Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

kona ya kutoka sebuleni kuingia chumbani kwangu hii kona noma sana hua inavunja sana meno nikirudi home niko mitungi lazma niangushe gari.
 
Ungekuwa mwanaume ningejua unabaki unaminya bleki za.........

Habari za asubuhi mkuu
 
UKIWA UNATOKA MAMSERA KAMA UNAKUJA ROMBO TARAKEA KUNA KONA HATARI SANA JAPO NI SALAMA.

MÊmENtO HoMO
Kuna siku nilipanda noah kutokea mkuu kwenda tarakea nikawa najisikia vibaya sana na kutapika juu. Later nikaja ambiwa ni spidi ya dereva na zile kona probably nilipata kizunguzungu. Hata unipe nini kule sithubutu kuendesha. Na mafuso yanavyotembea kule kama vile hamna kitu
 
usichanganye mbuzi,kuku,kondoo group moja kisa wote ni wanyama kumbuka kuku ni ndege.Hapa na manisha jadili mada husiki wewe unaingiza mengine porojo za kahawa hatuhitaji kuzijua hiyo ni personal issue
 
Wazo zuri na mimi nimefikiria hivyo. Binafsi hizi kona zinazotajwa hapa natamani nizitembelee nione mandhari ya nchi ya uchumi wa kati yalivyopambika
Kama ni muoga na unatumia usafiri wa bus usikae siti ya mbele maana ni hatari hususani unaposhuka kuja mbeya mjini.Kwa private Car sawa..

Hizo kona ni sawa na za kushuka Ziwa Rukwa kutokea Sumbawanga ,kuna njia 3 zote zina kona kali
 
Sema TZ hakuna barabara yenye kona mbaya. Tembeeni huko duniani muone maajabu. Last Year i was in Mumbay tukapanga tukatembelee safu ya milima ya Himalaya, mwenyeji wetu Mr Ramesh akatushauri tufanye safari ya kwenda kimji kidogo kiitwacho Mandahli (si mdogo kihivyo ila kwa kule ni mdogo)then tufike sehemu inaitwa Kinnaur and we took a Car instead of a Train which seems to be as cheaper than Car. Kwa Gari mnalipa 1700 Rupee sijui hapa Bongo ni kiasi gani wakati ukitumia Train ni around 900 Rupee. Tuliamua kutumia Gari kwa kuwa mwenyeji alituambia mtaona safu ya hiyo milima kwa uwazi lakn tunapaswa kuwa majasiri wa kiwango kikubwa mno maana ile barabara nadhani inaweza kuwa moja kati ya barabara za kifo zaidi duniani. Safari yetu ilianza mapema saa moja kwa saa za Mumbai (BOMBAY) kuelekea huko ambako ni magharibi ya India na ni mpakani kwa nchi PAKISTANI, CHINA na yenyewe INDIA, huko ndiko hupatikana jimbo maafuru la KASHAMIR ambalo lina mgogoro kati ya INDIA na PAKISTAN na ikumbukwe zamani hizi nchi ilikuwa nchi moja tu. Basi mzigo ukaamshwa na Gari moja matata sana huku sijawahi ona aina hiyo ya gari (MASERATI) aisee asikwambie mtu watu wanateseka kwenye hii dunia acha utani. Hiyo barabara unayopita kwanza nyembamba na mostly haina lami, na ni safari ya siku 2 hivi maana huwazi tembea usiku ile njia wallah. Mnatembea juu ambako chini kuna mto au korongo la urefu wa mita 150 na mkitumbukia huko hakuna atakuja kukutoeni. Muendako mnapaswa kubeba chakula kwa wingi maana hujui kitatukia nn, vyakula vya kihindi michosho kinyama, hawali ng'ombe nk, mi binafsi nilibeba maharage ya kopo, crips, Biskuti nyeupi zinakuwa na chumvi, maziwa na juice. Njiani mnaweza kuta migahawa ile local na sehemu chache vijiji ambako hutoa huduma ya kulala na pancha. Safari yetu ilituchuka siku 3 badala ya 2, mbaya kuna Baridi kali sana kwenye ile safu ya milima na barafu tupu juu huko. Hakuna chance yoyote kwa dereva kufanya makosa yoyote yale, kwanza hakuna vibao vya kuonesha mteremko mkali, au kona ni mwendo wa uzoefu wa dereva tu. Kwa jinsi nilivyokuwa nashikilia gari mungu ndio anajua. Itoshe kusema tembeeni duniani mjionee jinsi madereva walivyo na skills na niseme hapa wazi HAKUNA DEREVA WA TZ ATAENDESHA KWA ILE ROAD.
Next trip mungu akijaalia safari ya Argentina au Peru tutamuomba mwenyeji wetu atutembeze kwenye safu ya milima ya Andes kwa gari ili tujifunze zaidi. Ila pia nasikia CHINA kuna deadly roads sema kwakuwa wako more advanced kwenye technology ndio inapunguza ukali.
TZ hatuna hata barabara inayotisha sema tuna poor technology. Lkn huko India hata namna ya kuweka miundombinu ni mtihani sana.
Kurudi tulirudi kwa Ndege ambayo ni kama rupee 2200 hivi.
Ile barabara hata usisearch kwa Youtube mtajionea ni kama hadithi ila ni kweli kabisa. Wale wahindu wanateseka bhana waacheni waje huku wawe vibarua kwa Mo
 
Kona ya wabinuka(Wahaya watanisaidia) ukitokea Omurusha kule Karagwe kupitia Kyerwa kuelekea Murongo mpakani na Uganda, Nanyamba kule Mtwara
 
Kona hatari ni kona za kutoka Mbeya kwenda Chunya. Kona nyingine inaitwa Gangi tololi, kutoka Njombe kwenda Ludewa.
Pia kama unatoka Njombe kwenda Makete, barabara ina kona za hatari na milima kama unatafuta kuifikia Ikonda Hospital
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…