitambo, lakini hana uwezo wa kutengeneza hata mkokoteni, ila kila mahali anajitambulisha kuwa yeye doctor wa engineering na ni bingwa kwenye masuala ya mitambo.
 
Nilibahatika kutembea nchi za Scandinavia hususani Finland na Norway. Nilichogundua ni kuwa mfumo wao wa maisha hauna tofauti kubwa sana na ule ambao Nyerere alikuwa ameujenga. Kwa mfano nchi kuwa na mashirika na viwanda vya umma, kuhakikisha wananchi hawapishani sana kwa vipato hivyo nchi kutokuwa na matabaka ya matajiri sana na mafukara sana. Tangu kipindi hicho nimekuwa najiuliza: yale mashirika ya umma na viwanda vyote alivyoanzisha Mwalim mbona vilikufa lakini huku vina maendeleo mazuri? Inawezekana tatizo likawa ni watu na siyo mfumo? Kwamba sisi waafrika, hususan watanzania, hatuna uwezo wa kujitawala hivyo chochote tunachaanzisha hakidumu? Mbona basi nchi za Scandinavia wamefanikiwa? Je, ni sahihi kumlamu aliyeanzisha wakati sisi ndiyo tuliharibu?
Mkuu 'macho', umetoa mfano mzuri sana wa hizo nchi za Scandinavia jinsi ilivyoshabihiana na lengo alilokuwa nalo Mwalimu Nyerere kwa Tanzania. Lakini wenye kutaka kupotosha huwa hawafikirii kabisa hizo nchi ulizotaja kwa kutaka tu kuhusisha aliyofanya Mwalimu na Ukomunisti, ili kuweka mlinganisho na mafanikio ya ubepari.

Lakini wakati huo huo wanapotaka kutetea mafanikio ya ubepari wanashindwa kuonyesha nchi yoyote ya kiafrika iliyokumbatia mfumo huo na kupata mafanikio makubwa kwa wananchi wake.

Binafsi nimekwishajiridhisha kabisa kwamba tatizo letu lipo kwenye uongozi. Hatuna viongozi wenye dira ya kutupelekas kwenye mafanikio.
 
Mimi sitemi chuki bali natema ukweli na ndio maana hata wewe umeniunga mkono ninaposema Nyerere hakupigania uhuru wa nchi hii na umeniunga mkono unaposema Nyerere alidai uhuru wa nchi hii, kumbuka kuna tofauti kati ya kudai na kupigania, Nyerere alienda UNO kudai uhuru wetu kutoka kwa Waingereza, uhuru wetu Muingereza alikabidhiwa na League of Nations kutoka kwa mjerumani, Kenya ndio ilipigania uhuru wake kutoka kwa Muingereza, unakumbuka vita vya maumau??.

Sina chuki na yeyote bali nasema kweli yote na ukweli utakuweka huru.
Sijakuunga mkono bali nimekupa fact, Namibia ilikuwa koloni la Ujerumani na ilikuwa chini ya udhamini kama Tanganyija lakini mbona walipigana vita virefu kudai uhuru, Ghana uganda na Zambia walikuwa makoloni lakini wakipata uhuru kwa amani kana Tanganyika hapo unasemaje.

Nyerere huyo unayembeza alihukumiwa kwa uchochezi, alikuwa anatembea kwa miguu toka shule ya sekondari Pugu hadi Lumumba kushughulikia masuala ya TANU na kurudi jioni, pugu ya wakati ule ilikuwa misitu yenye simba sio kama unavyoiona leo. Uchaguzi wa kura tatu ulikuwa mgumu kwa TANU kwa sabqbu mkoloni alijua kuwa Tanu hata ikifanya vizuri itaambulia theluthi ya viti ambqvyo ni vya weusi tu lakini Tanu chini ya Nyerere waliunga mkono wagombea wao wazungu na waasia na kupata ushindi uliomshangaza mkoloni halafu unasema uhuru ulipatikana kirahisi!. Kwa taarifa yako mkoloni alitengeneza scheme ili Tanganyika iwe kama Rhodesia.
 
Nani alikuambia Nyerere alipigania uhuru wa nchi hii??--- na Jomokenyatta alifanya nini??, Samora, Mandela, Mugabe nk hao walifanya nini??.

Nyerere alipewa nchi na Waingereza, just simple.
Chuki kwa Nyerere hazijaamza Leo ma hazitaisha Leo kwa kuwa zimechagizwa na vitu vingi sana. Kuna mtu alisema ukipenda saana au kuchukia saaana uwezo wa kufikiri sawasawa unapotea. Naamini yuko sawa.
 
Mbali na dunia au nje ya dunia? Dunia kijiji hata uwe Equador habari itakufikia tu

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
Kama umeelewa hivyo basi bado umeenda alijojo, nje ya dunia ndiko tunakoishi kwa mujibu wa sayansi ya darasani.

Equador, sijui ulikuwa unalenga kusemaje ILA sikuwa na hiyo maana pia.

Choo gani kimempa hiyo heshima, Jalalani University?
 
Chuki kwa Nyerere hazijaamza Leo ma hazitaisha Leo kwa kuwa zimechagizwa na vitu vingi sana. Kuna mtu alisema ukipenda saana au kuchukia saaana uwezo wa kufikiri sawasawa unapotea. Naamini yuko sawa.


Huyo mtu aliyesema hivyo yupo sawa kabisa kukuhusu wewe pia kwani mapenzi na mahaba yako kwa Nyerere yamepofua uwezo wako wa kujua tofauti kati ya Kudai na kupigania, Nyerere alienda UNO kudai uhuru wala hakuenda UNO au kushika silaha kupigania uhuru wetu.

Mimi sina chuki na yeyote bali ninasema kweli na kama kusema kweli ni chuki basi hilo ni tatizo lako la kushidwa kufikiri kutokana na mahaba yaliyokithiri yaliyopofua akili zako.
 
Back
Top Bottom