Hizi ni kona kali na milima, kwa barabara nchini, taja nyingine

Mombo-Soni-Lushoto,
Mara ya kwanza unaweza usema huku sirudi tena.View attachment 1764642
Hii naona nafuu kidogo ni lami, kuna balaa njia ya Lushoto kwenda Mlola au uingie vijiji vya Lushoto kuna milima imesimama hatari. Niliwahi kwenda na bike kuna milima mpaka unaogopa ila wenyeji wanashuka na pikipiki za kichina na mzigo bila hofu.
 
Hii naona nafuu kidogo ni lami, kuna balaa njia ya Lushoto kwenda Mlola au uingie vijiji vya Lushoto kuna molina imesimama hatari. Niliwahi kwenda na bike kuna milima mpaka unaogopa ila wenyeji wanashuka na pikipiki za kichina na mzigo bila hofu.
Huko mzee ni hatari,
kuna jamaa yangu hio siku tunapeleka msiba ndio mara yetu ya kwanza, basi kakaa mbele kabisa,

Kila gari ikizunguka kona anaona jiwe hili hapa usoni, upande wa kushoto ndio hasubutu kugeuka maana ni bonge ya Korongo.

Akamwambia dereva "Sasa mbona kila saa unasukumizia gari upande wangu?

Baadae dereva akawa anabana chini,

Akaanza kusema tena...

"Dereva angalia tairi hio utatuangusha tufe".

Ilibidi akae kwenye korido sasa,

Tunafika msibani nako baridi ikamzidi akaona watu wamelala asijiingize kati, baadae kuja kushtuka kumbe kalala katikati ya Wamama wawatu, akatolewa mbio akaenda kujificha kwenye migomba, Baadae anatafuta chumba akajichanganya akaingia chumba chenye jeneza,

Alikua kituko cha mwaka.
 
Kona za Lushoto Mombo
 
Mi kona za kitonga aah sijawahi kuzioea kabisa, hasa nikiwa natoka Iringa to Moro (kushuka) huwa nahisi moyo unahama mahali pake huku maini kama yanatoka hivi, aah na madereva sijui ndiyo wamezoea hiyo speed yake sasa🤔 huwa nabaki nasali tu na kuminya breki za miguu😀
 
Ni tamu kweli kweli, napenda kukaa siti za mbele ingawa naogopa risk yake.

Vipi Sekenke, milima ya Usambara kuelekea Lushoto..
 
No 4 hapo huwa zinafahamika pia kwa jina la Nyang'oro ni noma sana hapo kuna madereva wa mabas huwa wanapita hapo kama hawana akir vizur..
Kuna siku nilipita hapo na KIMOTCO, dereva alikuwa noma sana, speed plus hizo kona, nikabaki kushangaa tu.

Aliomba assist ya overtake kwa dereva wa Lori akapewa na kupaa kileleni kama Bombardier
 
Hahahaaaa
 
Hizo kona zina raha yake ila ni balaa kwa upande wa pili.

Iheshimike kona ya Nyang'olo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…