Hizi ni siasa za kilaghai zisizo na tija kwa taifa letu. Kugawa mitundi ya gesi badala ya kukomaa JNHP ikamilike ni ni kutaka kutafuta kiki zisizofaa

Hizi ni siasa za kilaghai zisizo na tija kwa taifa letu. Kugawa mitundi ya gesi badala ya kukomaa JNHP ikamilike ni ni kutaka kutafuta kiki zisizofaa

Unampa mwananchi mtungi wa gesi. Kesho kutwa hana hata pesa ya kujazia gasi huo mtungi ukiisha.

Kwa nini msikomae JNHP ikakamilika alafu umeme ukashuka bei na bidhaa kushuka bei na maisha mwananchi yakawa nafuu.

👇Huu ni ulaghai usiofaa. View attachment 2289171
mnaoponda Julius Nyerere Hydro electric power ,mna lack of information.Mradi unaendelea vizuri sana, nitaanza kuwatumia picha za maendeleo ya mradi.
 
Bwashee tangu lini wewe ukawa mtetezi wa JPM na ccm? Ndiyo maana watu wanasema nchi hii hatuna upinzani nyie wote ni wachumia tumbo tu. Unageuka ghafla hivi kuwa mtetezi wa ccm kisa januari kalaumiwa?! Lazima uwe na maslahi na hilo.
Wapi nimemsifia JPM Wala CCM? Mie Sipendi hii tabia ya wafuasi wa JPM kupinga Kila kitu Cha Samia sababu ya chuki ya kuondolewa madarakani.

Ndio maana nahoji kama mlikua mnashabikia JPM kuwasha umeme kwenye nyumba za Tembe kipi Cha ajabu watu wakipewa gesi vijijini?

Mie sijawahi ipenda CCM but sipendi zaidi unafiki wenu nyie Team JPM.
 
Mtungi wa kijani, rangi ya chama.
Kila kitu wanachofanya wanafikiria uchaguzi 2025 kuanzia kiongozi namba moja mpaka makada uchwara.....
Sijui watapata akili lini ya kutatua changamoto za maisha ya waTanzania badala ya kuwaza chaguzi...
 
WaTanzania mpunguze kulalamika, dunia nzima inaongelea nishati mbadala pia Ilani ya CCM na mpango wa taifa wa maendeleo wa miaka 5 (Ambayo ndio inamuongoza Rais na Mawaziri) inaongelea energy mix sio tu kwenye vyanzo vya umeme ila hata kwenye matumizi ya nishati majumbani.

Hivyo uwepo wa Hydro Power unatakiwa uende sambamba na nishati zingine kama Joto-Ardhi, Umeme wa upepo, Gesi n.k

So kama hamtaki gesi itumike waambieni wabunge wapinge utekelezaji wa mpango wa taifa otherwise mnaongea mambo msiyokua na uelewa nayo.
Mbona gas ya mtwara kwa miaka 6 ya mwendazake haijawahi kutajwa popote !!
Leo unazungumzia eti green energy ,
Ccm mtakomaa lini bendera fuata upepo ????
 
Mbona hayo TPDC walishaongea kwamba wanampango wa kusambaza gesi majumbani kwa subsidized price!!

Maboresho lazima yatakuja lakini kuanza kupinga mtu kuhamasisha matumizi ya gesi ni ajabu sana.

Hata umeme enzi hizo unaletwa mara ya kwanza ulikua na gharama, in fact tulianza na majenereta huko bush linawashwa saa 12 hadi saa 4 usiku!! Lakini taratibu mambo yamebadilika na bei sio Ile ya miaka ya 90?

So kuliko kupinga kabisa mshauri njia nzuri zaidi ndio mjadala unakua na tija. Nakumbuka siku JPM anawasha umeme kwenye nyumba ya tembe mlimshangilia sana kwamba kavunja rekodi ila sikusikia mkiongelea gharama za Luku za kila mwezi kwa wananchi maskini!!! So tuache unafiki na tutoe support Ile Ile kwa huyu
Luku Bei ya kikijini unaweza kununua hata buku ukatumia wiki nzima hiyo gas elfu 25 !!!!
 
Mbona gas ya mtwara kwa miaka 6 ya mwendazake haijawahi kutajwa popote !!
Leo unazungumzia eti green energy ,
Ccm mtakomaa lini bendera fuata upepo ????
Kasome mpango wa taifa wa miaka 5 from 2016 na sasa 2021..... Pia Ilani ya hiko chama kiliahidi hivyo. Team JPM waache kujifanya wajuaji wakati hayo anayofanya January ndio JPM aliahidi kwenye Ilani.

Mie sio CCM ila kuna tabia imezuka ya wafuasi wa JPM kujaribu ku undermine Kila kinachofanyika Ili tuu legacy ikumbukwe whilst JPM huyo huyo aliwahi washa taa kwenye nyumba ya tembe kupitia kina Kalemani..... Na huo unafiki ndio naopinga hapa.
 
Luku Bei ya kikijini unaweza kununua hata buku ukatumia wiki nzima hiyo gas elfu 25 !!!!
Kwani hujasikia January kasema gesi itauzwa kwa subsidized price? Hata TPDC walikua na mpango huo kusambaza gesi nafuu majumbani!!

Na haiwezekani gesi ikaisha ndani ya wiki huo sio ukweli kwa hesabu zako, so kuliko kukatishana tamaa tushauri namna ya TPDC kuwahisha huu mpango kuliko kuukejeli Mradi mzima.
 
Mbona hayo TPDC walishaongea kwamba wanampango wa kusambaza gesi majumbani kwa subsidized price!!

Maboresho lazima yatakuja lakini kuanza kupinga mtu kuhamasisha matumizi ya gesi ni ajabu sana.

Hata umeme enzi hizo unaletwa mara ya kwanza ulikua na gharama, in fact tulianza na majenereta huko bush linawashwa saa 12 hadi saa 4 usiku!! Lakini taratibu mambo yamebadilika na bei sio Ile ya miaka ya 90?

So kuliko kupinga kabisa mshauri njia nzuri zaidi ndio mjadala unakua na tija. Nakumbuka siku JPM anawasha umeme kwenye nyumba ya tembe mlimshangilia sana kwamba kavunja rekodi ila sikusikia mkiongelea gharama za Luku za kila mwezi kwa wananchi maskini!!! So tuache unafiki na tutoe support Ile Ile kwa huyu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Aisee, sikujua kama wewe pia una mtazamo wa kichawa namna hii
 
Wapi nimemsifia JPM Wala CCM? Mie Sipendi hii tabia ya wafuasi wa JPM kupinga Kila kitu Cha Samia sababu ya chuki ya kuondolewa madarakani.

Ndio maana nahoji kama mlikua mnashabikia JPM kuwasha umeme kwenye nyumba za Tembe kipi Cha ajabu watu wakipewa gesi vijijini?

Mie sijawahi ipenda CCM but sipendi zaidi unafiki wenu nyie Team JPM.
Kwa hiyo kumbe hapa hutetei hoja bali unamtetea Samia?
 
Kasome mpango wa taifa wa miaka 5 from 2016 na sasa 2021..... Pia Ilani ya hiko chama kiliahidi hivyo. Team JPM waache kujifanya wajuaji wakati hayo anayofanya January ndio JPM aliahidi kwenye Ilani.

Mie sio CCM ila kuna tabia imezuka ya wafuasi wa JPM kujaribu ku undermine Kila kinachofanyika Ili tuu legacy ikumbukwe whilst JPM huyo huyo aliwahi washa taa kwenye nyumba ya tembe kupitia kina Kalemani..... Na huo unafiki ndio naopinga hapa.
Sasa umeme unafananisha na gesi?
 
Mtoa mada anachuki mpaka anapoteza uelekoe na kutokuona kazi za Waziri, kazi sii mbwawa tu hata Gas inamhusu. Tuache hizi chuki hazitatufikisha mahali. Kuondolewa kwa Kalemani kumewaumiza sana nyie watu. ERA imepita pisheni na wengine wafanyekazi hakuna alie na hati miliki ya hii nchi.
 
JPM ndio alitaka energy mix kupitia Ilani ya 2020-25 sasa kosa la january ni nini?
Kwa akili yako energy mix inahusisha kugawa mitungi ya gesi kwa wananchi bila kuweka mipango na mikakati sahihi ya upatikanaji wa bei nafuu kwa hiyo gesi
 
Kweli Tanzania kuanzia viongozi mpaka wananchi hatueleweki na ndio maana vitu vya aibu vinafanyika. Kwani tusilamilishe jambo moja moja kwanza la muhimu na msingi ndipo mengine yafuate, ina maana kweli ni muhimu kugawa mitungi ya gesi kwa wananchi ambao ikishaisha hawawezi tena kuijaza itabaki tu ndani. Badala ya kumalizia Mirada ya nishati ambayo inaendelea kwanza, pili kuongeza Miradi mingine mipya ya nishati ili gharama za nishati zishuke maradufu na huyu mwananchi wa chini aweze kujinunulia mwenyewe huo mtungi na kuuhudumia.
Kiwango hiki cha ujinga tuna safari ndefu sana ya kuumaliza
 
Unampa mwananchi mtungi wa gesi. Kesho kutwa hana hata pesa ya kujazia gasi huo mtungi ukiisha.

Kwa nini msikomae JNHP ikakamilika alafu umeme ukashuka bei na bidhaa kushuka bei na maisha mwananchi yakawa nafuu.

[emoji116]Huu ni ulaghai usiofaa. View attachment 2289171
NCHI hii sijui itaisha lini MAIGIZO Umssikini wa hao Wananchi ni Mkubwa sana hata hizo KUNI wanaokoteza Mabua leo UNAGAWA mitungi ya GESI ni Akili au Matope?Mijini kuna Watumishi wa Umma wanalipwa Mishahara lakini bado wanatumia MKAA kupikia kutokana na KUSHINDWA kununua GESI
 
Unampa mwananchi mtungi wa gesi. Kesho kutwa hana hata pesa ya kujazia gasi huo mtungi ukiisha.

Kwa nini msikomae JNHP ikakamilika alafu umeme ukashuka bei na bidhaa kushuka bei na maisha mwananchi yakawa nafuu.

👇Huu ni ulaghai usiofaa. View attachment 2289171

Angalia hapo unagusa maslahi ya watu. 😗😗🇹🇿🇹🇿
 
Back
Top Bottom