Hahahaaaaa! Huyu jamaa kazidi kunitoka kiukweli.
Yaani hata sijui atanirudi kwa lipi!
Wewe utakua umelewa sio bure! Umeheshimu maamuzi yangu wapi?
Hayo matusi unayotukana ndio heshima?
Hata hivyo sioni haja ya kuendelea kulumbana hapa.
Kila mtu abaki na maamuzi yake na kuheshimu ya mwenzie.
Hakuna aliye kutukana umeambiwa ukweli chuki zako mitandaoni kwa dimond hazimpunguzii chochote kuwa mpole
Angemchukia huyu sawa
Mondi kaniangusha sana. KingKiba naona kama nafsi yang imeanza kumuelewa lkn dah kulamba matapishi jinsi nilivyokua namponda dah yan sijielewi mondi kanichanganya sana dah
Ngoja nibaki na Weusi tu arif
Hahahaaaaa, mkuu unaona taabu gani? Huu ni mwaka wa kufanya maamuzi magumu na sahihi.
Kama Lowassa aliweza kwenda chadema kutoka CCM alikodumu tokea mwaka 70 ijekuwa wewe?
#TorokaUje
Ngoja nianze kuweka imani kwa Kiba mana hawa wasanii wa Bongoflavor sio wakuwaamini nifah ckutegemea kama mondi atakuja kutulet down like ths"
Nakuambia mimi leo nilikua nimefunga tumbo kwa mkanda maana kama Kiba angekuwa kwenye ule mkutano leo ningetundikiwa dripu.
Niliwaza itakuwaje? Kiba huyu ninayemkubali aje awaunge mkono mafedhuli CCM? Kiukweli nimemshukuru Mungu sana.
Ila Kiba ana busara sana, fikiria hata haya mapicha picha hajaweka kabisa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Hahaha: ila kanifurahisha sana kijana wenu" inaonekana hanunuliki na anaheshimu fans wake" I hop mwenendo wake utakua huu huu adi mwisho..
Weeee, Ali Kiba ni arrogant sana.Hapelekeshwi, akiamua kaamua.
Hata mimi naomba Mungu hadi mwisho aishie hivihivi maana akibadilika atanitia aibu sana.
Hahahaaaaa! Huyu jamaa kazidi kunitoka kiukweli.
Yaani hata sijui atanirudi kwa lipi!