Hizi ndoto zitakuwa na maana gani?

kiss ov love

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2025
Posts
9,388
Reaction score
16,188
Wakuu twende kwenye point πŸ‘‰ iko hivi mara nyingi mimi huwa naota nipo shule yaani O-level, unakuta hata shule tuliyopo no ya Msingi lakini wanafunzi tuliyopo hapo ni wale niliyosoma nao sekondari na hii hutokea mara nyingi tu hata muda mwingine shule inaweza kuwa tofauti, lakini watu niliosoma nao Sekondari ndiyo hao nakuwa nao kwenye ndoto.

Ndoto nyingine ni ya kutumbukia kwenye shimo refu, japo baadae huwa wanatokea watu wananitoa.

Ndoto nyingine ya kukimbizwa, huwa nakimbizwa sana lakini sikamatwi.

Naombeni maana ya hizi ndoto wakuu najua JF hamshindwi kitu.
 
Mshana Jr
 
Soma hapa
 
Maisha Yetu Yana Drama Mnoo,,,Na Sisi Tuishio Ndani Ya Hayo Maisha Ni Dreamers Kwa Hiyo Ni Lazima Dreams Ziwepo Tu,,,Shaka Ondoa Ewe Binti Sayuni Uwe Na Kwaresma Njema.
Barikiwa mtumishi πŸ˜ŠπŸ™
 
Pachaa kama bado unaenjoy kwenye maisha yako basi una roho ya paka.
Kwa kifupi ni wewe mwenyewe (roho yako) unajikumbusha kubadili lifestyle yako sababu usipobadili baadhi ya vitu kwenye maisha yako utaelekea pabaya.

Kuota ukiwa shule ambayo ulishaivuka= maisha ya mazoea ambayo hayatakufikisha mbali utajikuta unarudia maisha fulani ambayo hayana mabadiliko ya kusonga mbele bali kurudi nyuma au kusimama pale pale

Kutumbukia shimoni alafu baadae unaokolewa na watu= japo maisha yako yamesimama pasina mabadiliko au umerudi nyuma katika malengo yako, bado ungali na watu wa kukushika mkono kukurudisha relini mara kwa mara.

Unakimbizwa na watu lakini hukamatwi= misukosuko na mapito unayopitia yanaletwa na wabaya wako lakini hawatoweza kukuzima kabisa bali watashindwa mwisho utaibuka mshindi 😁

1. Pambana hadi huko ndotoni uvuke hiyo primary

2. Pambana hadi ndotoni ukiona shimo upae badala ya kudumbukia

3. Pambana hadi wanaokukimbiza uwageukie uwakimbize wewe hapo utakua umeshinda ulimwengu zote za roho na kimwili.

Kila la heri japo sijaandika haya maelezo nimetumiwa na babu yangu nikutumie πŸ˜€πŸ˜€
 
Aisee pole sana mkuu,
Ndoto ya kuota unarud shuleni ama unafanya mtihan na haumalizi au unakuwa stressed au unakutana na watu wa nyuma

sio nzuri, Hongera kwa kuwa na mind inayokukumbusha kuwa maisha yako hayako sawa

Kuota unadumbukia shimoni watu wanakutoa au haufiki chini ni Mind yako inakuamsha kutoka katika hali ambayo inaweza kuathiri mwili wako physically Mfano..Mapigo ya moyo yakiwa chini sana ubongo hukuwekea hiyo ndoto kukuamsha, hata hewa ikianza kukata ubongo hukuamsha kupitia ndoto
 
Haya maelezo yamenyooka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…