Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Ipo Njia ya Mkato, Unatokea Mwanza, Nzega, Tabora, Ipole, Chunya, Mbeya. Masaa 8 unaiona Mwanza kama gari iko poa.
We jamaa ni Muongo kweli!
Yaani utoke Mbeya hadi Mwanza kwa Massa 8 tu? Labda unazungumzia Mbeya to Tabora ndiyo Massa 8 kwa private car.
Japo kutoka Mwanza - Mbeya via Tabora inaonekana ni short cut, lakini umbali wake si mchezo.
 
Mbeya-Chunya walishatandaza lami..sijajua huko kwingine.

Ila kona haziepukiki[emoji1787]hizo za Chunya ni bora akapita tu hizo za Mtera.
Lami saiv imefika mpaka Makongolosi. Next ni kutoka Makongolosi hadi Rungwa, kisha itaunganishwa na sehemu ya Ipole, kwa upande wa Tabora.
 
Ile njia ni ya kifala sana. As if hayo makona hayatoshi, mwanzoni ilikua ukimaliza izo kona tu kwa mbele kidogo kuna mto mpana nadhani unaingiza maji lake manyara na palikua hamna daraja! Kwahiyo mnapiga mbizi na magari yenu mnaibukia upande wa pili.

Kuna siku nimepambana na makona yangu mpaka nimefika pale mtoni mbupu zote zimevimba, kichwa kinauma, mgongo haufai.. lahaulaa! kumbe kuna mamvua yamenyesha milimani huko mto umefurika balaa haupitiki na imeshabebwa coaster pale! Ikabidi nigeuze aisee nikaanza kupanda tena yale mamilima kwakweli nililaani sana iyo siku. Nimekuja kufika arusha saa 9 usiku.

View attachment 1765582
Duuuh pole sana, hii ilinikuta
 
Umewahi kupitia Ziwa Natron kwenda Loliondo?
Kuna kona 17 tishio
zile hata anayesema nyankoro ni kali hana lolote zile ni kona



kona ya mwanga ugweno haina wapitaji sana lakini ni kona kali kuliko zote yaani ni funga kazi mkuu afu haziishi sasa bora iyo nyankoro, nyankoro inatisha kutokana na zile landscape zake na misitu minene.
 
Kona za mlima Ndololo, Mlima nyani njia ya Ifakara-Mahenge. Kona za kuitafuta Mkamba/Sanje na Soni ukitoka Mikumi kwenda Ifakara.
Hata kutokea Mikumi kwenda Kilombero kuna kona nyingi na vidaraja vyembamba 18
 
Iringa - Dodoma
Mbeya - Kyela kuna sehemu wanapaita uwanja wa ndege
Nilihama shule kwa sababu ya kona za uwanja wa ndege

Iringa - Morogoro
Kitonga
Na pale ukitoka Mikumi sijui wanapaitaje

Same - Chome
Hedaru - Mamba vunta
Mwanga- Usangi

Moshi - Marangu - Tarakea
Mambo - Lushoto

Morogoro MJINI - Mgeta
Mvomero - Muscat mbele ya kibati

Njombe - Ludewa
Njombe - Makete

Ila nilipoogopa zaidi ni Iringa - Dodoma na Basi liitwalo Kimotco la Arusha
 
We jamaa ni Muongo kweli!
Yaani utoke Mbeya hadi Mwanza kwa Massa 8 tu? Labda unazungumzia Mbeya to Tabora ndiyo Massa 8 kwa private car.
Japo kutoka Mwanza - Mbeya via Tabora inaonekana ni short cut, lakini umbali wake si mchezo.
Wewe hujui usemalo, Unaijua V8 wewe! "in Pole Pole Voice" Mbeya Mwanza Masaa 8 unaona haiwezekani! Any way Kichwa kikubwa kimejaaa Maji badala ya Ubongo. Let me stay cool
 
Wewe hujui usemalo, Unaijua V8 wewe! "in Pole Pole Voice" Mbeya Mwanza Masaa 8 unaona haiwezekani! Any way Kichwa kikubwa kimejaaa Maji badala ya Ubongo. Let me stay cool
Acha utoto wewe. Kwani kakwambia yeye ana V8? Au kila mmoja ana V8?
Na isitoshe hujawai pita bara bara hiyo ya Tabora ndiyo maana una bwabwaja tu.
 
Back
Top Bottom