Hizi ni dalili kwamba mwanamke wako anatoka nje ya mahusiano, kuwa mwangalifu

Hizi ni dalili kwamba mwanamke wako anatoka nje ya mahusiano, kuwa mwangalifu

Wataalamu wa maswala ya mahusiano wanaamini kwamba, mwanamke anapotoka nje ya ndoa yake, inakuwa rahisi sana kubainika au kufumaniwa kuliko ilivyo kwa mwanaume.

Hii inatokana na ukweli kwamba, hisia zinakuwa na nafasi kubwa sana kwa mwanamke, kwani mwanamke huishi kwa hisia zaidi kuliko mwanaume. Bado nasisitiza kwamba, haipaswi na siyo sahihi mtu kuchukulia dalili hizi kama ushahidi wa mpenzi wake kutoka nje ya ndoa. Uchunguzi wa kina kufuatia dalili hizi ni muhimu sana.

Zifuatazo hapa chini ni baadhi ya dalili zinazoweza kuonyeshwa na mwanamke ambaye anatoka au yupo kwenye harakati za kutoka nje ya ndoa yake:

1.KUCHELEWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuaga kwamba anakwenda saluni au kusuka, badala ya kurejea kwa muda ambao umezoeleka, anachukua muda mrefu hata mara tatu zaidi. kuna wakati kwenda sokoni huchukua saa kadhaa bila kujali soko liko umbali gani. Kama ni mara moja sawa, lakini ikishakuwa zaidi ya mara moja huenda kuna tatizo la kukosa uaminifu.

2.KUBADILI MAENEO: Hebu chukulia kwamba, mwanamke amezoea kwenda soko fulani la karibu, hospitali fulani ya karibu, saluni fulani ya karibu na hata nyumba fulani ya ibada ya karibu. Unapoona anahama maeneo ya karibu ya huduma na kwenda ya mbali, bila sababu ya msingi, huna budi kuanza kutuhumu mwenendo mbaya.

Siyo lazima kuhama kokote kuwe na mwenendo mbaya, lakini kama kuhama kwenyewe kunatia shaka kwa sababu maelezo ya kuhama huko hayana msingi, mwanaume ana kila sababu ya kuchunguza kama hakuna usaliti unao anywa.

3.UNUNUZI USIO WA KAWAIDA: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa ajili ya kupata fedha, basi atakuwa na mabadiliko makubwa katika mtindo wake wa manunuzi.
Atakuwa ananunua vitu vya thamani kubwa kuliko uwezo wake, atakuwa na fedha nyingi tofauti na ambazo angekuwa nazo na pengine kumiliki mali kama nyumba kwa siri.

4.KUANZISHA VURUGU: Kuna wakati mwanamke anayetoka nje ya ndoa huanzisha vurugu za makusudi na mumewe. Lengo la kuanzisha vurugu hizo ni ili apate nafasi ya kujifanya amezira na kuondoka nyumbani kwa muda.

Huo muda anapoondoka nyumbani kujifanya kakerwa na vurugu hizo ndiyo muda ambao anautumia kwenda kwa hawara yake.

5.KUSITISHA UAMINIFU: Mwanamke anayetoka nje ya ndoa, mara nyingi husimamisha kumwamini mumewe, yaani hayuko tayari kushiriki masuala ya siri, ambayo wanandoa huwa wanashiriki.

Husita kumshirikisha mumewe kwenye mambo yake mengi. Lakini pia husita kumuomba mumewe ushauri, kama alivyokuwa akifanya siku za nyuma.

6.KUACHA KUVAA PETE: Kuna sababu nyingi ni kwa nini mwanamke anaweza kuacha kuvaa pete yake ya ndoa. Moja ya sababu hizo ni kusalitiwa na mumewe au ndoa yake kuwa kwenye misukosuko mikubwa sana.
Lakini nje ya misukosuko mikubwa ya ndoa, sababu nyingine inayoweza kumpelekea mwanamke kuvua mara kwa mara au moja kwa moja pete yake ya ndoa, ni kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake.

7.KUONESHA WASIWASI: Kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake , ni lazima atakuwa na wasiwasi na mashaka yasiyo na sababu mbele ya mume wake.

Anaweza kuonesha kutotulia kwa aina fulani kana kwamba, anahofia kuna siri itatoka au kuna kitu ambacho tayari mume wake anakijua dhidi yake. Mara nyingi wasiwasi na mashaka humtawala sana mwanamke anayetoka nje , hasa katika hatua zake za awali za kutoka nje.

8.KUZUNGUMZIA KUACHWA: Kuna wakati mwanamke anaweza kuwa anatoa kauli za kuonesha kwamba, kama mwanaume anaona vipi , wanaweza kuachana.

Kama kila penye ugomvi kidogo tu mwanamke anakimbilia kusema, “kama ni kuachana, tuachane tu” hiyo inaweza kuwa ni dalili mbaya kwa mwanamke anayetoka nje ya ndoa kwa sababu hana tena upendo na mumewe. Mia

Chanzo: Blogs
Na mwanaume je?
 
in general ratiba yake hua inabadilika na care ile kwako inapotea hata hisia zake kwako zinapotea thats why tunasema Women wengi hawawezi kutofautisha love and sex kama wanaume,wao walikofanya sex na akili yao inapeperukia huko huko
 
kinachofuata cm itaachwa ofcn....!!!!

Nop! Itategemea ni aina gani ya mwanaume uliyenaye....1) Kama mumeo ni aina ya mwanamuziki DUDUBAYA....mwendo ni ngumi jiwe no story, ikifika half time ww mweny simu unabaki na sura ya kitimoto(tena usiombe awe ni jamii ya Lorya/Tarime/Chaga original. 2)Kama mumeo ni aina Mchunga kondoo wa Mungu...ataenda kwenye maombi na maombezi,awaambie watumishi wakukalishe kikao waone kama una pepo. 3) Kama mumeo ni aina ya mwanadiplomasia/mwanasaikolojia atakupotezea, halafu anaanza kuishi life mfano wa bachelor, anakuwa na mawasiliano mema na watu wengne wote ila si ww, anakuwa mcheshi kwa wengne na si kwako, hatajali lolote kuhusu wew...lakn anakuchek unafany nn zaidi. Akiona hustuki wala hulalamiki...anaezeka kibanda kwa nyumba ndogo....anajiachia huko. Wew utabaki kuwa mlinzi wa nyumba na watoto. Wakati huo hana mapenzi na wew kwa kuwa umeiondoa imani yake kwako kwa kumzuia kuichunguza cm yako....ujue bado wew ni mke wake japo mnaishi kama visiki...ila anakutafutia sababu. Kwa kuona yeye anaishi kwa uhuru...na anachelewa kurudi/ harudi na hajali wew na familia yake...lazma utaanza mashtaka ama na wew utaamua uishi huru kama yeye kupunguza stress(maana lazma uchanganyikiwe). KOSA LAKO MOJA TU, LENYE NGUVU ATAKALOLIONA....ATALIPIGIA MSTARI...safari ni mahakamani kuvunja ndoa. Mwenzako alishajiandaa baada ya kuiona jeuri yako. Lakn wew ulizubaa ...ukaendeleza ushindani na aliyeshinda tayari. MATOKEO YAKE UNAPIGWA CHINI PASIPO KUTARAJIA.....AFU UNAANGUA MAYOWE WALIMWENGU WAKUSAIDIE....Mwenzio anakula bata...hana hata chembe ya wasiwasi. USHAKUWA BW*EGE. Kisa kidogo sana kwa mwanaume...cha wew mke kusimamia kucha kuonesha ujeuri na ukamwachia swali lisilo na jibu...mume makini hukuna kichwa na kujifikirisha ili apate jibu...ni kwanini upo hivi.

JEURI YA MKE KWA MUME ikiwa ni sehemu ya ukorofi...hainaga matokeo mema kwa mke ikiwa mumewe ni mtu smart(akilini na maishani). ILA KAMA MUME NI BWE*GE...aaah mbona utamuendeshaaa! Muhimu uwe na sura mwanana, una inye(wengi wanapenda), umekwenda hewani sekunde, mtanashati na una kamshahara...aaaaah we fanya utakavyo...mume ukirudi utamkuta hom anawaza mbunye tuuu. Yaani utamuongoza tuu, ukimwambia mm sitaki ivi..anatii tu. KAMA WEW MWANAMKE HUTAKI KUISHI VILE MUMEO ANATAKA.....BASI MTAFUTE MUME ANAYEDATA NA shepu na maumbile yako na kamshahara, kila utakachosema ama kufanya yey atasema "ndiyo". Hata ushauri hanaga(bwe*ge).

KUPANGA NI KUCHAGUA...CHAGUA MAISHA UNAYOTAKA KUISHI. Alimuradi uyaelewe hayo maisha unayo ishi. MBONA SIMPO TU JAMANII, EEEH!!!!
 
safi sana so smart nimeipenda!!!!
 
athanteeeeeeee

WEWE UNAMPENDA YUPI WW KATI YA HAWA...:-
1)Dudu baya(kichapo cha papo kwa papo ukimuonesha jeuri).
2)Mchunga kondoo wa Mungu(anayekwenda kwenye maombi/akubembeleze mwende church mkaombewe)
3)Mwanadiplomasi/mwanasaikolojia(yey hakudundi wala haendi kuombewa...anaicheck response yako, kama unajisahihisha ama unasimamia ulichosimamia).
4)Mume bwe*ge (ambaye amezuzuka na sura na shepu na mshahara wako, anawaza mbunye tu, lolote utakalo sema au kufanya kwake ni "ndiyo" tu. Yaan limbukeni wa mapenz kwako).

NI YUPI WEWE AKUFAAYE KATI YA HAWA WANNE???
 
Why....ikiwa mm na yeye ni mwili mmoja! Na kama nina mashaka na yaliyomo kwa cm yake??? UTANIZUIA NISIICHUNGUZE CM YAKO???
Unaju nn kitafuata.....!!!
Mwili mmoja ni imani yako ndo inasema,,,, mbona kila mmoja ana moyo wake......hayo mashaka yako yataakuua mapema mno,,, usitafute stress bro......fanya tafiti zako kimya kimya.... ukiigusa unaweza fanya kitu usichotarajia,,,,hao wewe waangalieeeee....endelea na maisha...
 
WEWE UNAMPENDA YUPI WW KATI YA HAWA...:-
1)Dudu baya(kichapo cha papo kwa papo ukimuonesha jeuri).
2)Mchunga kondoo wa Mungu(anayekwenda kwenye maombi/akubembeleze mwende church mkaombewe)
3)Mwanadiplomasi/mwanasaikolojia(yey hakudundi wala haendi kuombewa...anaicheck response yako, kama unajisahihisha ama unasimamia ulichosimamia).
4)Mume bwe*ge (ambaye amezuzuka na sura na shepu na mshahara wako, anawaza mbunye tu, lolote utakalo sema au kufanya kwake ni "ndiyo" tu. Yaan limbukeni wa mapenz kwako).

NI YUPI WEWE AKUFAAYE KATI YA HAWA WANNE???

namba 3...!!!!
coz hata mimi ndo akili yangu..!!! ukinuna utanikuta na kunitafuta mwenyewe!!!! ukiwa busy mara cku 2 mi nakuongeza 28
 
Mwili mmoja ni imani yako ndo inasema,,,, mbona kila mmoja ana moyo wake......hayo mashaka yako yataakuua mapema mno,,, usitafute stress bro......fanya tafiti zako kimya kimya.... ukiigusa unaweza fanya kitu usichotarajia,,,,hao wewe waangalieeeee....endelea na maisha...

"fanya tafiti kimya kimya", za nin tafiti ikiwa unaogopa kufa mapema???

Uwoga umasikini...binadamu tumeumbwa na tabia kupenda kujua yaliyomo nyuma ya pazia. Na kama ukihisi mahali pale kwenye eneo langu pana hatari / kitu kibaya...Kama umeweza tu kuhisi...basi una akili timamu na sensory nerve zako zinafanya kazi.

KAMA UNAJALI USALAMA WAKO....NI LAZIMA UCHUNGUZE ENEO LAKO NA UJIRIDHISHE JUU YA HISIA ZAKO KWAMBA KUNA HATARI.

Ni kwambaaa, usimchunguze mke...ishi nae kwa ananiiii...ila ukihisi hitaji la kufanya hivo, tena kwa kustukiza...siyo dhambi. Usifanye kwa kushawishiwa na mtu...fanya kwa msukumo wa nafsi yako. ILI KUREJESHA AMANI YA MOYO WAKO ILIYOPOTEA. Ni lazma uwe na uamuzi...hata ukiamua mkeo aishi atakavyo na wew hutamchunguza...pia ni sawa...coz ndiyo amani ya moyo wako. SEMA NA MOYO WAKO...syo kesi!!!
 
namba 3...!!!!
coz hata mimi ndo akili yangu..!!! ukinuna utanikuta na kunitafuta mwenyewe!!!! ukiwa busy mara cku 2 mi nakuongeza 28

Yap! Xafi..lkn samahani mkuu, halleluya moshi, wewe ni "KE" na kama ni single lady...na kama ni mwenyej wa K, Njaro. Nijibu tu yote matatu. Sio shida coz hapa vinaongea vivuli...ila mawazo ni ya mutu. Nipe jibu ili km vp turefushe story kidogo.
 
Jamaa yangu alimsevu mchepuko "Mwenyekiti voda" simu moja akasahau sim mwenyekiti voda ikaita shemeji si akapokea aisee ilikua kizaazaa.mchepuko syo dili baki njia kuu.
 
Back
Top Bottom