Hizi ndoto zitakuwa na maana gani?

Hizi ndoto zitakuwa na maana gani?

Pachaa kama bado unaenjoy kwenye maisha yako basi una roho ya paka.
Kwa kifupi ni wewe mwenyewe (roho yako) unajikumbusha kubadili lifestyle yako sababu usipobadili baadhi ya vitu kwenye maisha yako utaelekea pabaya.
Kuota ukiwa shule ambayo ulishaivuka= maisha ya mazoea ambayo hayatakufikisha mbali utajikuta unarudia maisha fulani ambayo hayana mabadiliko ya kusonga mbele bali kurudi nyuma au kusimama pale pale
Kutumbukia shimoni alafu baadae unaokolewa na watu= japo maisha yako yamesimama pasina mabadiliko au umerudi nyuma katika malengo yako, bado ungali na watu wa kukushika mkono kukurudisha relini mara kwa mara.
Unakimbizwa na watu lakini hukamatwi= misukosuko na mapito unayopitia yanaletwa na wabaya wako lakini hawatoweza kukuzima kabisa bali watashindwa mwisho utaibuka mshindi 😁

1. Pambana hadi huko ndotoni uvuke hiyo primary

2. Pambana hadi ndotoni ukiona shimo upae badala ya kudumbukia

3. Pambana hadi wanaokukimbiza uwageukie uwakimbize wewe hapo utakua umeshinda ulimwengu zote za roho na kimwili.

Kila la heri japo sijaandika haya maelezo nimetumiwa na babu yangu nikutumie 😀😀
Asante mkuu nitabadili life style yangu
 
Aisee pole sana mkuu,
Ndoto ya kuota unarud shuleni ama unafanya mtihan na haumalizi au unakuwa stressed au unakutana na watu wa nyuma

sio nzuri, Hongera kwa kuwa na mind inayokukumbusha kuwa maisha yako hayako sawa

Kuota unadumbukia shimoni watu wanakutoa au haufiki chini ni Mind yako inakuamsha kutoka katika hali ambayo inaweza kuathiri mwili wako physically Mfano..Mapigo ya moyo yakiwa chini sana ubongo hukuwekea hiyo ndoto kukuamsha, hata hewa ikianza kukata ubongo hukuamsha kupitia ndoto
Asante mkuu nimekupata vyema
 
Wakuu twende kwenye point 👉 iko hivi mara nyingi mimi huwa naota nipo shule yaani O-level, unakuta hata shule tuliyopo no ya Msingi lakini wanafunzi tuliyopo hapo ni wale niliyosoma nao sekondari na hii hutokea mara nyingi tu hata muda mwingine shule inaweza kuwa tofauti, lakini watu niliosoma nao Sekondari ndiyo hao nakuwa nao kwenye ndoto.

Ndoto nyingine ni ya kutumbukia kwenye shimo refu, japo baadae huwa wanatokea watu wananitoa.

Ndoto nyingine ya kukimbizwa, huwa nakimbizwa sana lakini sikamatwi.

Naombeni maana ya hizi ndoto wakuu najua JF hamshindwi kitu.
Unarudia makosa ya nyuma yanayokwamisha maisha yako au umeshindwa kujifunza. (Cha muhimu ni wewe unajiskiaje ukiwa shule ya msingi, unafurahi, unoaona aibu, unajuta, unajikuta unashindwa mtihani, unaonewa, etc)
 
Pit = death, failure, poverty.
Kukimbizwa= Death, spirit boundage & chains.
Solution: Jazwa Roho Mtakatifu.
Maombi utafunguliwa kwa muda tu vifungo bado vitakuandama na mwisho wa siku utaota unatumbukia mazima ndio basi tena umauti utakukuta
 
Unarudia makosa ya nyuma yanayokwamisha maisha yako au umeshindwa kujifunza. (Cha muhimu ni wewe unajiskiaje ukiwa shule ya msingi, unafurahi, unoaona aibu, unajuta, unajikuta unashindwa mtihani, unaonewa, etc)
Hapo ndotoni tunakuwa tu kawaida tunasoma au tunaendelea na mambo mengine
 
Mbona unanitisha mkuu
Mimi sikutishi nakuambia ukweli.
Sitafsiri ndoto kwa minajiri ya kukopi kwenye google au kwenye vitabu vya matapeli waliopigwa na maisha.
I tell you truth from my experience.
Hizo ndoto zote ulizoota nimeshawahi kuota, najua impacts zake. Pia natafsiri kulingana na Neno la Mungu.
Ila nimekupa solution moja nzuri sana.
Kajazwe Roho wa Mungu utanishukuru.
Shetani haogopi maombi, shetani haogopi ibada , shetani anaogopa Roho wa Mungu anayekaa ndani ya mtu
 
mwisho wa siku utaota unatumbukia mazima ndio basi tena umauti utakukuta
Kwa uzoefu wangu ukitumbukia mazima kufa hufi ila cha moto utakiona huku duniani
Au uote unakimbizwa na mnyama mkali akushike akukule hadi ufe, huku duniani hufi utakuwepo ila kwa msala utakaopitia utatamani ufe kwelikweli lakini hufi hata kwa kulazimisha.
Ndoto nyingine mbaya uote unapanda ngazi alafu ghafla badala ya kupanda ujikute unashuka automatic pasipo wewe kutaka
Pia kuna ndoto nyingine mbaya niliyoiona ambayo unakuta mtu anashindwa kupanda kimlima au kimuinuko kidogo tu ambacho huku duniani unaweza kukipanda kawaida! Ukiota hii ndoto jaribu kuwahi kwa wazee au pale ulipoweka imani yako upaelekee kwa nguvu zako zote

Mtumishi karibu na huku utupe neno Setfree
 
Back
Top Bottom