Hizi ndizo Shahada za Heshima na Tuzo alizotunukiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Mlengo wa sera ya ujamaa ndiyo uliyomuangusha aiseee
Ujamaa haukumuangusha bali kilichomuangusha ni kujitolea sana kuzisaidia nchi zingine zijitawale na baadaye ile vita na Iddi Amin ikahitimisha ! Matatizo yakaanzia hapo baada ya wakubwa huko Duniani kumlazimisha Mwalimu ashushe thamani ya pesa ya Tanzania ndio wakubali Nchi ikopeshwe na IMF na World Bank hapo Mwalimu akakataa ndipo matatizo yaongezeka !! Lakini kabla ya hapo maisha yalikuwa mazuri na rahisi sana !! Sisi tulikuwepo lakini ninyi wengi mnahadithiwa tu !!
 
Mlengo wa sera ya ujamaa ndiyo uliyomuangusha aiseee
Na kosa lake kubwa ni lile la kukubali kufa na tai yake shingoni. Wenzake wa China baada ya kuona huo Ujamaa ni kaa la moto, miaka ya katikati mwa 1970's waliamua kuuchanganya na ubepari!

Na matokeo yake ndiyo hii China ya sasa! Ila yeye kwa bahati mbaya alikomaa na Ujamaa wake wa kufikirika! na mwisho wa siku matokeo yake ndiyo haya sasa ya kutuachia ccm iliyooza na kunuka ufisadi kila upande.
 
Siyo kweli.
Ni mlinganisho wa nyakati tofauti kabisa na matukio yasiyohusiana.

"Structural Adjustment" mwarobaini alioukataa hadi leo unalalamikiwa duniaNI kote.
 
Na watu wanasahau kwaba hali ya uchumi duniani kote ulikuwa ni ngumu wakati huo.
 
Nadhani Vita vya Uganda vya 1978/79 ndio chanzo kikuu.
Baada ya vita vile uchumi wa nchi ukayumba ndipo mabeberu walipopata nafasi ya kumuadhibu Mwalimu kutokana na ile misimamo yake ya kuzipinga Nchi za magharibi kutokana na unyonyaji wao waliokuwa wakizifanyia nchi changa na hasahasa nchi za dunia ya tatu ! Wakajua lazima atakuja kuomba kukopa fedha ndipo walipokataa kumpa mikopo mpaka kwanza akubali kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania ! Mwalimu akakataa na akasema hawezi kukubali kugeuka jiwe na kuwaumiza wananchi wake. !! Wakati huo nadhani dollar ya marekani ilikuwa ikinunuliwa kwa shs tano za kitanzania kama ntakumbuka vizuri !!
 
Alafu kuna wajinga wanakaa na kumdharau Nyerere... shezi wa head kabisa...
 
Siyo kweli.
Ni mlinganisho wa nyakati tofauti kabisa na matukio yasiyohusiana.

"Structural Adjustment" mwarobaini alioukataa hadi leo unalalamikiwa duniaNI kote.
Mimi sipo huko kwenye Structual Adjustment Programmes (SAP's)!!

Hoja yangu iko kwenye Ujamaa wa Nyerere. Yeye aliamini katika Ujamaa pekee na kuupinga kabisa ubepari; jambo ambalo halikuwa sahihi kwa mtazamo wangu.

Binafsi nitamani kuona baada ya Uhuru, angechagua yale mazuri yote yaliyomo kwenye sera ya Ujamaa! Halafu angechagua tena yale mazuri yote yaliyomo kwenye ubepari! Na mwisho wa siku angekuja na itikadi moja ya nchi yenye mchanganyiko wa Ujamaa na ubepari, kama walivyofanya China.
 
Ujamaa ulimwangusha pesa nyingi alipata kutoa nchi za kisoviet.
 
Hata sasa atujachelewa.
 
Ujamaa ulimwangusha pesa nyingi alipata kutoa nchi za kisoviet.
Kama wasovieti wangekuwa wanampa pesa nyingi asingelazimika kwenda kuomba mkopo wa IMF na World Bank na ndicho kilichopelekea yeye kuachia madaraka kuliko kukubali masharti aliyopewa ya kushusha thamani ya shilingi ya Tanzania. !!
 
Honorary Degree hausomi ila unatunukiwa kutokana na mchango wako kwenye masuala husika hivyo haulipi ada.
Ila wananchi hatuulizwi kuthibitisha kama tuliupenda unga wa yanga uliochanganywa mayai toka marekani, wao wanatuthibitishia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…