1.Wanaotuombea mabaya ni wengi mno bila sisi wenyewe kujua.
2. Huwa nawaambia watu pesa Ina kawaida ya kuongea yenyewe Ina lugha yake,haihitaji msemaji Wala mwakilishi[emoji1][emoji1][emoji1].
Lugha rahisi angalia watoto wa kishua mionekano yao,utanielewa.
3. nilipokuwa mdogo nilikuwa nawaza nikifikisha miaka 40 najiua ili nife nikiwa HB, Saiv nmeongeza kwenye 70 au 80
4. Mwanamke ni kiumbe kinachokua haraka na kupoteza mvuto haraka kama jua la asubuhi linavyopendeza ila likifika saa nne tu unalichukia kabisaaa
5. Kuna mzee mmoja aliwahi niambia, hata ukiwa unafanya kazi ya kuzoa taka, basi ifanye smartly and integritly, utakuwa wa kipekee na watakuita mchawi kwa wateja utakaopata.
Wewe jamaa umeifanya kazi yako kwa misingi hiyo.
Huwezi fanya kazi ya usafirishaji unakunywa mapombe hovyo hovyo muda wote, ukiongea unanuka pombe sigara, uko mchafumchafu, hujali muda, huna lugha nzuri, hujui kumsoma mteja, hujui kudhibiti hasira zako, kwenye gari unapiga makaswida au makwaya tu, uko na mteja unaongeaongea na simu, hauna focus na attention kwa mteja uliyenaye kwenye gari, unaangalia angalia wanawake hovyo, unakosoasoa maoni ya abiria wako, unatangaza njaa zako, unalialia na kulalamikia matatizo yako kwa wateja, huna ufahamu wa mambo kichwani, mteja anaanzisha kila mada uko mweupe, Unaongea habari za wateja wengine kwa mteja uliyenaye, unaongea bila brake, gari yako mbovu mbovu, wese vibaba, fine hulipi, trafic wanakusumbua, huwezi toboa biashara ya abiria.