Hizi ndoto Zina madhara makubwa, zichukulie kwa uzani mzito

Hizi ndoto Zina madhara makubwa, zichukulie kwa uzani mzito

Ukiona unaota ndoto hizi chukua hatua mapema

Ukiona unaota ndoto hizi, ndugu yangu chukua hatua! Usifikiri ni ndoto tu! Ni Mungu anakujulisha hali yako ya kiroho! Kumbuka ulimwngu wako wa kiroho ndio hali yako ya kimwili na ndio maisha yako halisi hivyo usipuzie

Angalizo: nazungumzia ndoto inayojirudia zaidi ya mara moja!

1: Kuota unafanya mapenzi kwnye ndoto

2: Kuota unakula kwenye ndoto au kunywa

3: Kuota unakula nyama kwenye ndoto

4: Kuota unaogelea

5: Kuota unapaa kama ndege

6: Kuota unaonana na watu waliokufa au kuongea nao

7; Kuota upo makaburini

8: Kuota upo mtoni unaoga

9: Kuota umengatwq na mbwa au kushambuliwa na mbwq

10: Kuota unangatwq na paka au kushambuliwa na paka wengi

11: Kuota unakimbizwa na ngombe mkali

12: Kuota unakimbizwq na nyoka, au kungatwa na nyoka, ukumbwa wa nyoka una maana yake,

Hizo ni baadhi ya ndoto mbaya ambayo hupaswi kuzipuzia ndugu yangu, na kila ndoto hapo ina maana yake, madhara ya ndoto hizi ukizipuzia.

1: Vifo vya ghafula
2: Magonjwa yasiyotibika mfano ukimwi, pressure, kisukari nk
3: Kufa kwenye ajali
4: Migogoro kwenye ndoa
5: Kutokufanikiwa kama wewe umesoma unatafuta kazi hupati na hata kama ukipata unafukuzwa bila sababu
6: Kutokuolewa
7: Umasikini
8:kuasilika nyota yako kukosa mvuto kutawaliwa na mikosi nk
Kama umepangiwa kufa kwenye ajali, utakufa kwenye ajali. Kuota au kutokuota hakutasaidia chochote na hakuna hatua yoyote unayoweza kuchukua kubadilisha hilo.
 
Lets say umeota unakula nyama, ambapo kwa tafsiri yako ni kwamba utakufa kwenye ajali.

Ehe.. hebu niambie utachukua tahadhari gani?

Utaacha kupanda vyombo vya usafiri kwa maisha yako yote?
Wapi nimesema ukiota unakula nyama utakufa kwenye ajali?
 
Swadakta sheikh
Ndoto aina mbili ziliniganda kweli miezi kadhaa nyuma kwa kujirudia rudia. Kwanza nyoka niliwaota kwa siku 3 mfululizo. 1- Nilimuota akiwa anazunguka maeneo ya nyumbani lakini alivyotaka kuning'ata nikastuka. 2- Nilimuota akiwa maeneo yenye watu wengi na hawakuwa wakimuogopa(rangi nyeupe&nyeusi) hata alivyowang'ata walimtoa kiupole, lakini alivyonikaribia nikaanza kukimbia wacha anifuate nyuma. Ikafika mahali nimechoka aliponisogelea nikastuka. 3- Nilimuota nikiwa vichakani akaning'ata mkono wangu wa kulia, lakini na mimi nikamkamata na kumnyofoa kichwa. Ndoto namba 2 ni kuhusu KUPAA. Katika kupaa kwangu ilikuwa ninakaza mwili na mdogomdogo naanza kuelea hewani si juu sana. Lakini katika kupaa, MBAVU zilikuwa zinaniuma kadri muda ulivyosogea.
 
Hizo ndoto ulizoziweka hapo Kuna ndoto nzr na mbaya.
Ndoto nzr ni ,
-kupaa au kuruka.
-kuota umempiga mtu ujuwe umeshinda uchawi.
Ndoto mbaya ni hizo za Kula usingizini ,
-kung'atwa na mnyama au mdudu.
-kuota unapigwa na mtu au unapigana na mtu na kuumizwa vibaya sn.
-Kuota unachapwa viboko.
 
Mara nyingi sana naota nakula usingizini tena vinono vinono tuu,inakuaje hapo mkuu?
 
Back
Top Bottom